Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Kuna vitu viwili. Predestination na Foreknowledge.

Predestination, ni kwamba yeye ameweka plan toka mwanzo kwamba amekuumba na uwezo wa kumfuata yeye. Na ikiwa umefail basi amekuwekea njia ya kujirekebisha.

Foreknowledge, hapa ni Mungu anakuona wewe mwaka 2000, mwaka 2022 na mwaka 2040 (kwa maana ya past, present and future). Anaona unachofanya nyakati zote za maisha yako. Sio kwamba amekupangia au anacontrol unachofanya bali anakuona. Yeye hafungwi na muda.
Sikutaka kuchangia hii mada ila kuna sehemu nimeona hamuelewani hapo ndipo nilipoona nafasi ya mimi kuweka dokezo katikati ya mjadala wenu

Naomba kujua dini yako?
 
Hiyo hoja dhaifu sana,inaonekana alikuwa anafanya rhetoric tu.
 
Sikutaka kuchangia hii mada ila kuna sehemu nimeona hamuelewani hapo ndipo nilipoona nafasi ya mimi kuweka dokezo katikati ya mjadala wenu

Naomba kujua dini yako?
Mkuu mimi hata sina dini, nina ushirika (fellowship) na Yesu Kristo. Dini wanazo wale wanaotafuta ukweli kuhusu yapi ni maelekezo sahihi ya Mungu.
 
Mkuu mimi hata sina dini, nina ushirika (fellowship) na Yesu Kristo. Dini wanazo wale wanaotafuta ukweli kuhusu yapi ni maelekezo sahihi ya Mungu.
Unatumia muongozo upi?

Maana wakristo hutumia bible?
 
Ndio kipo, kitabu kizuri sana katika kulijua nafasi yetu ndani ya Kristo, urithi tulionao na ushindi katika vita ya kiroho.
Sasa waefeso 1:11 inasema kila kitu kinafanyika kwa mipango ya Mungu na yeye ndio anayechagua yupi wakuungana naye

Swali langu ni kwamba

Ikiwa kama kila kitu ni mipango ya Mungu utasemaje tuna freewill?

Na kama tuna freewill kwanini kila kitu kiwe sehemu ya mipango yake?
 
Nakuwekea hapa waefeso 1:11 kutoka toleo la NKJV:

"In Him also we have obtained an inheritance, being predestined according to the purpose of Him who works all things according to the counsel of His will"

Kwa kiswahili

"Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake."

Unaliona neno predestined? Hapo ndio kila kitu kinaanzia. Hapo ndio kuna perfect will of God. Mungu anayo mawazo mema juu ya kila mtu anayemleta duniani. (Yeremia 29:11) Na anayo matendo ambayo kama ukiyafuata unalifikia kusudi lake (waefeso 2:10)

Sasa akiwa ameshaweka njia sahihi sawasawa na mapenzi yake anakuachia wewe uhuru wa kuchagua eidha umfuate au uache.

Kwahiyo free will unayo.
 
Huu mjadala naona ni kama issue ya Mafarisayo na Yesu. Mafarisayo wanafuatilia maongezi ya yesu, akiteleza neno kidogo....wanae.
 
Huu mjadala naona ni kama issue ya Mafarisayo na Yesu. Mafarisayo wanafuatilia maongezi ya yesu, akiteleza neno kidogo....wanae.
Kiranga anamsimamo kwamba yeye ni atheist. Sasa anapoonyesha inconsistencies with his beliefs ni muhimu kumsaidia ajue anachokipinga hakijui.
 
