Kisa cha mzee Yusuph

Kisa cha mzee Yusuph

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Hazikuwa habari njema sana siku mzee Yusuph gwiji wa taarab za kileo pale alipotangaza rasmi kuachana na mziki huu na kumrudia Mola wake...
Habari zilienea kwa kasi na mijadala ilikuwa mingi..! Wengi wakimpongeza kwa hatua yake hiyo

Mimi napingana naye...kilichomfanya aachane na huo muziki(kwa tafsiri yake ni dhambi kwa imani yake)hili ni tusi na dhikaha kwa mziki huu adhimu...lakini yametokea haya kulingana na mahitaji ya nyakati na kile alichokuwa anafanya
Kiuhalisia mziki wa mwambao(taarab) ni mziki wa asili wenye kuheshimika mno ambao kiasili ulitumika kuelimisha kuonya kufundisha kuburudisha na kufurahisha, haukuwa na matusi vijembe dhihaka wala mambo ya kishetani
Miaka ile ya 1987 ndio taarab ilianza kubadilika na kupoteza mwelekeo...ujio wa Khadija Kopa (malkia wa mipasho) na Nasma Khamis Kidogo RIP kulibadilisha mwelekeo mzima wa taarab

Leo hii taarab ni mziki wa kusutana na mambo yote mabaya..ikuwemo ushoga umalaya bifu kusemana wazi wazi nk...
Mzee Yusuph ajiuzulu tu kwa matendo yake na nyimbo zake za kishetani lakini asihusishe na mziki huu adhimu wa taarab sio haki
 
1472915628134.jpg
1472915631665.jpg
1472915636085.jpg
 
whats your point sasa hapa yy ameacha sababu ya dini yake inamkataza ila andiko lako linajigonga gonga mambo ya kiimani yaachwe pls aheshimiwe kwa uhuru wake
Hakuna nilipotaja imani yake tafadhali sana BAFA usipotoshe! Nilichoandika mimi ni kutaka kutetea music wa taarab usiingize virus kwenye hii post
 
[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Kweli mshana hamna uhuni ambao hajaufanya acha tu amludie Mungu na kwenda makka kuhiji
 
Hakuna nilipotaja imani yake tafadhali sana BAFA usipotoshe! Nilichoandika mimi ni kutaka kutetea music wa taarab usiingize virus kwenye hii post
kilichomfanya aachane na huo muziki(kwa tafsiri yake ni dhambi kwa imani yake)hili ni tusi na dhikaha kwa mziki huu adhimu... HAYA MANENO YAKO ULIOANDIKA UMEONA
 
basi nikwambie tu kua katika uislam mziki wowote ni kharam sio kwamba sijui taarab zamani sijui bongo freva sijui kaswida hazi pigwi msikitini wala kwenye QURAN hapana penye mtume ameimba au yesu ameimba
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Hazikuwa habari njema sana siku mzee Yusuph gwiji wa taarab za kileo pale alipotangaza rasmi kuachana na mziki huu na kumrudia Mola wake...
Habari zilienea kwa kasi na mijadala ilikuwa mingi..! Wengi wakimpongeza kwa hatua yake hiyo
Mimi napingana naye...kilichomfanya aachane na huo muziki(kwa tafsiri yake ni dhambi kwa imani yake)hili ni tusi na dhikaha kwa mziki huu adhimu...lakini yametokea haya kulingana na mahitaji ya nyakati na kile alichokuwa anafanya
Kiuhalisia mziki wa mwambao(taarab) ni mziki wa asili wenye kuheshimika mno ambao kiasili ulitumika kuelimisha kuonya kufundisha kuburudisha na kufurahisha, haukuwa na matusi vijembe dhihaka wala mambo ya kishetani
Miaka ile ya 1987 ndio taarab ilianza kubadilika na kupoteza mwelekeo...ujio wa Khadija Kopa (malkia wa mipasho) na Nasma Khamis Kidogo RIP kulibadilisha mwelekeo mzima wa taarab
Leo hii taarab ni mziki wa kusutana na mambo yote mabaya..ikuwemo ushoga umalaya bifu kusemana wazi wazi nk...
Mzee Yusuph ajiuzulu tu kwa matendo yake na nyimbo zake za kishetani lakini asihusishe na mziki huu adhimu wa taarab sio haki
Labda kaukwaa.
 
Ndio yupo sahihi katika uislam kitu kinachoitwa music ni haramu iwe taarabu asil au mpya mipasho sijui na nini vyote haramu. Kwa hyo point ya mzee yusuph bado iko pale pale kaacha haramu
Kumbe ni wengi ambao hawakunielewa
 
Back
Top Bottom