Kirefu na maaana ya LLB

Kirefu na maaana ya LLB

Then mtahamia kwa engineers, scientists, computer system analysts, marubani, wahudumu wa ndege, koooote mtapita ili mradi tu ujemnge hoja kuwa fani/elimu yako ndo inafaa kuliko zingine.
 
Katika Kilatini kama neno liko katika wingi linafupishwa kwa kuiandika hiyo herufi mara mbili. mfano LL inamaanisha Laws, pp ni ufupisho wa pages in Latin

sasa nimeelewa, hasa hapo kwenye pp
shukran sana
 
Binafsi ni wakili na sababu ya Wanazuoni wa Taaluma ya Sheria kuitwa "Wasomi" ni mfumo tuliorithi kutoka kwa Mwingereza wa kuwaita wanasheria "learned brother/sister". Hili tunafundishwa kwenye somo linaitwa Legal Ethics tunaambiwa moja ya majukumu ya ethical practice ni kuheshimu na kutambua taaluma ya mwanazuoni mwenzako na tunawaita wasomi kama moja wapo ya recognition.
2. Kweli taaluma ya Law kwa sasa imepoteza ile heshima ya miaka ya nyuma ila sababu ni kuwa huko nyuma kwanza generally wasomi walikua wachache (katika fani almost zote), halafu Taasisi pekee iliyofundisha sheria ilikua moja tu (UDSM) baadae wakaja Mzumbe, then kulikua na kasumba kua Law ni fani ngumu, mwisho kabisa pia kuna ile "kasumba" ya Wanasheria kujivunia mno fani yao kua ni most Elite & Intellectual course ingawa mimi siamini hivyo.
Kwa sasa wasomi wa sheria ni wengi sana, vyuo pia vingi.
3. Anayesema sheria ni fani bora kuliko zote hii haijakaa sawa. Dunia ya leo inahitaji mjumuiko wa wataalam mbali mbali kufanikisha mambo. Sisi wanasheria tunawahutaji sana Forensic detectives kwenye kusolve criminal issues, tunawahitaji sana wahasibu na wakaguzi kuendesha biashara zetu (law firms), tunawahitaji sana madaktari kuweka afya zetu sawa tuweze kustand trial, tunawahitaji sana mainjinia atlist tuweke mawasiliano sawa na wateja wetu na kwa wakat.

Hizi ndizo hoja tunazoziitaji hapa jukwaani!!! Shukrani kwa mchango mzuri!!!! Mi nlijua wewe ni jasusi wa kiisrael katika kitengo cha kaidon ...(am jokin mkuu)...
 
Heshima kwako mkuu. Hii kitu kiingereza ni Bachelor in Legal Language

Bachelor of Laws (singular: lex/law - plural: legum/laws.) Vifupisho vya lugha ya kilatin hufanywa kwa ku-double first letters of a word which is in plural form eg "LL" for legum/laws na "pp" for pages.

Kuna mdau ametoa link ya google 2nd page fuatilia soma na uelewe.
 
Binafsi ni wakili na sababu ya Wanazuoni wa Taaluma ya Sheria kuitwa "Wasomi" ni mfumo tuliorithi kutoka kwa Mwingereza wa kuwaita wanasheria "learned brother/sister". Hili tunafundishwa kwenye somo linaitwa Legal Ethics tunaambiwa moja ya majukumu ya ethical practice ni kuheshimu na kutambua taaluma ya mwanazuoni mwenzako na tunawaita wasomi kama moja wapo ya recognition.

Twaib!

