PreGE2025 Kisa cha kesi za uhaini kwa Lissu na CHADEMA ni kama ANC na Mandela

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mdude_Nyagali

Member
Joined
Dec 11, 2022
Posts
84
Reaction score
1,494
Miaka ya 1950+ hivi chama cha ANC kule Afrika Kusini chini ya Mandela kilianza kuonesha makali kwa serikali ya makaburu. Harakati za ANC za kudai uhuru wa watu weusi zilipamba moto mno kiasi cha makaburu kukosa usingizi. Makaburu wakawaza ni namna gani wafanye kudhibiti harakati za chama hicho kama ambavyo SSH na wenzake wanawaza kudhibiti CHADEMA na #NoReformsNoElection .

Chini ya uongozi wa Mandela ANC ilikuwa msumari kwa serikali ya makaburu kama ambavyo CHADEMA imekuwa msumari kwa serikali ya Samia Suluhu. Fikiria hapo ANC ilianzishwa mwaka 1912 miaka 6 kabla Mandela mwenyewe hajazaliwa.

Baada ya hapo serikali ya makaburu ilianza kuteka na kuwauwa kikatili wanaharakati wote wanaodai uhuru wa watu weusi kama ambavyo serikali ya Samia imekuwa ikiwateka na kuwapoteza wapinzani wao kisiasa.

Wapinzani wengi hasa wanaharakati waliokuwa wakidai uhuru wa watu weusi walitekwa na kuuawa kule Afrika Kusini. Hii ilifanya mke wa kwanza wa Mandela Evelyn Mase aliyefunga naye ndoa mwaka 1944 kumkataza Mandela siasa. Mandela alivyokataa mwanamke huyo akampa taraka licha ya kuzaa na Mandela watoto 4. Baadaye Mandela akamuoa mwanaharakati mwenzake Winnie Mandela.

Mwaka 1961 Mandela na viongozi wenzake wakiwemo Oliver Tambo, Walter Sisulu, Govan Mbeki na wengine waliazimia kuanzisha kikosi cha wanamgambo kwa ajili ya kupigania uhuru. Hii ni baada ya njia za kawaida kupigwa stop na watawala. Kikosi hicho cha wanamgambo kiliiitwa uMkhonto weSizwe kwa kifupi MK. Maelfu ya vijana wengi walitoka Afrika kusini kuja Tanzania pale Morogoro na Dodoma kwenye mafunzo ya kijeshi kukomboa nchi yao.

Msumbiji ilipopata uhuru vijana wengine wa ANC walielekea Msumbuji kupata mafunzo ya Kijeshi. Baadhi yao walielekea Cuba baada ya Fidel Castro kuchukua madaraka.

Kama mnavyojua chama chochote kinachokuwa tishio kwa dola lazima serikali ipandikize mamluki. Vibaraka wa ANC wakatoa siri kwa mabwana zao makaburu kuhusu uanzishwaji wa kikosi cha wanamgambo wa uMkhonto weSizwe - MK. Makaburu wakaona wamkamate Mandela na kumfunga jela ilj kunyong'onyeza kikosi hicho na kukisambaratisha. Kwa staili ya piga mchungaji kondoo watawanyike.

Kwa bahati mbaya Mandela hakuwa Afrika kusini wakati huo, alikuwa anashinda Tanzania, Msumbiji na Cuba ambako vijana walikuwa wanafuliwa kijeshi huko. Basi, serikali ya makaburu ikatengeneza vijana kama hawa mnaowaita #Njaa55 . Hawa wakaanza kumchapa Mandela kwenye media kuwa anaua chama. Wakaenda mbali zaidi kuitisha mkutano mkuu wa ANC ili wamng'oe Mandela katika uongozi. Of course huu ulikuwa mtego wa serikali wakiamini Mandela akisikia anataka kung'olewa atarudi haraka wamnase.

