Kuna ile hadithi fupi ya mchina na ununuzi wa mbwa kwa wanakijiji.
Kwakuwa wachina inaaminika ni walaji wazuri wa mbwa,aliaminika kama muwekezaji kweli anakusanya mbwa kwa ajili ya kusafirisha kwenda kwao china.
Akatangaza kwa wanakijiji ananunua mbwa kwa 25000 kila mmoja,watu wakatafuta sana mbwa,walipoanza kuadimika huku wote akiwakusanya akapandisha bei mpaka 50000,watu wakaenda mpaka vijiji jirani kutafuta mbwa,wakawaleta.akawapa hiyo hela.aliposikia kwamba mbwa wameadimika mpaka vijiji jirani,hapa ndipo wanakijiji walipigwa sasa.
Aliondoka na kwenda kijiji cha mbali kabisa wasikomfahamu akaweka mawakala wake kisha akawakabidhi wale mbwa,kisha akarudi kijijini na kutangaza"sasa ananunua kila mbwa mmoja laki mbili.lakini kwanza anapeleka waliopo kwao china.wafamye kukusanya mbwa akija ni mwendo wa laki mbili mbli kwa kila [emoji240].
Wanakijiji walizurula kama mbwa kutafuta mbwa[emoji1787][emoji1787][emoji1787].wakafika mpaka kwa mawakala waleeee wa mchina,na kununua wale mbwa kwa mpaka laki sabini 170000,lakini waliporudi kumsubiri mchina,walimsubiri kweli kweli hakutokea.
NOTE:hizi biashara za aina hiyo,sarafu,mercury,birika,.ni kweli zipo.
Ila wajanja wachache wenye akili nyingi wametumia fulsa,mpaka kuweka na wanamazingaombwe huko kucheza na akili za mteja,ila matokeo yake siku zote huwa ni hasi kiuchumi.