Kisa Chid Benz, bifu la Lady Jaydee na Ray C laibuka upyaaaaaa

Nachokumbuka ni kwamba kila ijumaa nilikuwa naondoka shuleni mapema kwa ruhusa ya kwenda kusali ila kiukweli nilikuwa naishia salon moja mtaani jamaa alikuwa na deck ya cd(ya kwanza pale wilayani) na alikuwa na cd ililuwa na ngoma kadhaa za Ray C. Ki ukweli Ray C nilizipenda nyimba zake sana ila pia nilimpenda yeye kama yeye, lile jicho halikuwa la kawaida kwa kipindi kile kwa umri nilio kuwa nao. Mpaka leo jicho kubwa la mviringo ni kigezo kikubwa sana kwangu ukitaka nikuhonge hadi hela ya mwisho mfukoni. Ray C aliniteka sana japo Jide nae alikuwa na ngoma zake nzuri hasa alizoshirikishwa
 
Kweli kipenda roho ula nyama mbichi.
Jide sijawahi mkubali naona anaimba kwaya siyo muziki wa kawaida wa mtaani Kama Afro Pop, dance, n.k.
Dah mie jd hunipangi aisee,ile nyumbani lounge ,thai village, Machozi band ilikua bandika bandua hadi sasa nikiwa the marz naenda pale kumsalimia ,she is my sister kwa kweli
 
Mwambie Ray C kama ameamua kupambana na 'teja' mwenzake basi wapambane wenyewe asianze habari za kumhusisha mtoto kwamba eti yeye sasa ana mtoto.
Amuweke mtoto nje ya ligi yao asijemchulia bure.
 
Kwenye kipaji, Jide kamuacha mbali sana Ray C

Tokea ametoka miaka ya 2000 Jide kaachia hit songs back to back mpaka leo hii, lakini Ray C nina hakika turudi hata 10 years nyuma niambie katoa hit song gani ndani ya huo muda hakika hutaiona. . .

Hivyo Jide ndio Malkia

Tukija kwenye hii tweet, Ray C ana kiherehere tu ina maana hafatilii kinachoendelea kiasi kutojua kuwa ile tweet Jide alimjibu chuma??

Al in all, Jide 95% Ray C 5%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…