Kweli, Mandela akawa anamuaga Nyerere akashushe joto la #Njaa55 waliolipwa na makabulu. Nyerere alimtahadharisha kuwa unaweza kuwa mtego. Mandela alivyofika Afrika kusini akachukua tax kuelekea Pretoria ambako mkutano wa ANC ulipangwa akakamatwa na kupewa kesi ya uhaini yeye na wenzake. Kosa lao likawa kuanzisha kikosi cha wanamgambo wa uMkhonto weSizwe - MK.

Makaburu wakapiga marufuku shuguli zote za ANC Afrika kusini. Wakajiona wameshinda lakini kumbe mwisho wao ulikuwa umefika. Wale wanamgambo wa MK walianza kupeleka moto kwa kulipua viwanda, maduka makubwa huku raia wa kawaida wakiandamana kutaka Mandela aachiwe. Uchumi wa Afrika kusini ukaanguka. Wawekezaji wakakimbia na hatimaye makaburu wakanyosha mikono Mandela akaachiwa na kuwa Rais.

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Ukiacha Mandela lakini pia aliyekuwa Rais wa Zambia Edger Lungu alimpa kesi ya uhaini mpinzani wake mkubwa Hakainde Hichilema na kumfanya akae mahabusu miezi 6. Baada ya kutoka haikuchukua muda Zambia ikaingia kwenye uchaguzi mkuu ambao Hakainde Hichilema akatangazwa msindi na sasa ni Rais wa Zambia.

Kwa hiyo kesi hii ya uhaini kwa Tundu Lissu ni silaha ya mwisho ya Samia na ndilo litakuwa anguko lake na mwisho wake wa kuwepo ikulu.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
 
Attachments

  • 20250413_142941.jpg
    20250413_142941.jpg
    114.4 KB · Views: 50
Tatizo tulilonalo watanzania ni kwamba suala la uhaini tunalisikia tu redioni na sio kwa vitendo na ndio maana tukilala tukiamka tunawapa watu kesi za uhaini,. Enzi za JKN kulikua na matukio ya uhaini, msiombe , nchi inatikisika, rais halali, jeshi halilali, polisi hawalali,
Eti kuna suala la uhaini halafu mama anakwenda Angola, tusifanye mzaha kwenye mambo mazito.
Tabia hizi ndio zimepelekea hata maana ya ugaidi tanzania kubezwa kwa sababu ya watu wasiokua na hatia kubambizwa makosa eti ugaidi. Time will tell. Huu uroho wa madaraka ipo siku tutakuja kuongea lugha moja gaidi ni nani na muhaini ni nani.
 
Miaka ya 1950+ hivi chama cha ANC kule Afrika Kusini chini ya Mandela kilianza kuonesha makali kwa serikali ya makaburu. Harakati za ANC za kudai uhuru wa watu weusi zilipamba moto mno kiasi cha makaburu kukosa usingizi. Makaburu wakawaza ni namna gani wafanye kudhibiti harakati za chama hicho kama ambavyo SSH na wenzake wanawaza kudhibiti CHADEMA na #NoReformsNoElection .

Chini ya uongozi wa Mandela ANC ilikuwa msumari kwa serikali ya makaburu kama ambavyo CHADEMA imekuwa msumari kwa serikali ya SSH. Fikiria hapo ANC ilianzishwa mwaka 1912 miaka 6 kabla Mandela mwenyewe hajazaliwa.

Baada ya hapo serikali ya makaburu ilianza kuteka na kuwauwa kikatili wanaharakati wote wanaodai uhuru wa watu weusi kama ambavyo serikali ya SSH imekuwa ikiwateka na kuwapoteza wapinzani wao kisiasa. Wapinzani wengi hasa wanaharakati waliokuwa wakidai uhuru wa watu weusi walitekwa na kuuawa kule Afrika Kusini.

Hii ilifanya mke wa kwanza wa Mandela Evelyn Mase aliyefunga naye ndoa mwaka 1944 kumkataza Mandela siasa. Mandela alivyokataa mwanamke huyo akampa taraka licha ya kuzaa na Mandela watoto 4. Baadaye Mandela akamuoa mwanaharakati mwenzake Winnie Mandela.

Back
Top Bottom