Kisa cha ''magaidi'' wawili: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege

Nitavipitia vyote vitabu na nakala nivisome mzee wangu
 
Asome dini gani na Mungu Hana dini
Asome dini gani na Mungu Hana dini
Nyanza...
Umemjibu Abu Dharr kuwa mimi nisome dini gani.

Nimecheka.

Nimesikitishwa sana na lugha ya ndugu yangu Abu Dharr ya kibri na kejeli.

Mimi si mtu wa hayo.

Nasaha zake labda zingekuwa na maana kama ningekuwa nina elimu ya dini na kuwa na uwezo wa kuisomesha.

Bahati mbaya mimi ujuzi alionijaalia Allah uko katika usomi wa kisekula kama mnavyonisoma hapa.

Ama kwa kuwaita nduguze "genge" mimi namnasihi yeye ajizuie kuhukumu.

Hawa vijana nimeishinao Tanga kwa miaka 15 na hata siku moja sikuwasikia kama ni maadui wa taasisi yeyote iwe Shamsiyya, Maawa au Zaharau au wanasemwa kwa ubaya.

Nimewajua hawa vijana kwa sifa ya kusomesha Qur'an watoto wadogo na mengine mengi ya kheri.
 
Makanisani na misikitini na masinagogi watu wafundishwe kuwapenda binadamu wenzao bila kujali tofauti zao.

Ni kujidanganya kwamba Eti itatokea watu imani fulani wataangamizwa kisha wabaki wa imani nyingine pekeyao.
Lakini lazima tumtetee yesu mkuu,, yesu alisema injili lazima ienee kona zote za dunia🤷‍♂️
 
Atakuwa anakaribia 70 years, write-off. Labda afanye kazi za masjid tu maana amekuwa indoctrinated na radical islamism doctrine
Huihui...
Kipi kibaya nilichofanya kinakufanya utokwe na adabu kwangu?

Mwezi February In Shaa Allah nitafikisha miaka 71.

Nakuasa kijana chunga ulimi wako hilo neno, "write off," ni kufru kwa Muumba linaweza likarejea kwako Allah akunusuru.

Kuwa na adabu.

Huenda nina umri sawa na mama yako au baba yako.
 
Nelson...
Sijawahi kumwandika mtu yeyote kwa ubaya ikiwa una ushahidi wa hilo uweke hapa.
 
Nelson...
Sijawahi kumwandika mtu yeyote kwa ubaya ikiwa una ushahidi wa hilo uweke hapa.
Aaaah mzee wangu msimamo wako kwa watu wa msalaba unajulikana na hapo tu ndipo yalipo madhaifu yako anyway sisi ni binadamu hakuna aliyekamilika!!Lakini nje ya hapo wewe ni muandishi bora kabisa na vijana tuna mengi ya kujifunza kutoka kwako hasa kwenye fani hii
 
Msamehe tu huyo kijana mzee wangu
 
Unachukia sana Wakristu, ungekuwa na uwezo ungefanya Tanzania waishi Waisalamu tu. Hiyo ndiyo sababu nakuona write off
 
Unachukia sana Wakristu, ungekuwa na uwezo ungefanya Tanzania waishi Waisalamu tu. Hiyo ndiyo sababu nakuona write off
Huihui...
Siwezi kuwa hivyo.

Kuandika historia ya kweli kusahihisha ile iliyopachikwa sikufanya hivyo kwa kusukumwa na chuki.

Kisome kitabu na tafuta ndani yake chuki ukiikuta weka hapa tuishuhudie.
 
Uislamu ni amani huu uongo unadhihirisha kabisa uwepo wa shetani!
 
Dini yenye vijinasaba vya vurugu haina nafasi Tanzania unataka kutuambia serikali inawaonea hao magaidi wako
 
Hakunaga cha bure Kuna mtu wanamtumikia
Yomboo,
Sheikh Chambuso aliulizwa swali hili alipokuwa anahojiwa.

Akajibu kuwa anamtumikia Allah na huyo ndiye mlipaji wake.

Akawaambia kuwa kama yeye angekuwa analipwa na mtu wao polisi waliomkamata wangemjua huyo mlipaji na wangemkamata.
 
nakuheshimu sana kwa kuwa na huu mtazamo kiongozi.
Wewe unaweza fundisha dini kwa mtu asiekua wa dini yako na mkaelewana na hata aka silimu bila vitisho wala ghasia. Epuka hisia kwenye mijadala migumu,badala yake chambua facts na hoja tu.
Nimekuwepo "field" baada ya hizi ishu and trust you me,kuna mengi sana ambayo watetezi wa "wanaharakati" hawayajui!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…