2. Kweli taaluma ya Law kwa sasa imepoteza ile heshima ya miaka ya nyuma ila sababu ni kuwa huko nyuma kwanza generally wasomi walikua wachache (katika fani almost zote),

Hiyo ni kweli au ni perceptions tu za watu?

halafu Taasisi pekee iliyofundisha sheria ilikua moja tu (UDSM) baadae wakaja Mzumbe,

Kuna wakati taasisi pekee iliyokuwa inatoa shahada ilikuwa ni UDSM.

then kulikua na kasumba kua Law ni fani ngumu,

Huwa nauliza kila mara humu ugumu wa sheria ni nini hasa? Maana wengine siye hatujawahi kuuona ugumu wake hata kidogo!!

mwisho kabisa pia kuna ile "kasumba" ya Wanasheria kujivunia mno fani yao kua ni most Elite & Intellectual course ingawa mimi siamini hivyo.

Unaweza walau kueleza ni kwa nini kuna hiyo kasumba? What's so intellectual about it? Is it too abstract?

Kwa sasa wasomi wa sheria ni wengi sana, vyuo pia vingi.

Hata wasomi wa fani zingine nao wameongezeka unless nawe uwe muumini wa hiyo dhana potofu kwamba wasomi ni wale walosomea sheria tu (wakati ukweli wa mambo mimi sioni kama wana usomi wowote ule).

3. Anayesema sheria ni fani bora kuliko zote hii haijakaa sawa. Dunia ya leo inahitaji mjumuiko wa wataalam mbali mbali kufanikisha mambo. Sisi wanasheria tunawahutaji sana Forensic detectives kwenye kusolve criminal issues, tunawahitaji sana wahasibu na wakaguzi kuendesha biashara zetu (law firms), tunawahitaji sana madaktari kuweka afya zetu sawa tuweze kustand trial, tunawahitaji sana mainjinia atlist tuweke mawasiliano sawa na wateja wetu na kwa wakat.

Hivi huko UDSM ndo mlidanganywa kuwa sheria ndo fani bora kuliko zote duniani? Kama sivyo, hiyo dhana potofu inatoka wapi? Ndo dhana inayoshikiliwa na wanasheria wa kibongo?
 
other exceptions ndo kama izo wanascience like doctors and engineer nao ni wasomi(learned)

University professors siyo wasomi?

Mwanasheria mwenye kishahada kimoja cha UDSM atakuwaje msomi kumzidi PhD wa agricultural economics ambaye anafanya kazi Bank of America, kwa mfano?
 
Kilichonichukiza kuhusu huyo ODILI SAMALU ni pale alipoonyesha utovu wa nidhamu, dharua na kujifanya kujua katika kujaribu kujenga/kujibu hoja yake (dhidi ya MwanaJF, if I'm not wrong, Nyani Ngabu, whose michango na hoja zake are quite handsome always).

Thank you, kindly, my friend. I'm humbly humbled by your nice compliment.

We shouldn't let these harum-scarum types get us off track. I applaud your condemnation of such behavior.
 
Twaib!

Hiyo ni kweli au ni perceptions tu za watu?

Kuna wakati taasisi pekee iliyokuwa inatoa shahada ilikuwa ni UDSM.

Huwa nauliza kila mara humu ugumu wa sheria ni nini hasa? Maana wengine siye hatujawahi kuuona ugumu wake hata kidogo!!

Unaweza walau kueleza ni kwa nini kuna hiyo kasumba? What's so intellectual about it? Is it too abstract?

Hata wasomi wa fani zingine nao wameongezeka unless nawe uwe muumini wa hiyo dhana potofu kwamba wasomi ni wale walosomea sheria tu (wakati ukweli wa mambo mimi sioni kama wana usomi wowote ule).

Hivi huko UDSM ndo mlidanganywa kuwa sheria ndo fani bora kuliko zote duniani? Kama sivyo, hiyo dhana potofu inatoka wapi? Ndo dhana inayoshikiliwa na wanasheria wa kibongo?

Nyani Ngabu kwanza nikisema ww ni mkorofi by nature tu ntakua sijakosea. Hii ni Kwasababu zifuatazo huku nikijibu hoja zako.
1. Kwanza kusema zaman wasomi walikua wachache hii ni kweli wala sio swala la parception za watu.
2. Mimi sijasema sheria ni ngumu nimetumia neno "kasumba" au "dhana" waliyokua nayo watu kuwa sheria ni ngumu... Sasa kama hujui maana ya kasumba kwann usiulize? Hii ni evidence tosha kua ungepata elimu ya sheria ungekua makini sasa unaiponda taaluma halafu inakuumbua hapo hapo.
3. Unaposema nieleze whats so special about kasumba ya kua law ni intellectual unakua coward in a way kwamba kasumba ni "dhana" is like a myth it doesnt exist at all sasa mi ntakuelezeaje kitu kisicho exist..?? Ndio maana nkasema ni kasumba cz mimi siioni Sheria kua ni special kuliko fani nyngne na nimesema hivyo wazi ingawa mi binafsi ni wakili.
4. Mimi sijasema kua wasomi wa fani nyngne hawaja ongezeka nimesema wasomi wa sheria wameongezeka kwa sababu aliyeuliza alitaka kujua kwann hadhi ya wasomi wa sheria imeshuka.. Sasa ww kuniita muumini wa dhana potofu kua wasomi ni wanasheria tu huu ni ukorofi na upuuzi ambao hata sijui sababu yake hasa ni nini..?? Narudia.. ungetukiza akili yako ukaja hapa kisomi wala usingenishutumu na huu upumba.vu.
5. Mimi sijasoma UDSM na wala sijasema sheria ni fani bora nimesema wazi kabisa kusema sheria ni fani bora kuliko nyngne hilo halijakaa sawa. Ajabu ww umegeuza maneno yangu ili tu tuzue ntafaruku it looks ckearly ww ni mkorofi na unapenda shari cz hunijui wala hatufahamiani unaanza kubwatuka nimesoma UDSM huu ni upumbav.u wa wazi wazi kbsa. Ila kuonyesha kua ww ni mpumbav.u zaidi unaikashifu fani ambayo inakuumbua hapo hapo. Ingekua mahakamani hapa kwa hoja zangu ww wanakunyonga mpka kufa. Nataman sana nikujue bwana mdgo na tukutane mahakaman.
 
Nyani Ngabu kwanza nikisema ww ni mkorofi by nature tu ntakua sijakosea.

Ni mkorofi kiasi, siyo sana. Hivyo hujakosea kabisa, umepatia kiasi.

Hii ni Kwasababu zifuatazo huku nikijibu hoja zako.

Haya, twende kazi, ,mstari kwa mstari, hoja kwa hoja, na hata viroja kwa viroja.

1. Kwanza kusema zaman wasomi walikua wachache hii ni kweli wala sio swala la parception za watu.

Hilo ni kweli na ninakiri kuwa nilikosea katika kuuliza. Lengo langu halikuwa kuhoji ukweli wa wingi wa wasomi kati ya zama hizi na zile za zamani.

Kwa hiyo upo sahihi, kwamba zamani wasomi wa fani zote nchini Tanzania walikuwa wachache.

Hapo kwenye perceptions nilinuia kulenga zaidi kwenye taaluma ya sheria kupoteza heshima yake ya miaka ya nyuma (kama ulivyodai wewe) kulinganisha na hivi sasa.

Ndo sababu ya mimi kuuliza kuwa ni kweli hiyo taaluma imepoteza heshima au ni perceptions tu za watu? Hivyo hapo nakubali kosa, ilinipasa niwe mahsusi zaidi katika swali langu.

2. Mimi sijasema sheria ni ngumu nimetumia neno "kasumba" au "dhana" waliyokua nayo watu kuwa sheria ni ngumu...

Mbona hata mimi sijasema kuwa wewe umesema kuwa sheria ni ngumu! Kama ukituliza hisia na kurudi tena kusoma kwa utulivu nilichokiandika nadhani utakubaliana nami kuwa hicho nilichokiandika kilikuwa kinaunga mkono mtazamo wako huo.

Sasa kama hujui maana ya kasumba kwann usiulize?

Nadhani hapo umepaniki bure tu pasipo hata na sababu yoyote ile ya msingi. Hebu rudi tena upasome hapo nilipoandika mimi na ambapo wewe umepanukuu.

Mimi mimeandika kwa mtindo wa rhetorical question ambapo dhumuni lilikuwa ni kuunga mkono kile ulichokiandika wewe kuhusu kasumba ya ugumu wa masomo ya sheria na sikuuliza kwa dhumuni la kutaka kujibiwa.

Hii ni evidence tosha kua ungepata elimu ya sheria ungekua makini

Aaah sasa miye mbeba maboksi na kusomea sheria wapi na wapi bana? Sijawahi hata siku moja kudai humu kuwa nimesomea sheria mimi. Sina uwezo wa kiakili wa kuwa kaka msomi kama ulivyo wewe na wengineo. Nimeishia kidato cha nne tu mimi.

sasa unaiponda taaluma halafu inakuumbua hapo hapo.

Nimeiponda hiyo taaluma kivipi na imeniumbuaje?

3. Unaposema nieleze whats so special about kasumba ya kua law ni intellectual unakua coward in a way kwamba kasumba ni "dhana" is like a myth it doesnt exist at all sasa mi ntakuelezeaje kitu kisicho exist..??

Hmm...mbona ghadhabu nyingi kaka? Unajua ghadhabu huwa zina uwezo wa kufunika kabisa umakini wa mtu na hapa naona ndicho kilichotokea.

Mimi nilichokuomba unieleze ni kwa nini kuna hiyo kasumba. Na kama umenisoma kwa umakini basi utakuwa umegundua kwamba hapo uliponinukuu kuna maswali matatu ambayo yanahusiana.

Sawa, hata kama kasumba ni sawa na usasili (myth), lakini kama kuna watu ambao wana kasumba fulani fulani ni lazima hizo kasumba ziwe na chanzo. Haziweki tu kujitokeza kwa watu bila sababu.

Sasa, ni bora hata ungesema hujui chanzo chake ni nini kuliko kuanza kunishambulia kwa kuniita "coward". Ni uungwana unapoulizwa jambo, kama hulijui, unasema sijui. Lakini siyo kuanza kunishambulia kwa kuniita majina. Huo si uungwana hata kidogo.

Kwa hiyo, mimi sikusema kwamba unieleze. Nilikuuliza kama unaweza kueleza kwa nini kuna hiyo kasumba. Kuna tofauti kubwa tu kati ya kusema na kuuliza. Au alama za kuuliza hukuziona?

Ndio maana nkasema ni kasumba cz mimi siioni Sheria kua ni special kuliko fani nyngne na nimesema hivyo wazi ingawa mi binafsi ni wakili.

Baada ya mimi kuona wewe umesema hivyo, ndo nami nikauliza kwa nini kuna hiyo kasumba? Hukuwa na haja ya kunishambulia mimi kwa hasira. Ungesema tu hujui (kama hujui), basi. Lakini badala ya kufanya hivyo umenishambulia mimi. Hewala bwana.

4. Mimi sijasema kua wasomi wa fani nyngne hawaja ongezeka nimesema wasomi wa sheria wameongezeka kwa sababu aliyeuliza alitaka kujua kwann hadhi ya wasomi wa sheria imeshuka..

Mbona umekaa mkao wa kujihami hami sana kana kwamba mimi nimekushutumu wewe kusema wasomi wa fani zingine hawajaongezeka? Nilichoandika mimi kilipanua tu kile ulichoandika wewe. Kuna kosa hapo?

Sasa ww kuniita muumini wa dhana potofu kua wasomi ni wanasheria tu huu ni ukorofi na upuuzi ambao hata sijui sababu yake hasa ni nini..??

Hapana kaka, mimi sijakuita hivyo hata kidogo. Ningeandika wewe ni "muumini wa hiyo dhana potofu kwamba wasomi ni wale walosomea sheria tu" basi ungekuwa na hoja. Lakini kwa kutumia neno 'unless' (sina hakika na tafsiri yake kwa Kiswahili katika huu muktadha) maana nzima ya sentensi ni sivyo ulivyoichukulia wewe.

Lakini sasa huna hoja kwa sababu (1) hujaonyesha umakini wowote ule katika kusoma na kuelewa nilichokiandika na hivyo kupelekea kufikia hitimisho ambalo linamakosa na (2) hakuna ukorofi wala upuuzi wowote ule katika nilichokiandika na kama upo basi ni wa kufikirika tu.

Narudia.. ungetukiza akili yako ukaja hapa kisomi wala usingenishutumu na huu upumba.vu.

Nadhani ingekuwa ni vyema na busara kwa wewe kuanza kuufanyia kazi kwanza huu ushauri wako kabla hujaanza kuutoa kwa wengine. Unaonaje?

5. Mimi sijasoma UDSM

Hata mimi sijasema kuwa umesoma UDSM lakini nakiri kosa kwa kudokeza kuwa ulisoma hapo. Niwie radhi kwa hilo.

na wala sijasema sheria ni fani bora nimesema wazi kabisa kusema sheria ni fani bora kuliko nyngne hilo halijakaa sawa.

Mbona hata mimi sijasema kuwa wewe umesema hivyo. Kwa sababu jinsi unavyojihami unatoa taswira ya kana kwamba mimi nimesema kuwa wewe umesema hivyo. La hasha ndugu.

Ajabu ww umegeuza maneno yangu ili tu tuzue ntafaruku it looks ckearly ww ni mkorofi na unapenda shari cz hunijui wala hatufahamiani unaanza kubwatuka nimesoma UDSM huu ni upumbav.u wa wazi wazi kbsa.

Wapi nimegeuza maneno yako ili kwa lengo la kuzua tafrani? Hilo la UDSM nimeomba radhi na nimekiri kosa langu. Punguza jazba ndugu. Sawa?

Ila kuonyesha kua ww ni mpumbav.u zaidi unaikashifu fani ambayo inakuumbua hapo hapo.

Nimeikashifu fani wapi? Na wewe kuniita mimi mpumba.vu bila kuonyesha wapi nimeikashifu hiyo fani na bila kuonyesha hiyo fani imeniumbua vipi, sijui hata nikuiteje aisee!!

Ingekua mahakamani hapa kwa hoja zangu ww wanakunyonga mpka kufa. Nataman sana nikujue bwana mdgo na tukutane mahakaman.

You don't want to meet me anywehere in a court of law with your kind of elementary comprehension level and rudimentary arguing skills.

I'll eat your lunch, brother-man!
 
Ni mkorofi kiasi, siyo sana. Hivyo hujakosea kabisa, umepatia kiasi.

Kama unajijua we mkorofi bas jaribu kufanya ukorofi na mtu unayemfaham itakusaidia zaid. Ushauri tu..!!

Haya, twende kazi, ,mstari kwa mstari, hoja kwa hoja, na hata viroja kwa viroja.

Hilo ni kweli na ninakiri kuwa nilikosea katika kuuliza. Lengo langu halikuwa kuhoji ukweli wa wingi wa wasomi kati ya zama hizi na zile za zamani.

Kwa hiyo upo sahihi, kwamba zamani wasomi wa fani zote nchini Tanzania walikuwa wachache.

Nashukuru kwa kukiri kosa.

Hapo kwenye perceptions nilinuia kulenga zaidi kwenye taaluma ya sheria kupoteza heshima yake ya miaka ya nyuma (kama ulivyodai wewe) kulinganisha na hivi sasa.

Ndo sababu ya mimi kuuliza kuwa ni kweli hiyo taaluma imepoteza heshima au ni perceptions tu za watu? Hivyo hapo nakubali kosa, ilinipasa niwe mahsusi zaidi katika swali langu.

Mbona hata mimi sijasema kuwa wewe umesema kuwa sheria ni ngumu! Kama ukituliza hisia na kurudi tena kusoma kwa utulivu nilichokiandika nadhani utakubaliana nami kuwa hicho nilichokiandika kilikuwa kinaunga mkono mtazamo wako huo.

