Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaependa kuzurura sana....na wakati mwingine inatumika kumtambulisha mtu ambae ni mhuni (anaehama toka kwa mwanamke/mwanaume mmoja kwenda kwa mwingine kila mara).
Kwahiyo ni mtu asiyetulia sehemu moja iwe kimahusiano au kimazingira!!
Ahsante mkuu...natumai na wewe ni mmoja wao!
kuwa na mapepe... kutotulia... mcharuko.... fujo.... muhuni... mzurulaji..etc
May be..
Ila nimekutana na jambo ambalo limenifanya nipate msinyao wa ubongo..
Hivi mwanamume akio mke wa kwanza ila akakuta mama mwenyewe ni Tyson..kila siku baba hakosi vinundu usoni. Akaamua kubwaga manyanga na kumpata namba 2..huko nako akukana na moto wa aina nyingine...huyoooo akang'atuka kiaina na kupata namba 3....Labda bahati pia ikawa mbaya na huyo akawa si riziki!!
Au mdada wa watu ambaye ailiuvaa mkenge na kuolewa na jamaa mwenye wake 2 (yeye wa 3) kwa sababu hakumueleza ukweli...Baada ya vitimbi kibao naye akaamua kupanda dala dala ya 2...Hivyo hivyo hadi anafikia chuo cha 4 au 5 (married to 4 or 5 different men)!!!
Hawa watu wana-qualify kuitwa viruka njia???