Kisa cha George Floyd vs Siasa za upinzani Tanzania awamu ya tano

Kisa cha George Floyd vs Siasa za upinzani Tanzania awamu ya tano

G.Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
1,040
Reaction score
2,157
Habari wakuu,

Huku Marekani na ulimwengu ukiwa na taharuki kufuatia kifo cha mmarekani mweusi aliyeuawa na polisi, binafsi nimejaribu kulinganisha/kuhusishanisha hili tukio na namna serikali yetu inavyokabiliana na siasa za upinzani kama ifuatavyo:

1. Katazo la kufanya siasa/goti shingoni
Hili moja kwa moja linafanana na kitendo cha Floyd kukanyagwa shingoni. Ikumbukwe pumzi ya chama ya cha siasa ni siasa na licha ya upinzani kulalamika kwamba wanashindwa kupumua(kufanya siasa) lakini bado haikufanya waachiwe nafasi tumeona msajili wa vyama, jeshi la polisi TAKUKURU zote zimekuwa kama goti kwenye shingo za wapinzani.

2. Askari wengine waliokuwa pembeni
Hawa wanafanana mno na wanasiasa wa chama tawala wanaojiona wako salama bila ku-count concequence zinazoweza kuja baadaye. Kimsingi hapa dhana ya mkuki kwa nguruwe mtamu ndo hii

3. Nafasi ya wananchi waliokuw eneo la tukio
Hapa ni wazi kuwa wananchi walishindwa ku predict future na wengine wakaishia ku record video na kuongelea mbali. Hii ni sawa sawa kabisa na wadau tunaopiga mdomo chini chin na nyuma ya keyboard tukiwa hatuna uhakika kama matokeo yanaweza kuwa ya madhara kiasi gani. Na kimsingi ukimya wa wananchi ni kama umetoa go ahead kwa matendo ya watawala

4. Nguvu ya umma
Mwisho kabisa, baada ya yote umma unalazimika kuingia barabarani kupinga uonevu kwa nguvu yake,pamoja wanakuwa wamechelewa maana hawawezi kurudisha uhai wa mtu aiyefariki. kimsingi uma kuamua kuingia barabarani ni jambo la madhara makubwa hasa kwa amani na maendeleo ya taifa kwa ujumla, na ikitokea hali ikaendelea hivyo kwa muda, itakuwa maafa hasa kama viongozi hawatatumia hekima.

Nawasilisha.
 
.
 

Attachments

  • merlin_172942161_091637ed-4324-4383-bf62-644942090642-articleLarge.jpg
    merlin_172942161_091637ed-4324-4383-bf62-644942090642-articleLarge.jpg
    24.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom