Kisa cha Abdel Hakim Amer na Gamal Abdel Nasser

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Watu wanapozongwa na dhahma za wanasiasa hutafuta mambo ya kuwachekesha.

Vichekesho hivi wanavitengeneza kutoka kwa wanasiasa wenyewe kiasi kwamba wenyewe wanasiasa vichekesho hivi vinapowafikia na wao pia huangua vicheko wakacheka.

Abdel Nasser aliwaandama sana Ikhwan Muslimin (Ndugu Waislam) hadi akamuua kiongozi wao Hassan al Bana.

Baada ya Misri kushindwa vibaya sana katika vita vya mwaka wa 1967 dhidi ya Israel pakawa na msuguano mkubwa ndani ya serikali na ndani ya jeshi la Misri na pia baina ya serikali ya Nasser na jeshi.

Zilizuka lawama nyingi kwa mkuu wa majeshi Abdel Hakim Amer kwa kushindwa kwa Misri katika vita ile.

Haikupita hata miezi mitatu Abdel Hakim Amer akajiua na wengine wanasema aliuliwa.

Ikhwan wakawa sasa wamepata jambo la kulifanyia mzaha na tashtiti.

Wakawa wanasema Abdel Hakim alipokuwa kaburini malaika Munkar wa Nakir walifika kumuuliza maswali kama ilivyo ada, "Nani Mungu wako?"

Ikwan wakawa wanasema kuwa Abdel Hakim aliwajibu kuwa Mungu wake ni Gamal Abdel Nasser.

Malaika wajarejea kwa Allah kumpa jibu la Abdel Hakim.

Allah akawaamuru waende tena kwa Abdel Hakim wakamuulize swali lile kwa mara ya pili.

Abdel Hakim hakubadilisha jibu lake akasema, "Mimi Mungu wangu ni Nasser."

Malaika wale wakarudi kwa Allah kutoa jibu la Abdel Hakim.

Allah akawaambia waende tena wakamuulize.

Hii ikawa ni mara ya tatu.

Safari hii Munkar wa Nakir wakamwingilia Abdel Hakim Amer kaburini kwake wameghadhibika wakamuuliza kwa ukali sauti inavuma kama radi, "Nani Mola wako?"

Abdel Hakim akaogopa.

"Ndugu zangu hebu tulieni kwani nyie mnatoka wapi nani kakutumeni kwangu?"

Abdel Hakim akauliza.

Munkar wa Nakir wakamjibu wakamwambia, "Sisi tunatoka kwa Allah yeye ndiye aliyetutuma kwako."

Abdel Hakim Ameir akasema, "Mbona hamkuniambia toka mwanzo?

Mimi nilidhani nyie askari wa Nasser mmekuja kunipeleleza.

Mimi Mungu wangu ni Allah."

Wanaujua ukweli kama alivyokuwa anaujua Abdel Hakim Amer.

Wakati na muda ukifika aliopanga Allah watakiri ukweli.

Kama hizi mfano wa kichekesho hiki Ikhwan Muslimin wanazo tele.

Utake usitake utacheka.

Picha kulia ni Nasser na kushoto ni Abdel Hakim Amer.

Screenshot_20201127-091201.jpg
Screenshot_20201127-091548.jpg
 
iasee na mim nimecheka sana
hao watu kwanza muda wa kukuuliz amara tatu tatu utoke wapi ni kipondo heavy tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Julaibibi,
Hao Ikwan wanatengeneza vichekesho kuwafanya viongozi wajione vichekesho.
Ukimsoma Mohamed Haikal anavyomnanga Anwar Sadat utachoka!

Hapa unaona wewe unacheka.

Sasa utacheka zaidi.

Kuna version nyingine wanasema kuwa Munkar wa Nakir walikwenda kwa Allah kupeleka taarifa za Abdel Hakim kuwa ni mtu jeuri anajibu maswali kefedhuli Allah akaagiza aletwe kwake.

Munkar wa Nakir wakamwambia Allah kuwa huyu ni mtu hatari hawawezi kumleta kwake,
Allah akawaamuru waimarishe ulinzi wake!

Subahanallah!
Allah aongezewe ulinzi kabla Abdel Hakim hajapelekwa kwake!

