Kisa cha mtoto aliyezaliwa mara mbili

Kisa cha mtoto aliyezaliwa mara mbili

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Mwaka 2016 mwanamke mmoja aitwae Margareta Boemers akiwa mjamzito wa miezi 6 alikwenda kliniki kwa ajili kucheck maendeleo ya ujauzito wake.

Baada ya vipimo mbalimbali ikiwemo ultrasound, ikabainika Mtoto alie tumboni kwake ana uvimbe chini ya mfupa wa uti wa mgongo (tail bone tumor) unaozidi kukua kwa kasi.

Ikashauriwa uvimbe uondolewe haraka vinginevyo uvimbe ule usingeondolewa ungekuja kumletea matatizo ya moyo Mtoto alietumboni pamoja na mama yake, hasa upande wa mapafu maana ungemsababishia kushindwa kupumua vizuri.

Timu ya madaktari na wauguzi 21 ikiongozwa na dr. Olunyika Olutoye (Mnigeria) na Dr. Darrel Cass (mmarekani) walimfanya mjamzito yule upasuaji wa kujifungua, kwa kumtoa kichanga Moja kwa Moja toka kwenye mfuko wake wa uzazi.

Kisha Mtoto yule akawekwa pembeni kwa ajili upasuaji mwngn tena wa kumuondolea uvimbe ule mkubwa uliokua kwenye uti wa mgongo.

Na walipomaliza oparesheni ile, wakamrudishia kichanga kwenye mfuko wake wa uzazi na kuushonea Kama walivoukuta mwanzo, ili Mtoto yule aendelee kukua vzuri amalizie miez 3yake 3 iliyobaki kabla ya kujifungua.

Kwa bahati nzuri,
Miezi 3 ikaisha na mtoto yule akazaliwa salama kwa Mara ya pili na mwenye afya njema, akiwa na kilo 3.2 tofauti na mwanzo alipokua na kilo 1.9

NB: Mtoto yule na mama yake wote wako hai mpaka leo hii.

Nawasilisha
IMG_20240420_023349.jpg
IMG_20240420_023007.jpg
 
Kama tumepiga hatua kwenye Gastric bypass or baloon, hata hii tutaweza.....
Uzuri wa Tanzania kwa sasa, madaktari wana uzoefu na utaalami wa kiwango cha hali ya juu tofauti na zamani.
Mungu ibariki Tanzania
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Gastric bypass ni nini iyo mkuu
 
Mwaka 2016 mwanamke mmoja aitwae Margareta Boemers akiwa mjamzito wa miezi 6 alikwenda kliniki kwa ajili kucheck maendeleo ya ujauzito wake.

Baada ya vipimo mbalimbali ikiwemo ultrasound, ikabainika Mtoto alie tumboni kwake ana uvimbe chini ya mfupa wa uti wa mgongo (tail bone tumor) unaozidi kukua kwa kasi.

Ikashauriwa uvimbe uondolewe haraka vinginevyo uvimbe ule usingeondolewa ungekuja kumletea matatizo ya moyo Mtoto alietumboni pamoja na mama yake, hasa upande wa mapafu maana ungemsababishia kushindwa kupumua vizuri.

Timu ya madaktari na wauguzi 21 ikiongozwa na dr. Olunyika Olutoye (Mnigeria) na Dr. Darrel Cass (mmarekani) walimfanya mjamzito yule upasuaji wa kujifungua, kwa kumtoa kichanga Moja kwa Moja toka kwenye mfuko wake wa uzazi.

Kisha Mtoto yule akawekwa pembeni kwa ajili upasuaji mwngn tena wa kumuondolea uvimbe ule mkubwa uliokua kwenye uti wa mgongo.

Na walipomaliza oparesheni ile, wakamrudishia kichanga kwenye mfuko wake wa uzazi na kuushonea Kama walivoukuta mwanzo, ili Mtoto yule aendelee kukua vzuri amalizie miez 3yake 3 iliyobaki kabla ya kujifungua.

Kwa bahati nzuri,
Miezi 3 ikaisha na mtoto yule akazaliwa salama kwa Mara ya pili na mwenye afya njema, akiwa na kilo 3.2 tofauti na mwanzo alipokua na kilo 1.9

NB: Mtoto yule na mama yake wote wako hai mpaka leo hii.

Nawasilisha
View attachment 2968836View attachment 2968837
Chai.

Wangekuwa wameshamzalisha huyo angewekwa kwenye Neonatal ICU (NICU)hii ni chai.
 
Sahivi teclonologia imekua unafanyiwa upasuaji bila kupasuliwa
 
Duniani kuna vingi vinatokea kwa upekee lakini vipo vyengine hutokea kwa upekee zaidi ya Sana

Akiwa na Ujauzito wa wiki 16 Maggie Biemer alihisi hali tofauti iliyomlazimisha kwenda hospital ....mchunguzi wa awali aliona vichwa viwili kwenye tumbo la mwanamama huyo...

Baada ya uchunguzi zaidi ndio akagundulika na uvimbe uliojulikana Sacrococcygeal Teratoma ambao moja ya madhara yake ni kufeli kwa moyo, kuathirika kwa figo na mfumo wa mkojo

Baada ya kugundulikwa kwa SCT kukafanyika majadiliano ya muda ndio ikaamuliwa

Maggie Boemer akiwa na ujauzito wa wiki 23 chini ya wataalamu bingwa zaidi ya 20 alifanyiwa upasuaji kikatolewa kichanga tumboni kwa mama ake kisha akaondolewa uvimbe huo

Baadae kichanga hicho kikarudishwa tumboni kwa mama ake kwa ajili ya kuendelea na ukuaji wa kawaida

Wiki 13 baadae Maggie Boemer alijifungua tena mtoto huyo kwa njia ya upasuaji ndio wakampa jina la LYNLEE HOPE BOEMER

Na kuwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa Mara mbili duniani

Nikajaribu kugoogle maana ya jina LA mtoto huyo Lynlee -- lake or pool huenda ikawa isiwe maana halisi ila kwa uelewa wangu ni ZIWA LA TUMAINI
 
Attachments

  • FB_IMG_17409095808678832.jpg
    FB_IMG_17409095808678832.jpg
    649.3 KB · Views: 1
  • FB_IMG_17409095761880900.jpg
    FB_IMG_17409095761880900.jpg
    98.2 KB · Views: 1
  • FB_IMG_17409095682785232.jpg
    FB_IMG_17409095682785232.jpg
    23 KB · Views: 1
  • FB_IMG_17409095616438415.jpg
    FB_IMG_17409095616438415.jpg
    44 KB · Views: 1
  • FB_IMG_17409095502577958.jpg
    FB_IMG_17409095502577958.jpg
    49.1 KB · Views: 1
  • FB_IMG_17409095413285246.jpg
    FB_IMG_17409095413285246.jpg
    41.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom