Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,884
- 5,235
Salaam wanahistoria!
Leo nilikuwa mahala fulani napiga soga na kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki. Soga zetu ziligusa maeneo mengi hasa Historia ya Tanzania wakati wa utawala wa Mwalimu. Kwa sababu ya utofauti mkubwa wa kielimu, umri na uzoefu wa maisha, nilikuwa msikilizaji zaidi huku nikimchokoa zaidi.
Alinieleza kuwa changamoto kubwa ya utawala wa Mwalimu, ilikuwa ni kulewa madaraka kwa wengi wa viongozi wake hasa MaRC na MaDC. Alinipa visa vichache, kigeni kwangu kilikuwa cha RC wa Kilimanjaro, aliyeitwa Namfua. Kuwa;
Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro na Chama viliamua kuwa jengo lilokuwa la Watawa huko Kilimanjaro, lichukuliwe na kufanya shughuli za serikali. Walipouliza, wao wataenda wapi na wanachukua kwa utaratibu gani; jibu lilikuwa ni kuwa serikali na chama imeamua—enzi hizo, zilikuwa ni za chama kushika hatamu(Party Supremacy), RC pia alikuwa ni Katibu wa Chama wa Mkoa. Kisha kupewa siku 21 wawe wamehama.
Watawa wale, walimlilia Padre wao, aliyewapa majibu kuwa yeye hana cha kufanya, bali wafunge na kuomba. Kabla ya muda wa siku 21 kufika, RC Namfua, alipata safari ya kikazi nje ya nchi, maagizo yake ilikuwa akirudi, watawa wale wawe wameondoka (maana siku hizo 21 zitaisha akiwa nje ya nchi).
Aliporudi safari yake, baada ya kufika tu Airport, swali lake la kwanza likawa 'Watawa wameshahama?' Jibu alipewa kuwa bado wapo.
Basi, Namfua akaagiza Defender mbili (101 enzi hizo) za askari, wenye silaha, ziongozane naye na kuanza safari kuwafuata watawa wale. Kabla hajaenda hata ofisini kwake, moja kwa moja kutoka Airport, bila hata Protocol ya kuongozana na DC, na kuwatanguliza Askari mbele, msafara ulielekea kwa watawa wale.
Wakiwa njiani, alikatiza mbuzi, dereva katika harakati za kumkwepa; alifunga breki za ghafla, RC ambaye hakuwa amefunga mkanda, alichomokea kwenye windscreen, na maisha yake yakaishia pale. Msafara ukageuza, na kuwa msafara wa msiba.
Kisa hiki, na cha Dr Kleruu, vyaelezwa kuwa ndio vilichangia walau kuwafanya viongozi wa Nyerere kuwa na ustaarabu kwa wananchi.
Cc: Mohamed Said JokaKuu Sky Eclat Pascal Mayalla Red Giant