Hapa kuna nadharia nyingi sana zimezungumzwa kuhusiana na kesi hii, inawezekana ukawa sahihi, kwani bado kuna waandishi wa habari za kiuchunguzi wanendelea kuchimba ili kupata ukweli............... Kama mnavyowajuwa wenzetu, haliwezi kupita jambo likaachwa hivihivi, ni lazima kuna watu watadadisi ili kujiridhisha..................tusubiri.
Kingine ambacho mimi, wewe na wengine huenda tunajiuliza, ni Je iwapo tukio kama hili linatokea hapa nchini, Je Polisi wetu wamejandaa vipi kiuchunguzi, je tunavyo vifaa vya kitekolojia katika kufanya uchunguzi wa kesi za namna hii? Kama inavyojulikana kwamba uchunguzi wa kesi za namna hii zinahitaji fedha tena za kutosha, sasa je tumewawezesha vipi Polisi wetu kumudu kuendesha uchunguzi wa kesi za namna hii? Au yatakuwa ni yale yale ya kusema, "Amejitakia mwenyewe, kwa nini tujisumbue na mtu aliyeuawa miaka 20 iliyopita kwa ujinga wake mwenyewe" nimewaza kwa sauti tu