Kisa cha Shariff Abdallah Attas na mwalimu Julius Nyerere ofisi ya TANU baada ya uhuru

Ngamiani hilo jina unalojinasibu nalo huna kun'yya nalo kabisa wenyewe wazaliwa wa ngamiani tumekaa kimya!!
 
Haiwezekani, lah uswahiba umekufa au haujali yanayojiri kwa swahiba
Platozoom,
Nimerejea tena.
Uzee una starehe zake na kunwa ni mbili unaweza sana kulala na kusema.
Katika minhaji hii hapo ''kusema,'' weka ''kuandika.''

Hebu nisome huku ukitembea katikakati ya mistari yangu na huku ukiwasikiza
wanasiasa wenyewe:
Mohamed Said: MHESHIMIWA KATANI AHMED KATANI (CUF) MBUNGE KIJANA WA TANDAHIMBA (UKURASA WA NYONGEZA)

MHESHIMIWA KATANI AHMED KATANI (CUF) MBUNGE KIJANA WA TANDAHIMBA (UKURASA WA NYONGEZA)

Inawezekana kabisa kuwa hata kwa mbali au hata kwa ndoto mbaya ya kutisha ya jinamizi Mh. Ahmed Katani alipatapo kufikiri kuwa itatokea siku yeye atasoma tamko la uamuzi wa kumfukuza Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kutoka CUF. Kama wasemavyo wanasiasa wenyewe, siku ni muda mrefu sana katika siasa. Mwandishi alikutana na Mh. Katani siku chache zilizopita alipofika nyumbani kwake akiongozana na Mh. Riziki Shahari Mbubge wa Mafia Viti Maalum wakitokea Bungeni Dodoma. Mazungumzo aliyofanya na Mwandishi kwa muda mfupi kama ungewasikiliza utadhani wawili hawa walikuwa wanajuana kwa muda mrefu. Msomaji anaweza kusoma utangulizi hapo chini wa ukurasa ambao Mwandishi aliandika kama ufunguzi wa matumaini kuwa iko siku Mh. Katani atakuja na historia ya maisha yake katika siasa za upinzani. Mh. Katani Ahmed Katani tayari keshaingia katika jedwali la historia kwa kusoma tamko la kumfukuza Prof. Lipumba kutoka CUF.

Hivi yawezekana kwa Prof. Lipumba kumtazama usoni kijana wake Mh. Katani na akasema maneno aliyosema Julius Caesar, ''Et tu Brute?''

Msikikilize Mh. Katani hapo chini:


Utangulizi
Mheshimiwa Katani Mbunge wa Tandahimba ni kijana kwa maana halisi ya neno lenyewe. Katika muda mfupi wa kuzungumza nae kwa mara ya kwanza akisubiri kikombe cha kahawa alipopita nyumbani kwa Mwandishi, Mwandishi amegundua kuwa Mh. Katani amekalia kitabu ambacho ikiwa atakiandika kinatosha kuwa rejea ya kueleza adha za siasa za upinzani khasa wakati wa uchaguzi mkuu. Ukurasa huu umefunguliwa rasmi kumsubiri Mh. Katani afunguke kwa faida ya wapenda demokrasia...


Mheshimiwa Katani Mbunge wa Tandahimba
 

Dah, hao waliotajwa na hao kwenye picha nawaona hivi machozi. Maalim ulipomtaja Bi Mariam Zialor na Sauda nikahisi utamtaja na Bi Eshe Sururu.

Nnazikumbuka kumbuka enzi za Mariam na Hussein Shebe.
 
Ahlaan Wasaalan Maalim Faiza...
Kumekucha.

Huu ukimya wako naamini Wanabarza wengi tulikuwa tunajiuliza kulikoni?
Majlis ilipooza.

Asalaam Alaikum.

AlhamduliLlah nipo Alama, ni majukumu ya hapa na pale na hii holiday season iliyopita nilirundikiwa wajukuu wote basi ikawa hata muda wa kuchangia humu sina, si unajuwa hawa wanetu siku hizi wakikuwachia watoto zao wanakupa na time table, aah sisi wao tuliwalea kwa time table za kichwani. Na kama hukufata time table waliokuachia basi una kesi ya kujibu.

