Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Watu wanapozongwa na dhahma za wanasiasa hutafuta mambo ya kuwachekesha.
Vichekesho hivi wanavitengeneza kutoka kwa wanasiasa wenyewe kiasi kwamba wenyewe wanasiasa vichekesho hivi vinapowafikia na wao pia huangua vicheko wakacheka.
Abdel Nasser aliwaandama sana Ikhwan Muslimin (Ndugu Waislam) hadi akamuua kiongozi wao Hassan al Bana.
Baada ya Misri kushindwa vibaya sana katika vita vya mwaka wa 1967 dhidi ya Israel pakawa na msuguano mkubwa ndani ya serikali na ndani ya jeshi la Misri na pia baina ya serikali ya Nasser na jeshi.
Zilizuka lawama nyingi kwa mkuu wa majeshi Abdel Hakim Amer kwa kushindwa kwa Misri katika vita ile.
Haikupita hata miezi mitatu Abdel Hakim Amer akajiua na wengine wanasema aliuliwa.
Ikhwan wakawa sasa wamepata jambo la kulifanyia mzaha na tashtiti.
Wakawa wanasema Abdel Hakim alipokuwa kaburini malaika Munkar wa Nakir walifika kumuuliza maswali kama ilivyo ada, "Nani Mungu wako?"
Ikwan wakawa wanasema kuwa Abdel Hakim aliwajibu kuwa Mungu wake ni Gamal Abdel Nasser.
Malaika wajarejea kwa Allah kumpa jibu la Abdel Hakim.
Allah akawaamuru waende tena kwa Abdel Hakim wakamuulize swali lile kwa mara ya pili.
Abdel Hakim hakubadilisha jibu lake akasema, "Mimi Mungu wangu ni Nasser."
Malaika wale wakarudi kwa Allah kutoa jibu la Abdel Hakim.
Allah akawaambia waende tena wakamuulize.
Hii ikawa ni mara ya tatu.
Safari hii Munkar wa Nakir wakamwingilia Abdel Hakim Amer kaburini kwake wameghadhibika wakamuuliza kwa ukali sauti inavuma kama radi, "Nani Mola wako?"
Abdel Hakim akaogopa.
"Ndugu zangu hebu tulieni kwani nyie mnatoka wapi nani kakutumeni kwangu?"
Abdel Hakim akauliza.
Munkar wa Nakir wakamjibu wakamwambia, "Sisi tunatoka kwa Allah yeye ndiye aliyetutuma kwako."
Abdel Hakim Ameir akasema, "Mbona hamkuniambia toka mwanzo?
Mimi nilidhani nyie askari wa Nasser mmekuja kunipeleleza.
Mimi Mungu wangu ni Allah."
Wanaujua ukweli kama alivyokuwa anaujua Abdel Hakim Amer.
Wakati na muda ukifika aliopanga Allah watakiri ukweli.
Kama hizi mfano wa kichekesho hiki Ikhwan Muslimin wanazo tele.
Utake usitake utacheka.
Picha kulia ni Nasser na kushoto ni Abdel Hakim Amer.