enzo1988
JF-Expert Member
- May 26, 2018
- 1,838
- 7,346
Katika Utekelezaji wa Majukumu yake Mwenyezi Mungu muweza wa yote amekasimisha baadhi ya majukumu hayo kwa Malaika wake.
Sasa katika moja ya hao Malaika ndio huyu. Anaitwa ISRAEL A. S... Dah anatisha sana huyu kiumbe. Ndio aliyepewa jukumu la kutoa Uhai /roho na kupaa nazo kuzipeleka kwa Muumba.
Kisa chake hiki nimekikuta mahali nikaona nishare hapa kwa ndugu zangu Waislam na hata wasio waislam wapate Ukumbusho. Karibuni
Aliwahi kuulizwa malakul maut na ALLAH S.W Jee uliwahi kulia au kucheka pindi unapotoa roho za waja wangu?
Akajibu "niliwahi kulia, kucheka na kupatwa na fazaa".
Nilicheka siku moja nilipokwenda kwa mtu mmoja kuchukuwa roho yake nikamkuta anaongea na fundi wa viatu akimuambia nishonee vizuri nivae mwaka mzima, nitanunua vipya mwakani nikacheka na kuichukuwa roho yake kabla hajavivaa.
Na kilichoniliza ni siku Ulinituma kuchukuwa roho ya mwanamke mmoja aliekuwa pangoni peke yake akimnyonyesha mwanawe na hakuna mtu aliekuwa anajua mahali alipo basi nikaitoa roho yake huku mtoto akilia kwa uchungu na mimi nikalia.
Na kilichonipa fazaa ni siku ulionituma nikachukuwe roho ya mcha Mungu sana wakati nilipoingia chumbani mwake nikakuta chumba chake kimegubikwa na nuru nikapata tabu kumfikia nilipokuwa natoa roho yake fazaa kubwa ikanishika.
ALLAH S.W akamuuliza jee unamfahamu mtu huyo?
Akajibu malakul maut: lah simfahamu zaidi ya kuwa ni mwanachuoni.
ALLAH S.W akamuambia huyo ni yule mtoto aliyekuwa akinyonyeshwa na mama yake pangoni na ukaichukuwa roho ya mama yake.
Huyo ndio malakul maut anaewatenganisha wapendanao mama na mtoto wake, mtu na mkewe, mtu na rafiki yake mtu na mzazi wake.
Basi usimsahau malaika huyu hakika yeye hakusahau inapokuja amri kwake kaniitie mja wangu fulani basi hushuka kwa haraka na kutii amri ya ALLAH S.W tukumbuke ipo siku na saa atatutembelea wakati wowote saa yoyote dakika yoyote sekunde yoyote tukae tukilitaffakar hili kwani huenda chochote kile tunachokifanya kikawa ndio tendo letu la mwisho au ikawa ndio kauli ya mwisho
Tumuombe ALLAH S.W atupe khatma njema katika matendo yetu ya mwisho na atujaalie kauli yetu ya mwisho iwe LAAILAHA ILLA LLAH MUHAMMADU RASSULU-LLAH
AMIN.
FADHAKIR FAINNA DHIKRA TANFAUL MUUMININ.
Pongezi kwa atakayeisoma,
akaifahamu na akakimbilia
kuitendea kazi... na Allah
amjaze kheri atakayeituma hii kwa wengine.
ALLAH S.W akamuuliza jee unamfahamu mtu huyo?
Akajibu malakul maut: lah simfahamu zaidi ya kuwa ni mwanachuoni.
Hapa ni watu wawili wanapiga story au soga
Samahani mtoa mada 'Product ya Udsm' nina maswali yafuatayo
1)Malaika wanamuona Mungu ana kwa ana au uso kwa uso?????
2)Haya majina ya malaika Mungu aliwapa lini????Kwamba wewe jina lako ni hili na kazi yako ni hii????
ALLAH S.W akamuambia huyo ni yule mtoto aliyekuwa akinyonyeshwa na mama yake pangoni na ukaichukuwa roho ya mama yake.
Kwa kutumia ubongo wako unamuona Mungu mwenye huruma hapo?????Au Mungu mwenye roho mbaya???