Kisa cha kweli: Ndio kusema huyu mama alifunika nyota yangu kwa uchawi?

Kisa cha kweli: Ndio kusema huyu mama alifunika nyota yangu kwa uchawi?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Nimejikuta usingizi unakata na kuruka kama mtoto.

Baada ya kumaliza fomu six miaka 2000 siku moja nilienda kumtembelea jamaa yangu asubuhi ili tupige stori. Mama yake akaandaa chai ilikuwa, Dar maeneo ya Yombo Kilakala.. Basi wakati anatenga chai akaleta vikombe viwili cha kwangu na cha rafiki yangu

Kabla ya kumimina chai kile kikombe changu akakifunika juu chini. Yaani mdomo ukalala chini. Cha rafiki yangu mdomo ukawa kama kawaida juu. Baadae ndio akamimina chai.

Nilitoka hapo nawaza sana. Maana mpaka leo nafikria kwa nini alifanya hivyo. Mshikaji wangu sasa ni Engineer taasisi moja ya serikali. Mimi nauza Kangala japo Maisha yanaenda ila natafakari sana.
 
Kama alianza kuweka chai kikombe cha mwanaye ilikuwa sahihi kabosa kufunika kikombe chako kwa sababu za kiafya. Kwani wewe na mwanaye mlipata pata alama sawa kwenye vyeti vyenu? na mliomba kazi sehemu moja?

Na siku ya usahili mlifanya kila kitu sawa sawa ? Ndugu yangu Muamini Mungu kuwa yeye ndiye mtoaji na wewe uko kwenye foleni, zamu yako ikifika utapokea
 
Kama alianza kuweka chai kikombe cha mwanaye ilikuwa sahihi kabosa kufunika kikombe chako kwa sababu za kiafya. Kwani wewe na mwanaye mlipata pata alama sawa kwenye vyeti vyenu? na mliomba kazi sehemu moja? Na siku ya usahili mlifanya kila kitu sawa sawa ? Ndugu yangu Muamini Mungu kuwa yeye ndiye mtoaji na wewe uko kwenye foleni, zamu yako ikifika utapokea
Mimi nauza Kangala tu
 
Nimejikuta usingizi unakata na kuruka kama mtoto.

Baada ya kumaliza fomu six miaka 2000 siku moja nilienda kumtembelea jamaa yangu asubuhi ili tupige stori. Mama yake akaandaa chai ilikuwa, Dar maeneo ya Yombo Kilakala...
Yaani ufeli shule unaanza kusingizia watu. Ulikuwa hausomi tu ndugu yangu. Ungekuwa unasoma hata usingepata mda wa kuwaza ama kuandika vitu vya kijinga kama hivi
 
Kwani kufeli shule ndio kufeli maisha. Nyota yangu inatakiwq iwake niwe na baa kuliko kuuza kangala
 
Back
Top Bottom