Kisa cha panya na hali halisi ya siasa za Tanzania

Kisa cha panya na hali halisi ya siasa za Tanzania

musicarlito

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2020
Posts
591
Reaction score
909
Siku moja panya katika pita pita zake nyumbani kwa binadamu(chumbani),aliona kitu na haraka akang'amua kuwa ulikuwa mtego(alishawahi kuona kitu kama hicho kimenasa wenzake nyumba tofauti tofauti na akahudhuriq mazishi...mtego ulikuwa mbaya haukuacha manuscript

Kwa hofu alienda kumdokeza kuku wasaidiane kuutegua kwa sababu binadamu hakuwa na nia nzuri na panya...lakini kuku alimbeza akamwambia ngekusaidia lakini nna kazi nyingi isitoshe halinigusi moja kwa moja

Panya alikata rufaa akaenda kwa mbuzi...looh!mbuzi alicheka sana...akamwambia mtego ule si kitu kwake kwani angepiga teke moja wala usingefanya lolote...isitoshe yeye huwa hanging ndani kwa binadamu

Panya alizidi kuhamanika...katika hali ya upweke na kukata tamaa alijiambia labda nimshirikishe ng'ombe angeweza lau kunipa hata wazo nifanye nini...ng'ombe kama mbuzi alimdhihaki na kumfukuza kwa dharau...panya alikata shauri kuishi kwa tahadhari lakini kutosogelea mtego kabisa

Siku si nyingi siku moja binadamu alikuwa anataka kuchukua vyakula alivyoficha uvunguni huko karibu na mtego...masikini asijue mtego wake umeshika tayari windo lakini windo lenyewe!😮‍💨

Alipopeleka mkono tuu...lahaula!alipiga mayowe yalioshiria maumivu makali...walipomulika kurunzi/tochi waligundua nyika mbaya mwenye sumu Kali alikuwa kanaswa kwenye mtego...!

Huduma ya kwanza ilifanyika halafu mgonjwa alikimbizwa hospitali,mgonjwa hali mboga ya wote na kwa kuwa ugonjwa ni dharura,mgonjwa aliomba supu ya kuku...tukanunue wakati yuko nyumbani😄...masikini kuku alishangaa anakimbizwa hali sio sikukuuu akawa amekwenda kumlaki 'bwana' mawinguni

Taarifa za mgonjwa zikawafikia watu wengi...ndugu jamaa na marafiki walimiminika nyumbani...loh kuwahudumia chakula ikawa changamoto hasa kitoweo...likaja wazo achinjwe mbuzi...safari ikawa zamu ya mbuzi kushangaa kulikoni nakimbizwa sio sikukuu? Muda haukuwa mrefu nae aliishia sufuriani

Sikio la kufa halisikii dawa...sumu ya nyoka ilimuathiri vibaya mgonjwa,siku hazikuwa nyingi hali ikazidi kuwa mbaya na hatimaye aliaga dunia akaenda kumlaki 'bwana' mawinguni...

Marehemu tajiri anazikwa na kila mtu hata kama hana dini,ingetoka wapi mboga ya kulisha watu wote wale? Masikini safari hii n'gombe alijua kabisa ni zamu yake...aliishia kwenye masufuria kabla hata ya sikukuu

Kwa wakati huu watu wengi wanalilia haki,CHADEMA imebeba agenda hii....wapo wanufaikaji wachache wanaona CHADEMA ni kama anataka kuwaondolea utulivu wa kulamba asali

CHADEMA ni panya

KUKU ni chawa na wanufaikaji wanaodanganywa kwa pesa kidogo kama wasanii...wajumbe ...kwa ujumla machawa

MBUZI ni tabaka la kati la wanufaikaji kama watumishi mfano Polisi,Waalimu na kada nyingine ambao wao wana uhakika wa matibabu kwa BIMA...uhakika wa chakula na makazi na huduma kama Elimu nk

NG'OMBE...Hawa ni wanufaikaji wa moja kwa moja na mifumo yao mfano( chama tawala )kutoka kwa watawala wanaojifaidisha kwa rasilimali za wengi kwa mishahara minono namna na zote za fahari kutoka kwa wanyonyaji...hapa wapo wakurugenzi,mawaziri,makatibu wakuu au nafasi za teuzi...hawa wanamuona panya kama kitu kisichofaa na sio mnyama mwenzao kila mara wanamuuliza binadamu tukusaidie 'kumfuta' huyu? Wasijue wote wameumbwa na Mungu

Halafu binadamu ni watawala wanaonyanyasa viumbe wenzao bila kujua nao ni viumbe muumba ni mmoja Mwenyezi Mungu

NYOKA ni UOVU(Mifumo kandamizi ya unyonyaji na unyanyasaji)

Mwisho upo...Nyakati ngumu hazidumu
stock-vector-rat-try-to-stop-friend-to-trapped-because-cheese-ideal-for-illustration-about-bus...jpg
 
Back
Top Bottom