Kisa cha mfalme Belshaza na yanayofanyika CHADEMA

Chanzo changu kinaonyesha alikuwa mfalme, ila hebu tuache kubishania rangi ya paka, tujadili uwezo wa paka kukamata panya.... Je unaona jitihada zozote za Chadema katika kuipambania nafasi yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja zako ni mwendelezo wa kuipaisha act.
Lakini Mimi sioni mafanikio ya makubwa ya hicho chama,kama magufuli ataendelea kukaza kuviua hivi vyama.
Labda kama magufuli ana mkono ndani ya act ili kuzidi kuiangamiza chadema. WEKENI URINGO SAWA WA KISIASA MUONE KITAKACHOJIRI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma andiko lako lote kisha nikajiuliza huyu mleta mada ni mwana CDM ama siyo. Mada imejaa lawama tu, na tahadhari bila kuja na solution. CDM sasa ni taasisi imara sana, sasa ukianza kutishia nyau tunabaki tunakushangaa. Kama ni mwana ccm sawa lakini kama ni CDM njoo na mapendekezo nini cha kufanya na sio lawama. Kumbuka kuwa karibu viongozi wote wa chama wana kesi mahakamani, sasa unataka wafanye nini zaidi?
 
Since 1995 the ruling part used a lot of money and resources to underdevelop opposition .You can't imagine such embezellment of public fund ,stated by destroying UMD ,NCCR,CUF now they don't know where to CDM or ACT .sorry i used this language to avoid mataga at work here in the forum .
 
Mkuu hesabu zilikuwa hivyo kama unavyosema. Tatizo limetokana na Lowassa
Baada ya kuwaacha CDM, hilo imekuwa funzo kwa wahamiaji 'wahajiri'
Maalim angepokewa kwa mashaka makubwa. Kumbuka ukiuumwa na nyoka.....

Pili, maalim ana timu yake. Wote waliona kwenda CDM ni kuoteza nafasi zao

Tatu, badala ya kuanzisha chama wakaona ni bora watumie chama kichanga ACT
Hili litasaidia kuhama na 'mtaji' wa wanachama na kukuta 'mtaji wa Zitto' hata kama ni mdogo

Kwa upande mwingine nadhani ni vema kuwa na vyama viwili vikubwa vya upinzani

Hilo linawafanya CCM wakae mguu sawa na kupunguza hujuma
Watahitaji 'resources' znz na Bara na hivyo watavutika ''stretched'

Uwepo wa CUF ya nguvu visiwani uliwalazimu kupeleka resources huko na kutoa nafasi kwa CDM kupata idadi ya Wabunge.
Ukichanga wa CUF na CDM idadi ilikuwa kubwa, CCM hawataki hilo litokee

Tatizo ninaloliona ni maafikiano na hapa ndipo CDM wanatakiwa wawe makini
Kauli zao dhidi ya ACT ni za kubomoa na si za kujenga.
Hawa wanatakiwa wawe timu moja ikiwa na jezi tofauti kwasababu za kisheria

CDM na ACT waelewe ''adui'' yao si wao kwa wao ni CCM
 
Nimeona hoja yako, ni kweli sikuweka solutions huo unaweza kuwa Ni udhaifu wa andiko langu lakini viongozi wa CDM wanapaswa kulisoma kwa fikra jadidi na sio hisia mlipuko kisha kutathmini Kama Lina mashiko na kisha kuja na majibu toshelezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mpumbavu hasa huwezi kutolea mfano wa mfalme Belshazzar aliyemuudhi Mungu na CHADEMA inayofanyiwa hiyana na njama na Magufuli ili ianguke, kwanza Chadema haina Ufalme wa dola Kama CCM ,mjinga kweli wewe, itakayoanguka ni CCM na Magufuli na si CHADEMA, Mungu akupe uhai ili uje ushuhudie anguko la CCM na Magufuli, maana Magufuli ni mfalme na amekuwa akimuudhi Mungu akisema aombewe wakati anaua wapinzani na kuwafunga Kwa chuki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika mfano wako wa kisa cha Belshaza ,Belshaza alimuuzi Mungu Kwa kiuka utaratibu jambo ambalo lilikuwa chukizo kwa Kwa MUNGU,... je Kwenye Siasa za Tanzania Ni Nani anae muuzi MUNGU Kwa kuvunja taratibu za kidunia (KATIBA na HAKI ZA BINADAMU .....NK) NA ni nani anae Muuzi MUNGU kwa kukiuka taratibu za kimbingu (HAKI NA UTU) je katika mfano wako umemtaja?, ama we wajua kuunga mkono juhudi za NDULI tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umetoa angalizo zuri ila kama umefanya utafiti angalau sasa CDM wameanza kuamka, ukizunguka kuna operesheni "chadema msingi "inafanyika kwa kanda, nimeishuhudia maeneo km Shy tena wanaingia interior haswa. Binafsi nasisitiza mshikamano miongoni mwao pia kuimarisha intelijensia ya chama na kubadili wakurugenzi wa chama pale makao makuu kuongeza ufanisi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 


My brother you are filled with the foolishness mind, and your brain has been removed out by the ccm specialist brain remover.
Nani alikuambia kuwa Chadema wanajiandaa kuwa chama kikuu cha upinzani? CHADEMA INA JIANDAA KUWA CHAMA KITAKACHOONGOZA DOLA.

Halafu maneno ya MENE MENE TEKEL NA PERESI yalihusu ufalme uliokuwa madarakani kuondolewa soma vizuri Biblia, Chadema haipo madarakani kwa hiyo hayo maneno ya unabii yanatumika kuiondoa ccm.
I have helped you my brother
 
Haya uliyonena ni hakika kabisa. Kuna upofu na dharau zimejengeka miongoni mwa wanaCDM kwamba wao ndio chamakikuu cha upinzani na bila wao hakuna upinzani. Ni wakati muafaka kwa viongozi wa CDM kujitafakari na kujitazama ili wapate dira
 
Mbona hujaandika jitahada za maksudi za serikali na vyombo vyake vyote kuidhoofisha na hatimaye kutaka kuiua CHADEMA.

Huyohuyo Mbowe na wenzake walimudu kuijenga vyema CHADEMA ikawa na sura kubwa kitaifa, umejiuliza hivi sasa wanakwama wapi? Na kwa nini kipindi hicho hukujitokeza kuwasifu?

Bandiko lako ni rubbish tu. CHADEMA ikifa haikufanyi wewe kuwa na maisha bora. Shida ulizo nazo zimeletwa na CCM hiihii unayoipaka manukato
 
Nachokiona ni kwamba unalazimisha mfano wa kitabu cha Daniel 5:31 kuutumia kwa CHADEMA lakini hakuna kabisa uhusiano huo na CHADEMA kimantiki. Kwanza kabisa ukizungumzia ufalme maana yake ni Dola hivyo Mbowe hana Dola hapa hivyo ungefananisha na mfalme na sio Mbowe kwani hana Dola. Sijaona maana halisi ya kunywea vikombe vya hekaluni inaingia na kuwa chukizo kwa Mungu kwani hakuna sehemu Mbowe ametumia mamlaka yake kufanya maovu mpaka kumuudhi Mungu. Nakushauri uwe unatafuta mifano inayofanana na uhalisia au kuielekeza mifano ya namna hii mahali pake na sio kupachika tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
sasa
Vyovyote iwavyo ikiwa inahujumiwa au inajimaliza, swali Ni je viongozi wanachukua hatua stahiki kukabiliana na kadhia hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe unakumbuka hatua zilizochukuliwa dhidi ya zito ili asiidhuru CDM ulisikia popote? Ila nyiye ccm mna hali mbaya sana bila dola nyie hamna kitu ila kinachofanyika kwa taarifa yako ni kuwataarifu watanzania kuendana na hali iliyopo lakini kiufupi mazingira ya siasa ya vyama vingi kwa sasa ni magumu sana.

Sababu kubwa mtawala hataki kukosolewa na hana uwezo wa kupambana na upinzani kwa hatua waliyofikia wangeruhusiwa kufanya siasa leo hii tungekuwa tunaongea matanga ya ccm.
 
Mbona Ishara wazi zinaonyesha CCM ndo imeanguka Siku nyingi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…