Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
😳 Mapya yaibuka!! Licha ya Pele(82) kumkana mwanae huyo pichani wa nje ya ndoa maisha yake yote hadi alipofariki miaka 17 iliyopita, lakini kwa mujibu wa taarifa mpya kwenye mirathi aliyoiacha Pele yenye thamani ya £13 million ambazo ni zaidi shilingi bilioni 37.5 za Tanzania, amelijumuisha pia jina la mwanae huyo Sandra Regina kama mmoja wa watoto wake 7
Katika ndoa yake ya kwanza Pele alipata watoto 3, ndoa yake ya pili alipata watoto 2 mapacha, halafu mahusiano yake mengine ya nje ya ndoa na wanawake tofauti alizaa watoto 2 akiwemo Sandra pichani
Mama yake Sandra alikuwa mfanyakazi wa usafi wa Pele na ndipo alipopata mimba lakini Pele aliikataa kata kata kuwa yeye sio baba wa mtoto, walifikishana hadi katika vyombo vya sheria na DNA ilionesha pia kuwa Pele ndie baba mzazi wa Sandra ila bado Pele alikataa kabisa kukubali kumpokea Sandra kuwa mwanae
Mama yake Sandra kwa jina la Anisia Machado yeye alitaka tu pia Pele akiri kuwa Sandra ni mwanae lakini haikufua dafu
Sandra Regina alizaliwa 1964 na mwaka 1996 mahakama ilimruhusu kutumia jina la ukoo la Pele. Maisha yake yote Sandra alipambana kukubaliwa na baba yake huyo lakini haikufua dafu hadi alipofariki miaka 17 iliyopita kwa kansa
Pele ambaye pia alifariki kwa kansa hivi karibuni, siku moja kabla ya kifo chake kwa mara ya kwanza aliomba akutane na wajukuu wake wawili wa kiume ambao ni watoto wa Sandra ambapo wajukuu husika kwa jina la Gabriel na Octavio ndio watarithi sehemu ya utajiri wa Pele kwa niaba ya mama yao
Gabriel akizungumza amesema shangazi zao waliwataarifu kuwa babu yenu anataka kuonana na nyinyi na wamefurahi sana hatimae ndoto ya mama yao imetimia