Kisa cha kweli: Niliacha kazi nikajiunga masters ili nimsomeshe mdogo wangu chuo

Ingependeza ukaweka wazi kuwa kilikuwa chuo fulani katika nchi fulani na mchakato wake wa hizo scholarship unafanyika hivi na hivi .
Lengo ili kusaidia wadogo zetu walio vyioni wenye ndoto kama zako za kisomea masters nje ya nchi .

Lakini ulivyofanya wew umepelekea uzi uonekane hauna maana kabisa maana hakuna cha kujifunza ndani ya ulichoandika hao watu wa west Africa wangefanyiana kama ulivyofanya wewr humu sidhani kama wangejazana hizo nchi za U.K , U S A na AUSTRALIA.
Upo sahihi akusikilize
 
Kuna nini tena mkuu, tafuta uzi wa scholarship anza kufanya maombi au watumie ndugu jamaa na marafiki waapply hizo zote ni fursa.
Uvute alafu uweke pale chini ya Uzi wako

Andika

Pia soma: link.scholarship............
 
1.5m ndo unaona hela kubwa eti inazifi mfanyakazi wa wizara, mkuu uandishi wako sio wa mtu aliyesoma masters,
Mi nimecheka kifala balwaa,yaani watu hatupo Wizarani na tunajilipa zaidi ya hvyo na marupurupu kibao halafu wala haturingi,🤣🤣🤣🤣
 
Haturingi mkuu kuna watu wanataka kutimiza malengo yao wamekwama hii inaweza kuwasaidia mkuu wangu.
 
Uvute alafu uweke pale chini ya Uzi wako

Andika

Pia soma: link.scholarship............
Nimesha vuta uzi tayari, watu waliokwama na wanataka kuongeza kipato walau kwa kutumia elimu zao huu uzi ni mzuri. Mtatusamehe wakuu tumeficha baadhi ya taarifa.
 
Mkuu ahsante sana kwa mchango mzuri kila mmoja hulidhika na kile anachokipata kulingana na matumizi yake.
Ila kwa mbwembwe ulizonazo mkuu kwa comment mbali mbali naona kabisa hio stori haijabalance...Umesema uliajiriwa shirik X ulikua unalipwa mshahara mkubwa ila ukaacha kisa 1.5M hapo sinaelewa mshahara kubwa wa shirika X ndo upi kama hata 1.5M umeona kubwa.
 
Mbona najaribu kuifuatilia stori yako, sio hii hapa
Halafu nashindwa kuelewa, mara Uko China mara juzi kati uko Ardhi
Huyo mtu wa fiksi na kujikweza fuatilia comment zake hasa zinazowahusu watu wanaotafuta vyuo vya kati.
 
Kisa cha kweli: Niliacha kazi nikajiunga masters ili nimsomeshe mdogo wangu chuo
Hiki ni kisa cha kweli ilinitokea mara tu baada ya kupata kazi katika Shirika fulani hapa nchini.

Tangu zamani ndoto yangu kubwa ilikua ni kusoma nje ya nchi kwa scholarship. Mara tu baada ya kuhitimu masomo yangu ya shahada nilibahatika kuajiriwa kwenye shirika X ijapokuwa mshahara niliopewa ulikua mkubwa ila haukuweza kutosha kulipia karo ya mdogo wangu aliyekuwa akisomea astashahada katika chuo fulani jijini X.

Wakati nikiwa nafanya kazi katika shirika lile nilizoea kutumia simu yangu kuingia mtandaoni kufuatilia fursa mbalimbali za scholarship nje ya nchi. Ndipo siku moja nilikutana na tangazo la scholarship linalotoa ufadhili kusomea masters nchi X. Nilifurahishwa na kiwango cha pesa ya kujikimu iliyotajwa katika tangazo lile. Walikua wanatoa pesa ya kujikimu ya 1.5M kwa mwezi ukiachana na ada, bima na pesa ya malazi.

Hakika nilipopiga hesabu niligundua hiyo pesa ingeweza kuniokoa nikaweza kumsomesha mdogo wangu mpaka chuo kikuu. Basi usiku uleule wa mwezi wa 11 nilianza kufanya maombi ya scholarship, nilihakikisha natumia muda wangu ambao sina kazi ofisini na muda wa baada kazi kufanya maombi ya scholarship.

Mpaka kufikia mwezi wa pili nilikua nimeshamaliza kufanya maombi yote. Nikawa nasubiri majibu ya scholarship yatoke. Mwezi wa saba nilipigiwa simu kwamba nimefanikiwa kupata scholarship na hivyo kabla ya mwezi wa tisa nilitakiwa niwe nimeripoti chuoni nchi X.

Hakika sikuamini kama kweli muda umewadia wa kwenda ng'ambo lakini muda wote niliwaza jinsi nitakavyokwenda kutumia hiyo 1.5M kumsomesha mdogo wangu. Hivyo hata sikujiuliza sana, nilikwenda kwa mkurugenzi wa shule nikamweleza kwamba nimepata ufadhili wa kwenda kusoma nje na nitarejea baada ya miaka X.

Mkurugenzi alikubali kwa moyo wote. Basi mwezi wa nane tarehe za katikati nikaenda ubalozi wa nchi X jijini Dar es Salaam, nikaanza kufanya mchakato wa kupata VISA, nikafanikiwa nilihakikisha natumia fedha nilizo save kulipia maana nilijua zitaenda kurudi.

Muda wa safari ulipowadia nilipanda ndege na kuvuka ng'ambo, mara baada ya kufika siku zilizidi kwenda mpaka ilipofika siku niliyoanza kulipwa pesa zangu za scholarship kila mwezi. Pesa zililipwa bila kucheleweshwa wala usumbufu wowote tena bila makato. Lakini cha kushangaza hata bank walikua hawakati hata senti.

Nilihakikisha natumia hiyo fursa kusave hela zangu ili niweze kulipa ada ya kumsomesha mdogo wangu. Mbali na ada ya chuo, kila mwezi nilimpatia boom la laki moja na kumi ili aweze kujikimu lakini pia nilimpatia pesa ya malazi shilingi laki mbili na ishirini kwa mwaka. Ada yake ilikua ni milioni moja na laki mbili japo ilikua inaongezeka kila mwaka. Kiukweli nilipokuwa kazini nilishindwa kusave hata pesa nyingi lakini kule nilifanikiwa kusave pesa nyingi tu.

Katika kile chuo mdogo wangu alisoma kwa muda wa miaka mitatu yaani astashahada mwaka mmoja na stashahada miaka miwili. Nikamwombea shahada akafanikiwa kuchaguliwa kwa mkopo wa loan board. Hivi sasa ndio yupo mwaka watatu chuo X anamalizia shahada yake.

Nilipokuwa nje ya nchi nilijifunza mambo makuu mawili ambayo napenda kuyaongelea hapa.
1. Sio kila mtu anayesoma master's lengo lake ni kuongeza elimu tu rahasha wengine wanasoma master's kwaajili ya kutafuta pesa. Mtu anayesoma masters kwa scholarship mfano nchi niliyokwenda analipwa fedha ambayo inazidi hata mshahara wa mtu anayefanya kazi wizarani. Kwanza uzuri wa ile pesa haina makato hata kidogo unaipokea kama ilivyo.

2. Pili nilipokua kule nilikutana wafanyakazi wanaofanya kazi taasisi kubwa tu hapa Tanzania. Wamefanikiwa kujenga nyumba mara baada ya kupata scholarships.

Naomba niishie kwakusema kwamba watanzania wanafursa nyingi sana za scholarship za kusomea nje ya nchi lakini wengi wao huzidharau hizo fursa. Watu kutoka nchi za afrika magharibi ndio wamekua kinara wa kuchukua hizo fursa. Wamejazana US, UK, CHINA, GERMAN, AUSTRALIA n.k.
Maisha ni kuchagua... hongera kwa hesabu zako nzuri. Nadhani uliye mchukulia sacrifice yote hiyo basi na aje awe wa MATUNDA! Hongera sana.
 
chai
 
Back
Top Bottom