Wakati akifanya hizo harakati za kujisafisha alikuwa na matumaini kuwa atafanikiwa. sasa iliposhindikana kujisafisha na muda ulikuwa umebaki mchache kwa yeye kutoka Gerezani kwa Msamaha akaona kuwa ni bora ajimalize kuliko kupata huo uhuru wa kupewa ilhali ukweli ni kwamba hakuwa na hatia. Labda alifikiria jinsi jamii itakavyokuwa inamchukulia huko mtaani na akashindwa kuhimili, manake pamoja na kwamba angekuwa huru lakini miongoni mwa watu bado angeonekana muuaji jambo ambalo huenda hakulifanya.