Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
DC katika mambo magumu ni kutaka kumuelewesha mtu mwenye hisia tofauti kwako. Mimi kama Carol siwezi ishi na mtu ambaye ni kero kwangu, sina hisia nae, amenidhalilisha kwa namna moja au nyingine. Kuishi ni kuchagua jinsi gani uendeshe maisha yako wewe kama wewe. Ukianza kuangalia nini community inavyokuchukulia nafikiri utakuwa unapoteza muda wako.
Binadamu ana kawaida ya kufanya kila wazo lake analofikiria kwa mtu au kwake mwenyewe kuwa sahihi. Ebu DC nenda pale mtaa wa OHIYO waulize kwa nini wanasimama pale. Kila mmoja akianza kukupa historia ya maisha yake utalia machozi. Ila tayari kabla ya kujua nini tatizo lao, mlishawapachika majina mengi tu (malaya, Changudoa, maharage ya mbeya etc).
Kila kitu kia sababu siyo wote wanafanya vitu fulani kwa utashi wao wenyewe ni hali tu.
DC mimi nina mkakati naomba Mungu anijalie pumzi. JE Saccos ikikaa vizuri, nitaenda kutembeea wale wadada mtaa wa OHIYO, OYTERBAY na kwingineko. Nikae niongee nao nione wale wenye utashi wa kuacha na kufanya bishara basi tutawasiaidi kwa njia hiyo uone kama kutakuwa na malaya yoyote mji huu.
Wale wenye mguso kwa hili ebu tukamatane mikono kuwasaidia wenzetu, ile hali hawaipendi hawana jinsii. Ukona wewe unakula na kushiba mshukuru Mungu kuna watu kula kwao ni tabu, inafikia hatua anaamua kwenda kufanya vitu ambavyo sivyo. haya kwa wale wenye kukerwa na tabia hiyo na hizi NAME CALLING ziishe. Vitu vingine havihitaji PESA ni roho ya kuona mateso ya wengine na kuwasaidia. Kuna makanisa wana moyo wa kusaidia ila hawa watu hawawezi kujipeleka wenyewe huko wanahitaji watu wa kuwashawishi mpaka wafike huko. Na wewe ni mmoja wapo lets try this.
Ni mpango mzuri ila uwe tayari kwamba katika hao utaokusanya, kutakuwa na baadhi ambao hawawezi kuacha hiyo kitu hata ukiwapa milioni ngapi. Hata hivyo ni muhimu kuwasaidia wale ambao kweli wanahitaji msaada.
I can guarantee you my support!
Asante sana, nina uhakika kwamba wengii hawapendi kuwa hivyo walivyo ni matatizo. kwa wale wenye mapenzi na hiyo kazi basi wao wataendelea lakini wale wenye moyo basi tutawapeleka kunako.
Mimi nina uhakika 100% na nitakutafuta kukwambia ni kiasi gani nimefanikiwa.