Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI


Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.

Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.

Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro[emoji2955][emoji2955][emoji2955].

Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.

Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.

Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.

Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.

Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91].
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.

Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.

Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.

Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.

Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.

Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.

Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.
Daaah, jamaa akaenda kusema ulikuwa unabakwa. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.


Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Hahahahhahaha ngwiii ng'wiiiiii..Nishakujua..nikuulize kitu?? wewe jina lako halisi linaanzia na herufi G.. bishaa!
 
Nilibebeshwa mavi mkononi kwa sababu ya upole


Mimi ni mpole ila nilivyokuwa mdogo nilikua mpole kupitiliza ndo maana nilibebeshwa mavi ambayo sikunya mimi.


Kipindi nipo darasa la kwanza nilipelekwa boarding sasa hiyo siku tuko zetu tunacheza mida ya jioni akaja matron akatuita boys wote tulikua kama 30 hivi ambao tunakaa bweni na tulivyokusanyika akatuambia nifuateni tukaona anaelekea chooni basi tukamfwata tulivofika chooni ile sehemu ambayo ipo special kwa ajili ya haja ndogo tukakuta mavi yapo makimba matatu yamejipanga matron akauliza nani kanya hapa ina maana vyoo hamvioni mpaka mtumie sehemu ya haja ndogo nitajieni aliyekunya hapa.


Wote tulikua kimya mara ghafla kuna dogo mmoja mmasai anaitwa Lomnyaki akayasogelea yale mavi akayaangalia afu akanitaja akasema matron huyu Mafian cartel haya mavi yake kabisa yeye ndo kanya hapa mavi yake nayajua dah nilishangaa sana kumsikia Lomnyaki akinisingizia kosa ambalo sikufanya sijui alikua ana malengo gani kunichoma kwa matron


Basi Matron hakutaka maelezo akawaruhusu wenzangu waondoke akabaki na Mimi na kunihoji kwa nini nimekunya sehem ambayo siyo sahihi basi na Mimi na upole wangu ambao ulikua uboya nikawa nalia tu kwa kuonewa matron akasema wewe lia ila haya mavi uyazoe ukatumbukize Kwenye tundu la choo nikirudi nisikute mavi hapa afu akaondoka


Dah sasa nikabaki pale nahuzunika moyoni namlaumu Lomnyaki kwa kunichoma,basi nikachukua toilet paper nikaanza kuokota kimba moja napeleka kudumbukiza Kwenye tundu la choo nikachukua tena lingine hadi nikamaliza kuzoa makimba yote matatu kisha nikanawa na kumwambia matron nishamaliza kuzoa makimba yale.akasema sawa nenda ila usirudie tena.


watu walinicheka sana na kunitania pale shule mpaka Leo natafakari kwanini Lomnyaki alinichoma wakati mimi sihusiki labda yeye ndo aliyekunya n kuamua kuniuzia kesi

Mataccor yako Lomnyaki
Sitakaa nimpeleke boarding mwanangu mdogo maana uonevu wa kule hapana

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Nimeishia comment ya 132 ya Demi, ngoja nitoe juto langu badae Tena niwarudie.

Nlikuwa na urafiki na jamaa mmoja kutoka Mwanza kwa jina la Emmanuel, Alikuwa mbele darasa Moja lakini tulikuwa maswahiba.

Jamaa alikuwa mcheshi na mtu wa kunichangamkiaa mara tunapoonana, salamu za kisela kama TMK family.

Kama mnavojua urafiki wa chuo mara nyingi unaisha au kupungua mkimaliza chuo.
Basi jamaa mawasiliano yetu yakawa hafifu, na nikubal kuwa jamaa ndiye aliyekuwa akinitafuta mara nyingi.

Tukapotezeana kwa muda takriban mwaka hivi, SIKU JAMAA YANGU ANANIAMBIA YULE RAFIKI YAKO ALIFARIKI kwa matatizo ya Uti wa mgongo.

Nliumia sana nikakumbuka kuna muda we have to swallow our prides ,TAFUTENI RAFIKI ZENU MUWAJULIE HALI HUWEZI JUA NINI KINAMFANYA ASIKUTAFUTE pengine ashafariki we unakaa kusema Hadi ye anitafute.

MAJUTO NI MABAYA SANA.

Good night
 
Nimeishia comment ya 132 ya Demi, ngoja nitoe juto langu badae Tena niwarudie.

Nlikuwa na urafiki na jamaa mmoja kutoka Mwanza kwa jina la Emmanuel, Alikuwa mbele darasa Moja lakini tulikuwa maswahiba.

Jamaa alikuwa mcheshi na mtu wa kunichangamkiaa mara tunapoonana.

Kama mnavojua urafiki wa chuo mara nyingi unaisha au kupungua mkimaliza chuo.
Basi jamaa mawasiliano yetu yakawa hafifu, na nikubal kuwa jamaa ndiye aliyekuwa akinitafuta mara nyingi.

Tukapotezeana kwa muda takriban mwaka hivi, SIKU JAMAA YANGU ANANIAMBIA YULE RAFIKI YAKO ALIFARIKI kwa matatizo ya Uti wa mgongo.

Nliumia sana nikakumbuka muda we have to swallow our prides ,TAFUTENI RAFIKI ZENU MUWAJULIE HALI HUWEZI JUA NINI KINAMFANYA ASIKUTAFUTE pengine ashafariki we unakaa kusema Hadi ye anitafute.

Good night
Uko sahihi, pole.
 
Another One!

Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.

Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani wa Computer [Sitasema ni System gani].

Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu ya namna ambavyo mfumo uliwarahisishia kazi.

Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.

Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!

Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.

Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao kimya kimya na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!

Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee

Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh

Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.

Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.


Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favor tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.


Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.

Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!


Na hilo likawa funzo langu!
haha hili tukio mbona kama lakwangu tu but nchi ndio tofauti haha, dah kazi kweli kweli, pia najutia sababu nilipoteza kazi nayoipenda sana na ya pesa nzuri kwa tamaa za kijinga.

Sent from my vivo X6D using JamiiForums mobile app
 
Wenzio sisi tumekuwa ma MAJOR wewe umetolewa utoro
I'm happy for you Kamanda na pia hongera sana kwa kufika hizo level.

Naamini pia kilichokufikisha hapo ni uvumilivu. Na binadamu huwa tunavumilia vitu tunavyovipenda.

Nikijiona nashindwa kabisa kuvumilia vitu fulani kwenye maisha yangu, basi najua hivyo vitu havipo kwa ajili yangu, na bila kupoteza muda nina-achana navyo very quick. Kwa sababu in the long run, vitakuja kunigharimu zaidi.

Sijawahi kujutia ku.quit Jeshi ila nina appreciate sana watu wake. Waliokubali ku give up uhuru wao wa maisha ya kawaida kwa ajili ya maslai mapana ya Nchi yao. Kongole sana kwenu maana kazi za watu sio lelemama!
 
Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,

Wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa ww n km sister tu bhanaa ,

Weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA ,,,baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kbs
Peleka kwenye uzi wa kuliwa kimasihara[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom