Kisa cha mwanamke wa ziwani

Ni ndefu ya kusikitisha. Nahisi aliyemuua mke wake ndiye aliyemuua na yeye. Tena ni huyo aliyemuua na dada wa mke wake.Inaonekana alikuwa atakuwa na mahusiano na wale wafungwa walioleta ushuhuda kwamba Gordon alikiri. Na kama aliwahi kufungwa humo jela alikuwa anajua namna ya kuingia humo kinyemela. Na inawezekana akiwa jela Gordon alijua hilo na akajitahidi ili atoke amshughulikie. Sasa alipoona balaa hilo akamua kuwahi kabla hajatoka.
 

Hapa kuna nadharia nyingi sana zimezungumzwa kuhusiana na kesi hii, inawezekana ukawa sahihi, kwani bado kuna waandishi wa habari za kiuchunguzi wanendelea kuchimba ili kupata ukweli............... Kama mnavyowajuwa wenzetu, haliwezi kupita jambo likaachwa hivihivi, ni lazima kuna watu watadadisi ili kujiridhisha..................tusubiri.

Kingine ambacho mimi, wewe na wengine huenda tunajiuliza, ni Je iwapo tukio kama hili linatokea hapa nchini, Je Polisi wetu wamejandaa vipi kiuchunguzi, je tunavyo vifaa vya kitekolojia katika kufanya uchunguzi wa kesi za namna hii? Kama inavyojulikana kwamba uchunguzi wa kesi za namna hii zinahitaji fedha tena za kutosha, sasa je tumewawezesha vipi Polisi wetu kumudu kuendesha uchunguzi wa kesi za namna hii? Au yatakuwa ni yale yale ya kusema, "Amejitakia mwenyewe, kwa nini tujisumbue na mtu aliyeuawa miaka 20 iliyopita kwa ujinga wake mwenyewe" nimewaza kwa sauti tu
 
Marhaba mwanangu, ndio nimetoa POP jana na kutokana na kutype hii stori jana usiku, mkono wangu umevimba mbaya, lakini nimeanza kuuchua na Fastrum

Hukuyafanyia kazi yale mawaidha ya Mlevi Babu ee! Pole sn
 
Hukuyafanyia kazi yale mawaidha ya Mlevi Babu ee! Pole sn

Jamani Neggirl, hivi kweli ulitaka mpaka leo takriban wiki 6. mimi na mama Ngina tulale mzungu wa nne!? mie hilo limenishinda, wiki ya tano tu, mkono nimeuweka pembeni,.....................Kwanza ni nani alikuambia kuwa maneno ya mlevi yana ukweli?
Na aende zake huko.....LOL
 
it is an real an interesting story... i real would like to know the killer.... kama ingekua ni movie part 1 ningetatuta kwa udi na uvumba part 2 yake
 
Haha haha aaaaaaaa.. Haya babu nimekusomaa, tusije kuchakachua huu uzi wako wenye mashiko kwa Wanandoa, hasa katika kujaribu kuhakikisha hawaishi kwa vinyongo ambavyo vinaweza kusababisha wao kuishi maisha ya kuviziana viziana. By the way ... natumaini uanaendelea kufuatilia ili siku moja uje utupe habari waligundua nani muuaji.
 

Nimekuwa nikiifuatilia hii kesi tangu 1997, na nimekuwa niki up date data zangu kila tukio, mpaka hukumu ya mwisho..................... usihofu nitaendelea kuweka up date humu.......................
 
Jamani nimeumia sana huyu mume kufa siamini kama kweli alimuua mke wake yaani ashindwe kumwambia hata mtu wake wa karibu mmoja aje akiri kwa mvuta bangi kweli wanaokwenda jela sio wote wana hatia
 
me nimepatwa na utata hapo kwa wazamiaji waliposikia harufu,hivi mwili uliokaa muda wote huo majini bado unatoa harufu???haujawa decomposed completely ikabaki mifupa tu?? au ilikuwa sehemu ya baridi???embu nisaidieni.....
 
Ni sawa LIZAPIA hii ni copy and paste lakini mtoa mada alotuwekea tuone na tujue yaliyojiri ndo maana tunapata muda wa kuichambua,

Habari hii nimeitoa katika vyanzo mbalimbali vya habari mtandaoni na kuitafsiri kwa kiswahili, sio kwamba nilikopi tu na kupest kama LIZAPIA alivyodai. kuna habari zinahitaji uchambuzi wa kina hasa pale unapobadilisha kutoka lugha moja hadi nyingine, la sivyo habari hiyo haitanoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…