Hatari Sana mkuu,yaani nadharia zao ni Nonsense tabu hata wanaamini hizo nadharia hawajui ziliko anzia ila Sasa ni wabishi kama washawahi kumwona huyo Mungu,
Utasikia oooh Hilo ni swala la Imani yaani Mungu muweza wa yote anashindwaje kujidhihirisha pasipo shaka Kwa maelfu ya miaka ambayo waumini wake wameanza kumwabudu Huko wakiwa Hawana uhakika nae pamoja na mikanganyiko kibao ya kiimani na madhehebu Yao chungu mzima, huyo Mungu ana kiburi na jeuri ya Hali ya juu kajificha mafichoni tangu nadharia zake zianzishwe ila still wafuasi wake hawakomi kumfuata
Hahahahahah inafurahisha Sana aisee!
Mimi huwa nawauliza.

Suala la imani si lazima liwe kweli.

Unaweza kuamini hata uongo.

Sasa wanajuaje imani yao imejengwa kwenye ukweli, na haijajengwa kwenye uongo.
 
Kiranga anamsimamo kwamba yeye ni atheist. Sasa anapoonyesha inconsistencies with his beliefs ni muhimu kumsaidia ajue anachokipinga hakijui.
Ninachokipinga ni kipi? Na kwa nini sikijui? Na unawezaje kuthibitisha hilo?

Mimi nina belief gani? N aunajuaje hiyo ni belief? Inconsistency iko wapi?

Wewe unaposema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya, huoni inconsistency hapo? Huoni contradiction?
 
Ulitakiwa useme mapema kama hapakuwa na idhini. Umesubiria baada ya kushindwa hoja ndio unatoa matusi.

Matusi yako yamethibitisha akili yako ilivyo.
Wewe ngumbaru hata ukishindwa kuchamba vizuri ukala mavi na kupata kipindupindu utanilaumu mimi.

Nikikwambia ulitakiwa kuchamba baada ya kupata kipindupindu utasema nilitakiwa kukuambia ulitakiwa kuchamba.

Ujinga wako unanilaumu mimi.
 
Kwa aina hii ya majibu Sina shaka na destiny yako. Kuna siku utakumbuka kwamba Mungu aliendelea kukufundisha ukaamua kumpuuza.

Moderator msalimieni huyu.
Ulitaka mwenyewe sasa mod unawaita wa nini? Niliwaambia tangu mwanzo kuwa mtaishia pabaya ham kuamini.
Pambana na. Hali Acha kutafuta huruma ya mod
 
Ulitakiwa useme mapema kama hapakuwa na idhini. Umesubiria baada ya kushindwa hoja ndio unatoa matusi.

Matusi yako yamethibitisha akili yako ilivyo.
Kiranga sio wa. Kushindana nae humu maana hajawahi kukubali kushindwa.
 
Kwa aina hii ya majibu Sina shaka na destiny yako. Kuna siku utakumbuka kwamba Mungu aliendelea kukufundisha ukaamua kumpuuza.

Moderator msalimieni huyu.

kwanza Moderator ban topics za kum discredit member mwingine, amini unachoamini kama ni miti,tembo,sisimizi ila usitake kulazimisha wengine wafanane na wewe,lets learn from our differences and tolerate each other
 
Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao ujinga unawezekana kuwapo, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ujinga hauwezi kuwapo?
Unalazimisha kuhusisha kila kitu na ulimwengu tu, hiyo hoja uliyo ikariri ya kuhusu Mungu na huu ulimwengu imeshapitwa na wakati acha kuing'ang'ania. Wewe unadai hakuna Mungu unashindwa kueleza ni vp huyo Mungu hayupo unaishia tu kuhoji kwanini Mungu afanye hivi na sio vile?

Kubali tu hiyo hoja uliyoikariri ya contradiction haina mashiko tena.
 
Wewe ngumbaru hata ukishindwa kuchamba vizuri ukala mavi na kupata kipindupindu utanilaumu mimi.

Nikikwambia ulitakiwa kuchamba baada ya kupata kipindupindu utasema nilitakiwa kukuambia ulitakiwa kuchamba.

Ujinga wako unanilaumu mimi.

846a45dc2f6b35bcbe92b8aed2d9e8a5.jpg
 
Back
Top Bottom