Kisa Chid Benz, bifu la Lady Jaydee na Ray C laibuka upyaaaaaa

Kisa Chid Benz, bifu la Lady Jaydee na Ray C laibuka upyaaaaaa

Kwenye kipaji, Jide kamuacha mbali sana Ray C

Tokea ametoka miaka ya 2000 Jide kaachia hit songs back to back mpaka leo hii, lakini Ray C nina hakika turudi hata 10 years nyuma niambie katoa hit song gani ndani ya huo muda hakika hutaiona. . .

Hivyo Jide ndio Malkia

Tukija kwenye hii tweet, Ray C ana kiherehere tu ina maana hafatilii kinachoendelea kiasi kutojua kuwa ile tweet Jide alimjibu chuma??

Al in all, Jide 95% Ray C 5%
Kaa pembeni jay dee hakuwahi kumuacha Ray c ,jay dee han hit sema ni mtu ambaye kapta sapot nzuri kwa wasanii wa kiume kaimba nyimbo kibao na Mwana Fa ,professor j na wengine kibao.

Ray c jeshi la mtu mmoja wewe ,ngoma zake zimehit jay dee kazi kutafuna maneno.

Enzi hizo wazee wa viuno alikuwa Ray c na best wa Marlaw huyo jay dee wako kazi kuimba kama mwanaume
 
You're entitled to your own opinion bro but pls be frank, she's not relevant a long time ago.

Nilimaanisha ile sassy & sexy image na lifestyle ya Ray C ipo more relevant na kizazi cha sasa kuliko Lady jay dee ambaye yake ipo more matured.

Sikuongelea level of fame cause it's obvious amekuwa inactive for too long na hii ni Bongo sio hollywood
 
Kwa kizazi cha sasa katoa hit gani Ray C? Wote old school kwa sasa ni wa enzi zetu tu.

Nimesema "Lifestyle au image". Sijaongelea hitz

Ukifuatilia chochote wanachokivaa au lifestyle ya hawa socilites au waimbaji wa sasa. Ray C alishakifanya au bado anakifanya vizuri zaidi.

Kwa hiyo inampa edge kwa kizazi cha sasa tofauti na jide ambaye anaonekana irrelevant kwa kizazi cha sasa nje ya muziki
 
Nachokumbuka ni kwamba kila ijumaa nilikuwa naondoka shuleni mapema kwa ruhusa ya kwenda kusali ila kiukweli nilikuwa naishia salon moja mtaani jamaa alikuwa na deck ya cd(ya kwanza pale wilayani) na alikuwa na cd ililuwa na ngoma kadhaa za Ray C. Ki ukweli Ray C nilizipenda nyimba zake sana ila pia nilimpenda yeye kama yeye, lile jicho halikuwa la kawaida kwa kipindi kile kwa umri nilio kuwa nao. Mpaka leo jicho kubwa la mviringo ni kigezo kikubwa sana kwangu ukitaka nikuhonge hadi hela ya mwisho mfukoni. Ray C aliniteka sana japo Jide nae alikuwa na ngoma zake nzuri hasa alizoshirikishwa
Kuna ile Ngoma ya ray c inaitwa NATAKA KUWA NAWE MILELE alooo ni balaa kipindi hicho...
 
Jide ana kisirani sana, anajiona star mkubwa sana na kiburi ila pia stress zinamsumbua.

Kuna siku nilikuwa airport kwenye yale madirisha ya kukata ticket na kuulizia ratiba za ndege,nikashangaa mtu ananigusa begi eti kaka naomba nipishe nina haraka,nikamwambia ungewahi kabla yangu subiri huko, basi akaanza kufoka pale, ana kisirani sana nadhani ndo maana hana hata marafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom