VISA NI VINGI,ILA ACHA NIANZE NA HIKI...
Ni 2010's niko form 4 shule ya kata hiyo mkoani Iringa huko. Nilikua mtoro sana,yani nikisema mtoro ni mtoro kweli. Kwa week naweza kuhudhulia shule mara mbili tu,siku nyingine zote nashinda Samora pale katika maroli ya mchanga,mawe fofali,n.k tunasubiri kazi za upakiaji. Au nakua Isakalilo nachimba zangu mchanga au mawe.
Licha ya mahudhulio yangu kuwa mabaya,ila walimu wengi wa ile shule walikua wananijua,haswa Headmaster. Huyu alinijua kwasababu alinisaidia sana kipindi naingia pale form 1.(Hili nilieleza katika ule uzi wa "Msoto")
Tatizo lilianzia hapa.Siku moja bila hata kutarajia alikuja ndugu yangu mmoja wa karibu kabisa akanichafua sana pale shule,wakati huo nimewekwa mtu kati ofisi za Walimu. Yani aliongea mambo mengi sana,kutokana nae ni mtu mzima na ana mwonekano wa busara busara! Basi walimuamini 100%.
Alisema mimi mhuni(Kibaka),MLEVI sana na nakunywa Ulanzi sanaaa! Nashinda na wahuni, sina nidhamu hata kidogo,n.k,n.k. Wakati huo kumbuka sijawahi kuishi nae tangu namaliza standard 7 huko,nikitelekezwa nikawa naishi tu kama mtoto wa mtaani. Nilikua Chokoraa ambae shule niliipenda ila nilikua nashindwa nijigawe vipi,huku nihudhurie shule au nitafute hela ya kula.
Basi ndugu zangu tuendelee, Headmaster na wale maticha hawakutaka hata kunipa nafasi nijitetee, na hata wangenipa nafasi ya kujitetea sidhani kama ningeweza,nilikua nacheka cheka tu kwa hasira. (Mimi nikikasirika sana huwa natabasamu sana na kakicheko kwa mbaliii).
Kama unavyojua shule zetu za kata,mimi nikadhani yanaishia pale,ajabu yule ndugu yangu akaamuru nichapwe viboko hadharani. Ikagongwa kengere pale,wanafunzi wakakusanyika pale,nikachafuliwa sana pale assemble,daah yani chafuliwa sanaaaa! Muda huo mimi hasira zimejaa level yake ila tabasamu limejaa usoni halikauki,ndio nilivyo.
Kama unavyojua wanafunzi, mashtaka yalikua kibao,ila points za msingi walizochukua ni "Mimi Kibaka" na "Mlevi,nakunywa sana Ulanzi".
Daah wakawa wananitania sana kila nikienda shule katika zile siku mbili zangu za week, nikawa nahisi karaha,basi nikapunguza mahudhulio kutoka siku mbili mpaka siku moja kwa week au siendi kabisa.
Basi kuna siku nikaenda shule ni kipindi tunakaribia kufanya mtihani wa Mock, Headmaster akaniita Ofisini. To be honest sijawahi kwenda shule nikiwa na "Majagi" kichwani,ila siku hiyo nilikua Majagi haswaa,ila nimekula majani ya mti wa limao ili kuzuia harufu. Daah kufika ofisi ya Headmaster si akaanza kunikumbushia yale ya siku zile,akawa kama ananisimanga na ule msaada ambao alinipa kipindi naanza form 1.
Siwafichi uvumilivu ulinishinda,nikawa natetemeka kwa hasira yule mzee yuko mbele yangu kakaa anaendelea kutema shombo zake. Nikagonga meza kwa hasira "Kaa kimya wewe mzee",...aah mzee akajaa upepo baada ya kuona kama namchimba mkwara,si akasimama tukawa tunatazamana ila yeye yuko upande wa pili wa meza.
Aisee! Nilimpa ndonga (Kichwa) moja matata sana mpaka akajikuta kakaa chini bila kutarajia,alafu kimyaa!. Nikajua nimeua wakuu,ila nikavaa roho ngumu nikatoka mle ndani kama hakuna kitu kimetokea,nikatimkia mtaani.
KITU NAJUTIA
Ni kumpiga kichwa mtu ambae anakaribiana na babu yangu. Yani najuta sana.