Alipofikiwa kwake Allah akamuuliza, ''Nani Mola wako Abdel Hakim Amer.''
Abdel Hakima akajibu, ''Allah.''

Baada ya hapo Abdel Hakim akamwambia Allah kuwa yeye akimuogapa sana Nasser sasa alikuwa na wasiwasi kuwa Munkar wa Nakir ni watu wa usalama wa Nasser wametumwa kumpeleleza.

Tunacheka lakini haya mambo ukiyaleta katika hali zinazowakabili wanasiasa wetu hakika utawahurumia.
 
Watu wanapozongwa na dhahma za wanasiasa hutafuta mambo ya kuwachekesha.

Vichekesho hivi wanavitengeneza kutoka kwa wanasiasa wenyewe kiasi kwamba wenyewe wanasiasa vichekesho hivi vinapowafikia na wao pia huangua vicheko wakacheka.

Abdel Nasser aliwaandama sana Ikhwan Muslimin (Ndugu Waislam) hadi akamuua kiongozi wao Hassan al Bana.

Baada ya Misri kushindwa vibaya sana katika vita vya mwaka wa 1967 dhidi ya Israel pakawa na msuguano mkubwa ndani ya serikali na ndani ya jeshi la Misri na pia baina ya serikali ya Nasser na jeshi.

Zilizuka lawama nyingi kwa mkuu wa majeshi Abdel Hakim Amer kwa kushindwa kwa Misri katika vita ile.

Haikupita hata miezi mitatu Abdel Hakim Amer akajiua na wengine wanasema aliuliwa.

Ikhwan wakawa sasa wamepata jambo la kulifanyia mzaha na tashtiti.

Wakawa wanasema Abdel Hakim alipokuwa kaburini malaika Munkar wa Nakir walifika kumuuliza maswali kama ilivyo ada, "Nani Mungu wako?"

Ikwan wakawa wanasema kuwa Abdel Hakim aliwajibu kuwa Mungu wake ni Gamal Abdel Nasser.

Malaika wajarejea kwa Allah kumpa jibu la Abdel Hakim.

Allah akawaamuru waende tena kwa Abdel Hakim wakamuulize swali lile kwa mara ya pili.

Abdel Hakim hakubadilisha jibu lake akasema, "Mimi Mungu wangu ni Nasser."

Malaika wale wakarudi kwa Allah kutoa jibu la Abdel Hakim.

Allah akawaambia waende tena wakamuulize.

Hii ikawa ni mara ya tatu.

Safari hii Munkar wa Nakir wakamwingilia Abdel Hakim Amer kaburini kwake wameghadhibika wakamuuliza kwa ukali sauti inavuma kama radi, "Nani Mola wako?"

Abdel Hakim akaogopa.

"Ndugu zangu hebu tulieni kwani nyie mnatoka wapi nani kakutumeni kwangu?"

Abdel Hakim akauliza.

Munkar wa Nakir wakamjibu wakamwambia, "Sisi tunatoka kwa Allah yeye ndiye aliyetutuma kwako."

Abdel Hakim Ameir akasema, "Mbona hamkuniambia toka mwanzo?

Mimi nilidhani nyie askari wa Nasser mmekuja kunipeleleza.

Mimi Mungu wangu ni Allah."

Wanaujua ukweli kama alivyokuwa anaujua Abdel Hakim Amer.

Wakati na muda ukifika aliopanga Allah watakiri ukweli.

Kama hizi mfano wa kichekesho hiki Ikhwan Muslimin wanazo tele.

Utake usitake utacheka.

Picha kulia ni Nasser na kushoto ni Abdel Hakim Amer.View attachment 1635980View attachment 1635981

Mzee kwa haya maandishi yako ya hivi karibuni, kuna giza kubwa limeingia ndani ya nafsi yako. Nini kinakuhangaisha, mpaka unakosa furaha kiasi hiki? Kwa hakika nimezoea kuona unaandika historia ya mambo ya zamani, ukijaribu kuwaibua watu kadhaa wa dini ya kiislamu, ambao unaamini wamesahaulika.
Haya ya sasa si kama yale uliyokuwa unaandika. Naam, dunia inaendelea kusonga na kila uchao yaja mapya
 
Back
Top Bottom