Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

ahh… jmn coment km hizi mi huwa zinanipa wasiwasi

kwani tunashida gani sisi wake wa ndoa??? si mtuambie basi pengine tutajirekebisha

why wanaojuta kuoa ni wengi sana
Muda mwingine kuoa ninkama kuchukua mkopo benki na kusema ngoja nitunze hela ntapata cha kufanyia..
Utafurahia mwanzoni ila kama hukujipanga na makato na mipango mizuri utaishia kulia.
 
VISA NI VINGI,ILA ACHA NIANZE NA HIKI...

Ni 2010's niko form 4 shule ya kata hiyo mkoani Iringa huko. Nilikua mtoro sana,yani nikisema mtoro ni mtoro kweli. Kwa week naweza kuhudhulia shule mara mbili tu,siku nyingine zote nashinda Samora pale katika maroli ya mchanga,mawe fofali,n.k tunasubiri kazi za upakiaji. Au nakua Isakalilo nachimba zangu mchanga au mawe.

Licha ya mahudhulio yangu kuwa mabaya,ila walimu wengi wa ile shule walikua wananijua,haswa Headmaster. Huyu alinijua kwasababu alinisaidia sana kipindi naingia pale form 1.(Hili nilieleza katika ule uzi wa "Msoto")

Tatizo lilianzia hapa.Siku moja bila hata kutarajia alikuja ndugu yangu mmoja wa karibu kabisa akanichafua sana pale shule,wakati huo nimewekwa mtu kati ofisi za Walimu. Yani aliongea mambo mengi sana,kutokana nae ni mtu mzima na ana mwonekano wa busara busara! Basi walimuamini 100%.

Alisema mimi mhuni(Kibaka),MLEVI sana na nakunywa Ulanzi sanaaa! Nashinda na wahuni, sina nidhamu hata kidogo,n.k,n.k. Wakati huo kumbuka sijawahi kuishi nae tangu namaliza standard 7 huko,nikitelekezwa nikawa naishi tu kama mtoto wa mtaani. Nilikua Chokoraa ambae shule niliipenda ila nilikua nashindwa nijigawe vipi,huku nihudhurie shule au nitafute hela ya kula.

Basi ndugu zangu tuendelee, Headmaster na wale maticha hawakutaka hata kunipa nafasi nijitetee, na hata wangenipa nafasi ya kujitetea sidhani kama ningeweza,nilikua nacheka cheka tu kwa hasira. (Mimi nikikasirika sana huwa natabasamu sana na kakicheko kwa mbaliii).

Kama unavyojua shule zetu za kata,mimi nikadhani yanaishia pale,ajabu yule ndugu yangu akaamuru nichapwe viboko hadharani. Ikagongwa kengere pale,wanafunzi wakakusanyika pale,nikachafuliwa sana pale assemble,daah yani chafuliwa sanaaaa! Muda huo mimi hasira zimejaa level yake ila tabasamu limejaa usoni halikauki,ndio nilivyo.

Kama unavyojua wanafunzi, mashtaka yalikua kibao,ila points za msingi walizochukua ni "Mimi Kibaka" na "Mlevi,nakunywa sana Ulanzi".

Daah wakawa wananitania sana kila nikienda shule katika zile siku mbili zangu za week, nikawa nahisi karaha,basi nikapunguza mahudhulio kutoka siku mbili mpaka siku moja kwa week au siendi kabisa.

Basi kuna siku nikaenda shule ni kipindi tunakaribia kufanya mtihani wa Mock, Headmaster akaniita Ofisini. To be honest sijawahi kwenda shule nikiwa na "Majagi" kichwani,ila siku hiyo nilikua Majagi haswaa,ila nimekula majani ya mti wa limao ili kuzuia harufu. Daah kufika ofisi ya Headmaster si akaanza kunikumbushia yale ya siku zile,akawa kama ananisimanga na ule msaada ambao alinipa kipindi naanza form 1.

Siwafichi uvumilivu ulinishinda,nikawa natetemeka kwa hasira yule mzee yuko mbele yangu kakaa anaendelea kutema shombo zake. Nikagonga meza kwa hasira "Kaa kimya wewe mzee",...aah mzee akajaa upepo baada ya kuona kama namchimba mkwara,si akasimama tukawa tunatazamana ila yeye yuko upande wa pili wa meza.

Aisee! Nilimpa ndonga (Kichwa) moja matata sana mpaka akajikuta kakaa chini bila kutarajia,alafu kimyaa!. Nikajua nimeua wakuu,ila nikavaa roho ngumu nikatoka mle ndani kama hakuna kitu kimetokea,nikatimkia mtaani.

KITU NAJUTIA
Ni kumpiga kichwa mtu ambae anakaribiana na babu yangu. Yani najuta sana.
Powaa tuu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja hivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja.

Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....

I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel naamini asingekutana na yaliyomkuta, ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako.

Kifo ni fumbo kubwa.

Tuwajali Sana wanaotupenda, life is too short.
Malizia tujifunze...please
 
Aise nikimkumbuka yule mwanamke naishia kujuta kwa nini nilimgegeda siku ile....ndio safari yangu ya arv ilipoanza[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54][emoji54]
 
Nima visa vyangu vilivyowahi kunitokea maishani nikiviweka hapa mnaweza kudhani mimi ni fiction/animation character
Wacha nile kaya kwanza nije kushusha stanzas
karibu stejini hata Yesu kuna watu walimkataa
kikubwa ni kuachana nao tu
tunasubiri story yako
 
And Another!

Katika harakati za kutafuta Ugali nilijikuta nimeomba kujiunga na jeshi la JKT. Nikatupiwa Kigoma, kule Bulombora 821KJ.

Nikapigishwa jaramba na kulishwa vumbi huku nikitazama ziwa Tanganyika kwa ukaribu kabisa lililozungukwa na mawese ya kutosha. Ruka Juu, Kanyaga Chini kwa nguvu mpaka mguu utoke nje ya kiatu.


Mikesha ilivyozidi nikaona hapa nitakufa. Nikaanza harakati za kutafuta nafasi ya kulala vizuri maana zile Dakika 5 unazopewa za kulala hazitoshi kabisa. Nikaanza kutafuta machimbo. Wenzangu wakienda mkesha, mimi najipeleka porini. Siku nyingine nakutana na ma afande na wao wamedoji kwenda lindo wananitimua najikuta nimerudi kulala uvunguni.

Tabia yangu ya kujizoesha kulala ikaanza kunigharimu. Ikafika mahali nikawa siwezi kabisa kwenda kukesha hata siku moja. Nikaanza kuona hadi uvivu wa kwenda kulala mbali na anga letu. Nakumbuka nilikua Eagle Coy.

Siku hiyo nimelala uvunguni nakoroma kabisa, saa ngapi afande asiingie ndani kutafuta watoro. Si akaniskia navyokoroma kule chini ya kitanda. Dah sitasahau hiyo kipigo niliyopewa. Nakumbuka al manusura nipoteze jicho. Maana vile vitanda vimechomelewa kwaiyo kuna kama vichuma flani hivi kama nondo vimejitokeza kwa juu, alinibamiza kichwa kwenye kile kitanda ile nondo ikachubua kidogo pembeni ya jicho.

Sijui nilipata wapi ujasiri nikamsukuma pembeni nikasogeza kioo cha dirisha nikarukia nje nikaanza kukimbia huku nachechemea machozi yananitoka ya kutosha. Jamaa nadhani aliniangalia navyokimbia kwa tabu akanionea huruma akaamua kuachana na mimi huku akisema "Nitakuua Mbwa Wewe".

Nilivyofika walipo wenzangu kwenye mkesha nikapokelewa tena na adhabu za kubiringita na kukwepa ndege za kivita. Dah.. nilihisi mwisho wangu umefika, nikasema kwa sauti "Nakufa" huku machozi yanatoka ili hata jamaa anionee huruma lakini wapi. Yeye kakazana kunioshea na kunifanya mfano kwa wengine. Saiyo pumzi imekata, maumivu kila mahali, machozi yameshatoka mpaka yamekauka, siwezi kuongea tena. Ni kwa Neema za Allah pekee nilifanikiwa kuona tena Jua siku iliyofuata maana nilikua nahisi kabisa nakufa. Hali yangu ilikua mbaya sana!

Sikuwahi kujuta kwenye maisha yangu kama hiyo siku. Nililaani uamuzi wangu wa kwenda huko. Kile kitu kilinikaa sana moyoni kwa muda mrefu. Niliona kabisa huku sio kwangu. Course ilivyoisha, wakati wengine wanasikilizia kwenda JWTZ na Polisi, mimi nikaandaa nauli yangu, nikavizia ule muda tunaotumwa kwenda town...nikatorokea huko mazima na nikaapa sitarudi tena. Ikawa imeisha hiyo!

Kwa kweli mambo ya Jeshi yana watu wake. I was not one of them!
Wenzio sisi tumekuwa ma MAJOR wewe umetolewa utoro
 
Back
Top Bottom