aise
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 5,175
- 16,488
Habari zenu wakuu, rafiki yangu wa mafia ananiambia hivi.
Mimi nimezaliwa na kukulia kisiwani mafia, shuleni kwetu tangia naanza darasa la awali mpaka namaliza darasa la saba, hapakuwahi kuwa na mwanafunzi mkristo, sote tuliwa wa imani ya uislamu. Aliwahi kuja mwalimu mmoja wa imani ya ukristo lakini hakukaa sana akaondoka.
Kwa ufupi sisi tangu utotoni katika ukuaji wetu tulifundishwa kwa msisitizo sana kuwa mtu ambaye si wa imani yetu, huyo mtu haifai hata kumsogelea kwa namna yoyote ile, mtu ambaye si muislamu ni sawa au ni zaidi ya nguruwe au mbwa. Mara kadhaa walipokuja watalii wa kizungu, hao ndiyo tuliaminishwa kabisa ni watu wanaopigana na Mungu anayetupatia uwezo wa kuishi. Alipopita mzungu tulikuwa tukitema mate kwa nyuma kuashiria ni kitu ambacho hata kukiona ni dhambi.
Mimi nilipomaliza darasa la saba nilitafutiwa uhamisho na nikahamia Vikindu, na hapo nilianza kidato cha kwanza. Kwakweli niliteseka sana siku za mwanzo pale shuleni, maana nyumbani Mafia nilifundishwa kuwa mtu asiye wa imani yangu ni haramu na haitakiwi hata nimsogelee.
Darasani nilipangwa dawati moja na mkristo, aliyeitwa Yohana Frank, kwakweli nilikaa naye kwa taabu sana nikiamini kukaa dawati moja na yeye natenda madhambi na nitaikosa pepo. Baada ya kuzoea mazingira ya shuleni nilipata rafiki wa imani yangu aliyeitwa Omari.
Cha kusikitisha huyo Omari alikuwa na marafiki wa imani ya kikristo, na walikuwa wakigawana vyakula pale shuleni. Mimi kwa mazingira niliyokulia na mafundisho niliyofundishwa tangu utotoni nilikuwa na wakati mgumu sana pale shuleni. Watu nilioaminishwa ni haramu na haitakiwi hata kuwasogelea, iweje leo nikae nao meza moja na kula pamoja nao?
Kwakweli nilikuwa nikijiuliza maswali mengi sana, na nikaanza kuyafikiria upya mafundisho yote niliyofundishwa tangu utotoni ikiwa yana mantiki au la! Nilianza kuifikiria imani yangu yote kwa ujumla. Mpaka leo nimeanza kufikiria kama kweli Mungu yupo? Huyu Mungu niliyefundishwa tangu utotoni yupo? na vipi kuhusu hawa miungu wa imani nyingine tofauti na imani yangu?