Nakusoma Maalim, umenitajia kaka na Dada zangu wa karibu kabisa. Akina Hennin, Hussein, Chico, na Da Mariam. Bila kumsahau Salum Hiriz. Aah nilitamani nimsome na Ali Bobo, Abdallah Awadh, Abby Sykes, Salmin Tamim, Marehem Ali Ghafur (mabichwa).

Aah, ni mambo adhyim na Adim hayo.

Juu huko nimemsoma Mzee Tuli, jee huyo ni baba yake Dr. Mohamed Tuli?
 
Maalim Faiza,
Nimefurahi sana kukusikia.
Allah atukuzie wajukuu zetu.

Amin.
Hakika najua jukumu ulilonalo.

Katika hao wajukuu unao waume zako na mawifi na najua hutaki kujiharibia kwa hawa
waume kwani ni ghali na adimu hivi sasa hapa mjini wanasakwa kwa udi na uvumba.

Ukiwafurahisha mawifi na kaka zao wanafurahi, ''and they will be looking forward to go
to their heartthrob next holiday.''

Wajukuu ni watamu kuliko watoto kiasi unataka Allah angetupa kwanza wajukuu kisha
wafuatie wana.

Ali Bob na Abdallah Awadh watu muhimu sana katika mji wa Dar es Salaam na wataacha
historia nzuri In Shaallah.

Watu waungwana, wastaarabu.
Kila shughuli wao hutaka kuwatumikia watu tu, kuwaandalia chakula na nini.

Siku moja nilimuuliza Ali Bob, ''Kaka iweje wewe na Abdallah Awadh siku zote nyie ni
waandazi?''

Ali Bob
akanijibu kuwa wakati mwingine wao hualikwa shughuli kama watu wengine lakini
wanachelea shughuli kuharibika ndipo husimama kuandalia.

Akaongeza na kusema wao wanawajua watu wengi wa Dar es Salaam na anapompokea mtu
anajua amkalishe na nani.

Anawajua kuwa nani hali nyama, nani hali pilau kwa hiyo anawatengea jamvi lao maalum na
hivyo taklif huondoka.

Nami umenipeleka mbali.
Siku hizi shughuli hatuli tena katika sinia tumekizunguka chakula kama ilivyo ada.

''Catering is taking over.''
Kila mtu na kisahani chake mkonini, ''already packed.''

Maalim Faiza huu ni msiba.

Nakutakeni radhi Wanabarza huenda wengine wasielewe lakini hii ndiyo ilikuwa Dar es Salaam
tuliolelewa sisi miaka hiyo.

Dr. Tulli ni mtoto wa Madhehebi Tulli.
 

sasa kwa porojo kama hizi kweli tutafikia nchi ya viwanda????
"et na wewe msomi na hivi ndo vitu unavyojinasibu navyo"

wewe ni mwandishi 'mwanasesere'
 
sasa kwa porojo kama hizi kweli tutafikia nchi ya viwanda????
"et na wewe msomi na hivi ndo vitu unavyojinasibu navyo"

wewe ni mwandishi 'mwanasesere'

"Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba".

Nnauhakika hujaelewa kinachoongelewa. Hayo ya Dar za enzi hizo tuwachie sisi, Alama Mohamed Said kishawaomba radhi wana jamvi.

Jee, umewahi kumsikia Mshume Kiyate?
 
sasa kwa porojo kama hizi kweli tutafikia nchi ya viwanda????
"et na wewe msomi na hivi ndo vitu unavyojinasibu navyo"

wewe ni mwandishi 'mwanasesere'
Mtanganyika...
Ndugu yangu mimi si lolote wala si chochote kaka.
Sina moja nilijualo mie kwa hiyo unistahamilie tu ndugu yangu.

Mwanasesere mbona ana afueni?
Mimi ni Karagosi.

Huyu Karagosi ni mwanasesere zuzu tukimwangalia vituko
vyake pale Mnazi Mmoja siku za Eid.

