Kisa cha kijana aliyetokea Jamhuri ya Taured

mikedean

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Posts
3,267
Reaction score
4,634
Habari zenu wadau

Leo katika kupitia baadhi ya mambo mtandaoni nikakutana na kisa cha "Republic of Taured".

Ipo hivi, miaka ya 1950 ilitokea kisa cha kijana wa makamo katika airport moja huko Japan na kuwaeleza maofisa wa uwanja wa ndege kuwa anatoka nchi ya Taured. Maofisa wakamwambia kwamba nchi hiyo haipo kwenye ramani ya dunia. Cha ajabu yeye akang'ang'ania kuwa anatoka huko na akaonesha vitu vya kumtambulisha vya mamlaka ya Taured.

Vitambulisho kama vile passport na fedha alivionesha. Maofisa walipomwonesha ramani ya dunia akaonesha ilipo nchi ya Andorra na kusema hiyo ndio Taured ilipo tangu maelfu ya miaka. Wataured wanaongea Kiingereza, Kifaransa na Kispain.

Lakini baada ya maofisa waairport kumchunguza muda mrefu na kumpa chumba cha kulala kesho yake asubuhi walikuta chumba kitupu na haieleweki alipotelea wapi wakati chumba kilikuwa kikilindwa na maofisa usalama usiku kucha ili kupata ufumbuzi wa tatizo lile. Cha ajabu ni kwamba hata passport na nyaraka nyingine walizomnyang'anya kwa uchunguzi zaidi zilipotea kimazingara. Mpaka sasa haijulikani mtu huyo alipotelea wapi.

Pia kuna mtu wa ajabu alikutwa huko Ufaransa akiongea lugha ya ajabu. Alionesha sehemu aliyotoka kuwa Lisbon Ureno japo lugha haikuwa ya Kireno pia yeye alionesha kuwa sio mreno bali ni kutoka nchi ya 'Lizbonia'.

Nataka kujua je, ni kweli kwamba kuna milango ya siri ambapo ukiingia unaweza kukuta nchi nyingine kama hizi za Lizbonia na Taured?

Asante na karibu tujuzane.
 
Daah.. Mambo mengine si ya kupuuzia.. Huenda ni kweli
 
Hizo ni habari za kusadikika kama hadithi za mashimo ya mfalme sulemani na visa vya Adili na Nduguze.

Binafsi ukiamini vinakuwepo katika dunia yako na wasiomini havipo katika dunia zao
 
Hii nilishawahi kusimuliwa na Babu yangu Mzee Ismail Kanungila aliyekuwa anafanya kazi Japan miaka hiyo yaani 1949
 
Tumsubirie labda mshana jr anaweza kutuambia habari hizo..
 
Kuna series inaitwa the crossing ina stori kama yako....Kwamba jamaa wanaweza kuwa wanatoka past o future (inawezekana hizo nch za lizbonia na Toured zipo future ko huyo jamaa katoka mbele ya mda ndo maana hatukumuelewa/hawakumuelewa)
 
Habari zenu wadau

Leo katika kupitia baadhi ya mambo mtandaoni nikakutana na kisa cha "Republic of Taured".

Ipo hivi, miaka ya 1950 ilitokea kisa cha kijana wa makamo katika airport moja huko Japan na kuwaeleza maofisa wa uwanja wa ndege kuwa anatoka nchi ya Taured. Maofisa wakamwambia kwamba nchi hiyo haipo kwenye ramani ya dunia. Cha ajabu yeye akang'ang'ania kuwa anatoka huko na akaonesha vitu vya kumtambulisha vya mamlaka ya Taured.

Vitambulisho kama vile passport na fedha alivionesha. Maofisa walipomwonesha ramani ya dunia akaonesha ilipo nchi ya Andorra na kusema hiyo ndio Taured ilipo tangu maelfu ya miaka. Wataured wanaongea Kiingereza, Kifaransa na Kispain.

Lakini baada ya maofisa waairport kumchunguza muda mrefu na kumpa chumba cha kulala kesho yake asubuhi walikuta chumba kitupu na haieleweki alipotelea wapi wakati chumba kilikuwa kikilindwa na maofisa usalama usiku kucha ili kupata ufumbuzi wa tatizo lile. Cha ajabu ni kwamba hata passport na nyaraka nyingine walizomnyang'anya kwa uchunguzi zaidi zilipotea kimazingara. Mpaka sasa haijulikani mtu huyo alipotelea wapi.

Pia kuna mtu wa ajabu alikutwa huko Ufaransa akiongea lugha ya ajabu. Alionesha sehemu aliyotoka kuwa Lisbon Ureno japo lugha haikuwa ya Kireno pia yeye alionesha kuwa sio mreno bali ni kutoka nchi ya 'Lizbonia'.

Nataka kujua je, ni kweli kwamba kuna milango ya siri ambapo ukiingia unaweza kukuta nchi nyingine kama hizi za Lizbonia na Taured?

Asante na karibu tujuzane.
Dunia hii inatisha Sana mkuu, kuna mdogo wangu sasa hivi ni marehemu aliwahi kupotea kijijini kwetu usiku ktk mazingira ya utata Sana, tulimtafuta kila sehemu hatukumwona, alikuwa na miaka 8 tu kipindi kile, tulipokata tamaa na kurudi nyumbani ili tujipange upya mida ya saa 9 alfajiri, marehemu mama alifungua chumba kilichokuwa kimefungwa muda mrefu na tukamkuta amekaa humo akiwa kimya haongei lolote, hadi alipokuja kuwa mtu mzima na kujitambua ,aligoma kabisa kusema alikuwa wapi hadi anafariki.
 
Alika

alikaa humo ndani kwa muda gani? Naje Mlango ulifungwa kwa komeo Na kufuli? Maana mtoto wa miaka nane anakili za kutosha
 
Dunia hii inatisha Sana mkuu, kuna mdogo wangu sasa hivi ni marehemu aliwahi kupotea kijijini kwetu usiku ktk mazingira ya utata Sana, tulimtafuta kila sehemu hatukumwona, alikuwa na miaka 8 tu kipindi kile, tulipokata tamaa na kurudi nyumbani ili tujipange upya mida ya saa 9 alfajiri, marehemu mama alifungua chumba kilichokuwa kimefungwa muda mrefu na tukamkuta amekaa humo akiwa kimya haongei lolote, hadi alipokuja kuwa mtu mzima na kujitambua ,aligoma kabisa kusema alikuwa wapi hadi anafariki.
Hii n stori ya kutisha nilioisoma leo
 
hebu jazia Nyama vyema ...huo mkasa ulikuwaje ""?? kuwaje ? mmmh
 
Kuna series inaitwa the crossing ina stori kama yako....Kwamba jamaa wanaweza kuwa wanatoka past o future (inawezekana hizo nch za lizbonia na Toured zipo future ko huyo jamaa katoka mbele ya mda ndo maana hatukumuelewa/hawakumuelewa)
Naomba kukubaliana na wewe mkuu.
 
Science fiction haswa kwenye time travelling, i like these movies. These guys put their dreams in the movies, nice to watch.
 
Back
Top Bottom