Nadhani hapo umepaniki bure tu pasipo hata na sababu yoyote ile ya msingi. Hebu rudi tena upasome hapo nilipoandika mimi na ambapo wewe umepanukuu.

Mimi mimeandika kwa mtindo wa rhetorical question ambapo dhumuni lilikuwa ni kuunga mkono kile ulichokiandika wewe kuhusu kasumba ya ugumu wa masomo ya sheria na sikuuliza kwa dhumuni la kutaka kujibiwa.

Inshallah kama ulimaanisha hivyo.

Aaah sasa miye mbeba maboksi na kusomea sheria wapi na wapi bana? Sijawahi hata siku moja kudai humu kuwa nimesomea sheria mimi. Sina uwezo wa kiakili wa kuwa kaka msomi kama ulivyo wewe na wengineo. Nimeishia kidato cha nne tu mimi.

Ajabu useme ugumu wa sheria hujawahi uona halaf hapa unajitangaza form 4 mara mbeba boksi mi sijauliza unacho fanya alafu nlifikiri ukiwa sensible enough utasema ulisoma japo ABC za sheria ndio ukaiona unyanya wake.. Kumbe uliongea out of blue? Sasa kama unajijua we mbeba maboksi form 4 how comes useme hujawahi uona ugumu wa fani usiyo ijua..??

Nimeiponda hiyo taaluma kivipi na imeniumbuaje?

Kwa wewe kusema huwaoni wanasheria kuwa wasomi huku ni kuiponda taaluma..!! Huu utaratibu wa kuwaita wanasheria wasomi sio majigambo hizi ethical rules katika legal practice Judge anaitwa Lord/Lorship, Advocate anaitwa Msomi, Magistrate anaitwa Honour (mheshimiwa) huu ni utaratibu tu unao exists katika ulimwengu wa Wanasheria.
Halafu kwa kua ww ni form 4 then unasema huuoni ugumu wa sheria bas utakua unatuletea dhihaka hapa huku pia ni kuiponda taaluma utabisha..??

Hmm...mbona ghadhabu nyingi kaka? Unajua ghadhabu huwa zina uwezo wa kufunika kabisa umakini wa mtu na hapa naona ndicho kilichotokea.

Mimi nilichokuomba unieleze ni kwa nini kuna hiyo kasumba. Na kama umenisoma kwa umakini basi utakuwa umegundua kwamba hapo uliponinukuu kuna maswali matatu ambayo yanahusiana.

Kuilezea hiyo kasumba binafsi ntakudanganya sina majibu. Nimeikuta nimeicha sikuifuatilia nlichofuata ni elimu na nnachojua hiyo kasumba sio kweli.

Sawa, hata kama kasumba ni sawa na usasili (myth), lakini kama kuna watu ambao wana kasumba fulani fulani ni lazima hizo kasumba ziwe na chanzo. Haziweki tu kujitokeza kwa watu bila sababu.

Sasa, ni bora hata ungesema hujui chanzo chake ni nini kuliko kuanza kunishambulia kwa kuniita "coward". Ni uungwana unapoulizwa jambo, kama hulijui, unasema sijui. Lakini siyo kuanza kunishambulia kwa kuniita majina. Huo si uungwana hata kidogo.

Niwie radhi kwa hilo

Kwa hiyo, mimi sikusema kwamba unieleze. Nilikuuliza kama unaweza kueleza kwa nini kuna hiyo kasumba. Kuna tofauti kubwa tu kati ya kusema na kuuliza. Au alama za kuuliza hukuziona?

Baada ya mimi kuona wewe umesema hivyo, ndo nami nikauliza kwa nini kuna hiyo kasumba? Hukuwa na haja ya kunishambulia mimi kwa hasira. Ungesema tu hujui (kama hujui), basi. Lakini badala ya kufanya hivyo umenishambulia mimi. Hewala bwana.

Niwie radhi kwa hilo

Mbona umekaa mkao wa kujihami hami sana kana kwamba mimi nimekushutumu wewe kusema wasomi wa fani zingine hawajaongezeka? Nilichoandika mimi kilipanua tu kile ulichoandika wewe. Kuna kosa hapo?

Hapana kaka, mimi sijakuita hivyo hata kidogo. Ningeandika wewe ni "muumini wa hiyo dhana potofu kwamba wasomi ni wale walosomea sheria tu" basi ungekuwa na hoja. Lakini kwa kutumia neno 'unless' (sina hakika na tafsiri yake kwa Kiswahili katika huu muktadha) maana nzima ya sentensi ni sivyo ulivyoichukulia wewe.

Unles kwa kiswahili fasaha tunasema "labda" sasa kama umeweza kuuliza kwenye kasumba kwanini usiulize hapa kama mimi ni mmoja wao wa hiyo dhana na mrengo wangu nimeueleza wazi kbsa ..??

Lakini sasa huna hoja kwa sababu (1) hujaonyesha umakini wowote ule katika kusoma na kuelewa nilichokiandika na hivyo kupelekea kufikia hitimisho ambalo linamakosa na (2) hakuna ukorofi wala upuuzi wowote ule katika nilichokiandika na kama upo basi ni wa kufikirika tu.

Nadhani ingekuwa ni vyema na busara kwa wewe kuanza kuufanyia kazi kwanza huu ushauri wako kabla hujaanza kuutoa kwa wengine. Unaonaje?

Kama unaona kuna eneo umekiri kosa bas ulichoandika hapa kitakucheleweshea maendeleo ila kama unafikiri hukuomba radhi bas mimi nitakuwa wa kwanza kuufanyia huu ushauri.

Hata mimi sijasema kuwa umesoma UDSM lakini nakiri kosa kwa kudokeza kuwa ulisoma hapo. Niwie radhi kwa hilo.

Nashukuru kwa Kukiri kosa.

Mbona hata mimi sijasema kuwa wewe umesema hivyo. Kwa sababu jinsi unavyojihami unatoa taswira ya kana kwamba mimi nimesema kuwa wewe umesema hivyo. La hasha ndugu.

Inshallah kama hukumaanisha hivyo.

Wapi nimegeuza maneno yako ili kwa lengo la kuzua tafrani? Hilo la UDSM nimeomba radhi na nimekiri kosa langu. Punguza jazba ndugu. Sawa?

Nimeikashifu fani wapi? Na wewe kuniita mimi mpumba.vu bila kuonyesha wapi nimeikashifu hiyo fani na bila kuonyesha hiyo fani imeniumbua vipi, sijui hata nikuiteje aisee!!

Sasa kama wewe form 4 unaanzaje kusema huwaoni wanasheria kama wasomi..??
Unaanzaje kudai hujawahi kuuona ugumu wa sheria ilhali huna background yoyote..??

You don't want to meet me anywehere in a court of law with your kind of elementary comprehension level and rudimentary arguing skills.

I'll eat your lunch, brother-man!

Kama myn is elementary hii yako tuiiteje sema mwenyewe manake sitaki kukuomba radhi baadae.
 
Duh! Hivi hujui namna ya kunukuu? Nina shauku ya kukujibu lakini hata sijui pa kuanzia.
 
Wa kuilaumu hpa ni Samsung sio mimi..

Haya, tuilamu Samsung basi.

Ila, kama ukipata muda jaribu basi kufanya marekebisho ili niweze kupata fursa nzuri ya kuziponda ponda na kuzivunjilia mbali hizo hoja zako dhaifu. Sawa?
 
Haya, tuilamu Samsung basi.

Ila, kama ukipata muda jaribu basi kufanya marekebisho ili niweze kupata fursa nzuri ya kuziponda ponda na kuzivunjilia mbali hizo hoja zako dhaifu. Sawa?

In ur dreams.. its allowed!
 
Back
Top Bottom