Aliyekuwa akimcheza (puppet on a string) alikuwa mtu mmoja
anaitwa Juma Mlevi lakini jina lake khasa ni Juma Sulemani.

Huyu Juma Mlevi alikuwa katika TANU mstari wa mbele katika
vijana na alihudhuria Mkutano wa Kura Tatu Tabora, 1958.

Sasa mimi ni mbumbu na Waarabu wana msemo, ''Sababu huondoa
ajabu.''

Ukishakubali kuwa mimi ni mbumbu utakuwa huna tena sababu ya
kuja hapa barazani kunitukana maana tayari mimi ni maadhura.

Maana yake nishasamehewa kwa kuwa punguani.
Kama kweli nilitegemewa mimi kuendeleza viwanda....
 
Mkuu Mohammed Said kwa maoni yangu ulitakiwa uwe part time lecture for African/East African history hususan kwenye hizi East African colleges and universities
Waonekana una hazina kubwa sana kwenye historia Ya nchi hii. Kutokushare hiyo rich history uliokuwa nayo Ni kutotutendea haki sote wenye kiu Ya kutaka kufahamu na kujifunza historia Ya nchi hii
Ni ombi langu binafsi tu
 
Mtanganyika...

Hapana mimi sijapata kulalamikiwa ''udini,'' na wasomi wakubwa waliofanya
''review,'' ya kitabu changu cha Abdul Sykes na paper nyingine nilizowasilisha
katika vyuo kadhaa Afrika, Ulaya na Marekani ila hapa JF na watu mfano
wako.

Lakini kila ninapoomba ushahidi wa hilo wanashindwa kutoa na wengine kama
wewe huishia matusi.

Yawezekana ndugu yangu unahangaishwa na wivu na hasad na haya ni maradhi
mabaya ya nafsi na husababisha kensa mwilini madaktari wamethibitisha hili.

Hapa JF kuna wengi wanapenda kunisoma.

Ama hilo la ''porojo'' Allah hakunijalia kipaji hicho na ndiyo maana nimeweza
kuchapwa na Oxford University Press (East Africa) na New York.

Ndiyo maana pia kitabu changu kilipotoka 1998 mabingwa wa African History
John Iliffe na Jonathon Glassman wakanifanyia ''review,'' katika Cambridge
Journal of African History.

Ndiyo maana naalikwa kwingi ndani na nje ya nchi kuhadhiri.

Huu ndiyo mchango wangu kwa taifa hili kwa kuihifadhi historia ambayo tayari
ilikuwa imeshapotea.

Hapo chini niko VOA Washington wamenialika kwa mahojiano waliposikia nipo
mjini.

 
Sheriff,
Ahsante kwa kuniwazia makubwa.
Nimejitahidi kuandika mengi ninayoyajua.
 
Sheriff,
Ahsante kwa kuniwazia makubwa.
Nimejitahidi kuandika mengi ninayoyajua.

Obviously yote uyajuayo hujayamaliza yote na I have a feeling that unayo Mengi sana ambayo hayajachapishwa wala kuelezwa
Tafadhali funguka
 
Obviously yote uyajuayo hujayamaliza yote na I have a feeling that unayo Mengi sana ambayo hayajachapishwa wala kuelezwa
Tafadhali funguka
Sheriff...
Ni kweli huwezi kuandika yote.

Inawezekana ninayo mengi ambayo sijasema kwa sababu hii au ile au
kwa sababu ya kusema haipo.

In Shaallah tusibiri ikitokea fursa nitazungumza.
 
Mohamed, unakosea unaposema historia ya hao wazee ilifutwa. Labda mchango wao ulipuuzwa lakini historia yao haikufutwa. Huwezi kufuta historia. Haiwezekani.
 
Mzee Said kuna watu wengi ktk TAA ambao nimewasoma kwa mara kwanza ktk bandiko lako.

Kitabu chako hicho kinaitwaje na kinapatikana wapi? Nadhani nikikipata nitaongeza elimu na ufahamu wangu kuhysu historia ya Tanganyika.


Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…