Kisa cha wanawake wa JF kuitwa vikongwe/vibibi

Uzee ni baraka sana aisee, na ni kwa neema tu ya Mungu tumeweza kufikia uzee Wengi wamekufa wakiwa bado vijana wadogo kabisa, sisi tuliofika huku tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu. Sasa kumcheka mtu kwa sababu ana umri mkubwa ni upungufu wa akili, kwa sababu wengi wetu tunaomba na kutamani tuendelee kuwa hai, ikimaanisha tunatamani tuishi hadi tuwe vikongwe, so as long as mtu anaendelea kuishi uzee utamkuta tu.

Ukiwa interested na mtu mfuate tu PM, muulize umri wake, tumianeni na picha then ndiyo muanze kufikiria na mengine. Sio hadi vikongwe eti tutumie ID na avatars za wazee jamani, msitunyime raha tafadhali
 
Sio hadi vikongwe eti tutumie ID na avatars za wazee jamani, msitunyime raha tafadhali[emoji4][emoji4][emoji4] sijasema ID za wazee hapana jamani
 
Nilijua ni pisi kali baada ya kuona avatar yake nikaingia pm mambo yakaenda poa tuka date tukutane 77 hotel pale Arusha.

Niliwahi kufika mapema hapo hotel ili nimuone mpenzi wangu atakapokuwa anaingia jinsi alinyo kimwondoko mapozi nk.

Sitasahau siku hiyo baada ya kujikuta nipo na shangazi yangu na sio pisi kali niliyemtarajia yaani kumbe nilikuwa nachat pm na dada yake baba yangu mzazi,dadeki nilifuta kila kitu nikafungua acc mpya hata shangazi alifuta acc yake na sijui anatumia jina gani ila najua tunaye hapa JF

Yaani tangu siku hiyo nikawa naiheshimu JF na namheshimu kila member
 
 
Umeandika ya sawa kabisa.

Ila umezidi kuwaondolea hali ya kujiamini wanawake wa jf, subiri utaona kitakacho fata humu katika hui uzi, utaona mabinti vigoli au wadada wa makamo watajiita wao ni vibibi wakati si kweli.

Hawa viumbe sijui kwanini hawajiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…