La Princesa
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 1,049
- 1,160
Duh
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mchungaji katunzi yuko dar hapo mpeleke vifungo vya uchawi vimtoke sikumoja tu utabadili maisha yake msaidie rafiki yako eagt city center njia ya mbagala kitua stand ya shamba juu inapita reli ninamfano kama huo maombi ni bure kabisa ni True pastor huyu.Kuna watu hapa duniani wanapitia maisha magumu kwenye ndoa.
(Samahani mimi sio mwandishi mzuri wa story)
Kuna mwenzangu tulisoma naye O level, mimi niliendelea A level na yeye akaenda DIT kipindi hicho ikiitwa Dar Tech, hatukuonana miaka mingi sana na sikujua yupo wapi. Kwa bahati tu nikawa nimepata uhamisho kwenda ofisi nyingine, nikamkuta jamaa pale ofisi na ana madaraka makubwa kuliko mimi.
Na wafanyakazi wa pale anawanyanyasa sana ila wakaona kwangu ni tofauti kabisa akiniona au akiwa anatoa majukumu kwangu huwa anakuja kuniomba labda kwakuwa najua kila kitu chake na najua uwezo wake kwenye fani ile maana tuna fani moja.
Nikaambiwa huyo bosi hana ushirikiano na wenzake hata michago ya kijamii hatoi, kwahiyo watu wanamwangalia tu ngoja apatwe na tatizo tutamkomesha haswa. Kusikia hivyo nilishtuka sana ila nikasema labda ni maneno ya watu kwakuwa ni mgeni.
Pia niliambiwa kuwa hawajawahi kumuona anakula chochote mpaka anatoka kazini.
Kuhusu chakula nikanza kwenda ofisi kwake kumwita kuwa twende tukanywe chai na chakula kwa muda wa wiki hivi akagomesha kuwa hanywi chai wa chakula kwenye restaurants za hapa kazini kuwa sio safi kumbe alikuwa anaogopa kununua.
Ikapita kama mwezi nikamwambia twende tutoke nje kuna sehemu nimeona chakula kizuri nitakununulia jamaa akakubali kwa shingo upande tukaenda tukala, kesho yake ikawa hivyo hivyo na kuendelea, mpaka ikafika muda akawa anakuja ofisini kwangu kuniambia twende kula ila yeye ni kuagiza tu kulipa ananiangalia mimi ndo nilipe ikaenda kama kwa muda wa miezi miwili na nusu kama sikosei kwa hali hiyo mpaka nikasema kumbe nilifanya kosa kumwambia siku ya kwanza nitakununulia chakula.
Ila nikajipa moyo kuwa mbona nyumbani nina watu wengi na sio watoto wangu ila wanakula na kushiba na wala sijafirisika, ngoja tuende hivyo hivyo pia muda wangu wa kukaa pale kazi ikuwa unaisha narudi kofisi za mwanzo ko isinipe tabu.
Kuna siku tukiwa tunafanya kazi moja nikaamua kumueleza jinsi wafanyakazi wenzake wanavyomsema kuhusu kuwanyanyasa na kutokuwa na ushirikiano katika mambo ya kijamii, alishtuka kiasi akasema kwa mshangao, "kumbe!''
Akawa kama mtu aliye changanyikiwa akaongeza sauti ya juu kuwa achana na wale hawana elimu niwajinga tu na hawanisaidii chochote.
Nikamwambia hapana kuna umuhimu wa kukaa vizuri na jamii maana unaweza ukapatwa na tatizo ikashindikana kusaidiwa, nikampa mfano itokee mtoto wako au mke wako amepungukiwa damu na wafanya kazi wenzako wakagoma kujitolea utajisikiaje?
Hapo akatulia kwa muda bila kuongea na mimi nikajifanya nipo busy na simu yangu.
Baada ya dakika kama tano hivi akanimbia wewe kweli ni rafiki mzuri umeongea jambo jema huku akionekana ubongo wake kama ame RESTORE TO FACTORY SETTINGS.
Akaniamia ngoja nikuambie rafiki, sio kuwa sipendi kushirikiana na wenzangu ila saivi sina pesa angalia hata uvaaji wangu sio ule ulionizoea.
Hapo nikashtuka tena huyu mtu anaongelea nini wakati mshahara wake umenizidi kama 500k kutokana na madaraka aliyonayo pia ana allowance nyingi kuzidi mimi? Ikabidi nicheke na kusema acha utani ndugu.
Akanza kujifikicha macho kama mtu anayejifuta machozi na sauti ikabadilika kuwa ya upole na kuanza kuniambia kuwa yeye hana madaraka na mshahara wake wala posho zake bali mke wake ambaye ni mama wa nyumbani yeye ndo ENGINEER wa mambo yote.
Akaendelea kusema kuwa yeye ana pewa elfu 45 tu kama nauli ya usafiri, na anaambiwa kuwa chakula akale home tu, akifika huwa ananushwa kama amekula huko nje na ikigundulika hapewi chakula siku hiyo nzima.
Pia akaniambia ndo maana kila akila nje lazima apige mswaki ili mke wake asijue maana hata akila muhindi tu ni shida. Na wakati mwingine huwa anatembea kwa mguu umbali wa lisaa na nusu akikosa nauli.
Nikampa mpole huku nikishangaa maisha anayopitia mtu anaye pata mshara wa 3M.
Nikamuliza una nyumba ngapi maana gari nilijua hana, kwa Ubahili huo na muda alio fanya kazi ni mrefu maana aliajiriwa akiwa na diploma ila alijiendeleza akiwa kazini.
Akanijibu bado amepanga ila gari alimnunulia mke wake na hairuhusiwi yeye kulitumia kwa shughuli yoyote ile labda mke wake ndo ampeleke na gari.
Akaniambia kuwa akifika nyumbani huwa hana amani pia anamuogopa mke wake kama yupo na simba nyumba moja, ndo maana huwa anachelewa kutoka kazini.
Nikamuliza unaishi vipi na mtu unaye muogopa? Akasema akiwa huku nje huwa hogopi na unakuta anapanga akilini mwake kuwa nikifika home nitaenda kufanya mapinduzi na kumfukuza mwanamke ila akifika tu home anakuwa mnyonge ila anakuwa na uelewa wa kwake kabisa ila anamuona mke wake kama simba.
Pia yeye akaniuliza sijui nifanyaje, ingawa siku hizi uwoga umeanza kupungua kiasi chake na anaweza kubishana naye ila kwa uwoga sio kama mwanzo ambapo kila kitu ni kuitikia kwa kichwa maana alikuwa anaogopa kutoa sauti asije pigwa na mke wake.
Tuliongea mengi na mwishowe nikabaki kuumpa pole tu nilishindwa kumpa ushauri wowote, na muda wangu wa kukaa hapa umekaribia kumalizika.
Sikuamini niliyo ambiwa ila kweli kuna watu wanapitia magumu katika ndoa. Muombe Mungu yasije kukukuta ya kupewa 45k out of 3m kwa mwezi.
Yaani nimecheza humo humo tena karibu sana. Babu yangu mdogo alioa shangazi wa bamkwe so undugu wa kujiamini.nakula chakula najua siwezi kula na kinyama kimekaa kwa k kwa 7days.Ushauri wangu Ni huu
1. Oa rafiki yako
2. Oa kutoka the same background
3. Oa mtu wa kwenu
4. Mkeo asikuzidi kipato
5. Epuka kuoa makabila usiyojua Mila na desturi zao. Wachaga wananielewa kwa hili
Mkuu mie nakazia sijui kwa almasi kabisa.Nakazia
Keep left the
Huyo rafiki yako yuko mkao gani? Maombi yanasaidia sana ila kwa vile ameteswa kwa muda, atakuwa anabisha kwa vile hajafunguliwa kutoka katika mifungo hivyo vya kishirikina.Dah,msaidie ndugu yako aseee,amefungwa hata kama kuna kupangiana mshahara si kwa staili hyo inamaana,labda tuseme labda kuna siri anamtunzia maana mambo ya family huwez jua lakini hata kama ni hivo basi hamna faida huo ni ukatili,asa kama ni hyo hela tu anapata vipi kuhusu ndugu zake
n..!
Angenitembelea mimi, siku ya pili hiyo ndoa ingekufa kifo kibaya. Ndo madhara ya wataalam.Kusema ukweli sina uzoefu wowote na hao watu unao waita wataalamu, ila mpango wangu ni kumpeleka akaombewe, kama atakubali
Kafungwa huyo hakuna mwanaume yeyote mwenye hela au mshahara wa m 3 akamwogopa mke wake never...Ndo maana mimi sitaoa Forever ushenzi gani huu tunafanyiwa na Madem.
Hapa kwenye kabila nakataaUshauri wangu Ni huu
1. Oa rafiki yako
2. Oa kutoka the same background
3. Oa mtu wa kwenu
4. Mkeo asikuzidi kipato
5. Epuka kuoa makabila usiyojua Mila na desturi zao. Wachaga wananielewa kwa hili
Hapa kwenye kabila nakataa
Chezea limbwata la kijijini weyeeeh, hadi tumbo la uzazi wa mama yake linatikisika. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kweli limbwata lipo mpe pole rafiki yako
Ila huyo mkewe kiboko
Maombi tena? Wee cc hauko serious sasa.Rafiki yako anahitaji kufunguliwa ..mpeleke kwenye maombi
Acha kabisa watu na vipaji vyaoChezea limbwata la kijijini weyeeeh, hadi tumbo la uzazi wa mama yake linatikisika. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]