Kisa cha kweli, mbingu ipo na moto wa jehanamu upo

Kisa cha kweli, mbingu ipo na moto wa jehanamu upo

( kwa mjibu wa dakitari )
Hearsay stories

lakini ghafula wakashuka watu wawili wamevaa nguo nyeupe wale majitu waliopoona wale watu wawili walirudi nyuma, wale malaika wakamwambia arudi abatizwe kwa maji mengi
Kuna dhana mbovu imejengeka kuwa malaika huva mavazi meupe na shetani ni mweusi siku zote

Unataka kuwafundisha watu ukweli kupitia uongo?
Hakika

Astra projection
Haswaa!
 
Warumi 2:11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. Warumi 2:12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. Warumi 2:13 Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. Warumi 2:14 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Warumi 2:15 Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;
mi nimekuandikia kwa luga rahisi unanijibu na vitu vigumu jioni hii mi nakula k vant yangu tumia lugha rahisi kujibu sio ku QUOTE mavifungu hata wewe mwenyewe huyaelewi
 
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Hayo yalikua maandiko ya Paulo Myahudi mwenye uraia wa rumi aliwaandikia Wakorintho wakati
Huo ili watu wale wa Uyunani wamrudie mungu wao
Sasa sisi wamatumbi na hao Wakorintho wapi na wapi jamaa?

Funguka akili wewe humpati mtu hapa labda wayahudi weusi wenzio!
 
Habari ya asubuhi wakuu!! Hiki ni kisa cha kweli kwa ambaye sio muumini wa Mbinguni na kuzimu hivyi vyitu ni halisi.

Miaka kadhaa iliyopita ndugu yangu, aliumwa sana wakati yupo hospitalini tunaamuuguza, alikuwa ameokoka (mlokole), hivyo kwenye ile wodi wachungaji mbalimbali walikuwa wanapishana kuja kumuombea maana aliumwa kipindi kirefu sana, Siku moja jioni alizidiwa na hatimae kufariki dunia( kwa mjibu wa dakitari ) baada ya taratibu za hapa na pale mwili kuandaliwa! Kupelekwa mchowari alipiga chafya na kurejea na kutoka pale akawa mzima mpaka leo, alichokisema ni hiki hapa baada ya kuzinduka

1: Kuna maisha baada ya haya, anasema alitoka nje ya mwili wake na akaona jinsi dakitari alivyokuwa anampima pima na jinsi ndugu walivyoanza kulia, baada ya hapo alijikuta yupo dunia nyingine kabisa tofauti na hii!!

2: Anaendelea kusema unakuwa na akili zako zote na kumbukumbu zako zote, maana yeye alipofika eneo hilo alikuwa anakumbuka kila kitu kilichopo duniani, na alijua amekufa!

3: Matendo yako ndo yataamua uende njia ipi , ya mbinguni au kuzimu, anasema baada ya kufika eneo aliona kwa mbali majitu mawili ya kutisha yanakimbia kuja kumlaki!, lakini ghafula wakashuka watu wawili wamevaa nguo nyeupe wale majitu waliopoona wale watu wawili walirudi nyuma, wale malaika wakamwambia arudi abatizwe kwa maji mengi, maana hawezi kuingia mbinguni, na ndo maana wale majitu yalikuwa yanamfuata!! Baada ya kuambiwa rudi duniani ukabatizwe ndipo akarejea duniani!

Note:
1: Hamna mtu atakayeenda mbinguni bila kumwamini Yesu!!
2: Ukitaka kwenda mbinguni fuata yote aliyoyafanya Yesu ikiwemo ubatizo aliobatizwa sio vinginevyo.

Huu ushuhuda ni kweli wakuu, Sio wa kudharau.
Inawezekana Kuna jehanamu na pepo,lakini hatuwezi kudhibitisha Hilo kwa story kama hii,vitu vya kiroho havina ushahidi wa kisayansi,ni mambo ya kufikirika,ukiamini masimulizi kama haya,hata akija "nabii"au "mtume "(Hawa wa siku hizi)akikuambia ameoteshwa na roho mtakatifu,amchukue mkeo na binti yako wawe wake zake,utakubali.
 
Inawezekana Kuna jehanamu na pepo,lakini hatuwezi kudhibitisha Hilo kwa story kama hii,vitu vya kiroho havina ushahidi wa kisayansi,ni mambo ya kufikirika,ukiamini masimulizi kama haya,hata akija "nabii"au "mtume "(Hawa wa siku hizi)akikuambia ameoteshwa na roho mtakatifu,amchukue mkeo na binti yako wawe wake zake,utakubali.
wakina gwajima na mchungaji mashimo ha ha ha ha ha
 
GOD is real mungu yupo na mbingu ipo na kuzimu kupo , ila wanaoona ni wachache mpaka uyaishi maisha yakumpendeza mungu ndo unaona hayo mambo.
 
Ndugu yako anaitwa nani na tukio lilitokea katika hospitali gani?
 
Back
Top Bottom