Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nakumbuka A-level mi na mwanangu cayafas tulikuwa hatupigi msuli na kuingia darasani ilikuwa kwa makando makando
Muda wetu mwingi tulikuwa bwenini tunapiga stori, kucheza draft nk, sometimes tulikuwa tunashinda kijijini.

Ilifika time mwalimu wa darasa alinikana kuwa mimi sio mwanafunzi wake maana hajawahi kuniona darasani.
Bas bwana kutokana kutoingia class perfomance ikawa siyo ya kuridhisha.

Kuepuka hilo me na kayafa tukasema kama vip hatutakuwa tunafanya mitihani, bas tukaadhimu mioyoni mwetu kuwa hatutakuwa tunafanya mitihani na huo mswada ukapitiswa.

PAUKWA PAKAWA hatukufanya baadhi mitihani kadhaa huku tukisingizia kuwa tumefanya na tumekusanya hivyo tunahitaji matokeo yetu. Issue ilikuja sanuka kuwa hatufanyi mitihani baada ya kukwepa test paper kadhaa za ticha mmoja, nae akamua kuwa anatubana tukawa tunafanya kishingo upande.

Basi siku moja huyo ticha akatangaza kuwa atatunga mtihani ila kila mwanafunzi anayetaka kufanya atatoa buku.
Me na kayafa tukajisemea "tayari huu umetupita", sio kwamba hatukuwa na pesa ila kukwepa paper maana kuna mishe tulikuwa tunazifanya pale school zinatupatia pesa za kuishi ki doni.

Siku ya paper me na mwanangu pamoja na wengine ambao hawakujisikia kutoa buku tukawa tuko huko bwenini tunapiga stori Ticha kaingia kugawa paper haoni watu kadhaa kuuliza akaambiwa ni watu ambao hawakutoa pesa.

Ticha akasema poa ila "The asker na cayafas" hawa watafanya huu mtihani bure.
Basi akaamua kutufuata bwenini kutupige paper. Sisi pale ndani tulikuwa tuna kaa kwa machale so wakati anakuja nikamuona nika msitua mwanangu.
Kumbe yule ticha alimstua ticha mwengine waje kutuvamia afu yule ticha mwingine akapita njia ambayo ni blind spot.

Basi pale bwenini kulikuwa na ki store ambacho juu tulitoboa ceiling kwa ajili ya kujificha endapo tuta vamiwa na vikosi vya urusi. Mim nikachumpa nikazama kwenye dari,cayafa akaamua kukimbilia uhamishoni( vichakani) coz bweni lilikuwa karibu na vichaka MAKOSAA

Yule ticha aliyekuwa blind spot akamnoki jamaa yetu akaanza kumuita "we cayafas unakwenda wap embu twende ukafanye mtihani" kayafa hakutaka kugeuka akaendelea kutokomea, mwalimu akasema tena "we kayafa nimekuona embu njoo hapa ukafanye mtihani" lakini kayafa asisikie.

Wakati huo mm nipo darini nawasikiliza nkatamani kucheka ila nkajizuia maana pia ningetoa siri juu la lile handaki.
Basi walimu wakatoa maneno yao pale ya ghadhabu na uchuro kisha wakaondoka.

Basi wakati wa chakula ukafika tukaenda kuchukua chakula hakukuwa na ticha na mtihani ushafanyika so amani amani.
Akatumwa Headboy akaja kutuambia tunaitwa na headmaster. Hapo hata hatujagusa msosi.

Tukaenda mpaka ofisi ya walimu tukawakuta wamejaa full maana walikuwa wanakula pamoja pale ofisini.
Basi tukasomewa mashitaka tukajitetea hatukuwa na pesa, walimu wengine wakachangia tabia zetu mbovu kama za mademu, kutohudhuria parade, class na kulala bwenini.

Basi ikaamuriwa tutafanya mtihani pale ofisini mbele yao na tukitoroka siku nyingne tutafanyia paredi mbele ya halaiki ya wanafunzi,
Tukapewa mtihani kisha wao wakapakua wali nyama na kuanza kula huku sisi tukiteseka na maswali ya physical geography. Nakumbuka ubwabwa ulikuwa unanukia sana na wakati huo sisi hatujala hivyo akili ikawa inawaza chakula kuliko contour za map.

Baada ya kumaliza paper tukakusanya tukarudi kukaa wakatuambia mnaweza kwenda, sisi tukasema huko chakula kimeisha na sisi tuna njaa tukiwa tunalenga ule ubwabwa, maana msosi wa skuli ulikuwa ugali na mchuzi wa wadudu wale weusi wa kwenye maharage maana walikuwa wengi kuliko maharage yenyewe.

Basi tukatia ngumu pale maana tuliona ubwabwa umebaki, headmaster akaamua kutupatia ule ubwabwa tukala kisha tukatokomea kama washindi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaa mnooo yaan khaaaah
 
Hahahahaahahah
 
Dah inauma mbaya
 
[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We mwana pamoja na Cayafas hamuendi mhinguni
 
Kupona na miwaya ni kumshukuru Mungu tu, kuna wahuni kibao hawapati, mwana mara moja tu kaungwa
 
Nilifaulu A Level moja ya shule bora Mkoani kilimanjaro, Kipindi hicho ndo nipo maskani nafanya maandalizi ya kununua baadhi ya vitu ili niweze kusafiri siku inayofuata, Nakumbuka nilikuwa nimepiga mishe mishe nyingi sana kitaa tangu nilivyomaliza form 4 nikajichanga kununua simu ya elfu 40 ya button , kipindi hicho ni simu nzuri sana yenye display ya visamaki vikiwa vinatambaa, pia nikanunua baadhi ya vitu vya muhimu vya shule kama sabuni, viatu, sare nk. na hela ikawa imeshakata, nikabaki na hela ya ada nikaamua kuiweka kwenye simu ili nikifika Moshi niweze kuitoa nikalipie shuleni.

Sikuwahi kufika Moshi kabla, na Mzee hakunipeleka kwani alikuwa anasumbuliwa sana na miguu kipindi hicho, Ikabidi nikomae mwenyewe nianze safari, bahati nzuri nikawa nimepata connection ya mawasiliano na bro mmoja aliyemaliza shule kabla yetu hivyo alipangiwa shule ninayoenda mimi , yeye alikuwa form 6. Akaanza kunielekeza baadhi ya vitu na kipi nifanye nikifika moshi. Haya Safari ikaanza, nilikuwa natokea Dodoma, Kipindi hicho unapitia kwanza Singida kabla ya kujengwa hii barabara ya shortcut ya babati. Safari imeanza vizuri tu tukafika Singida fresh, tukapiga tea dakika 10 tukaingia tena kwenye basi hadi babati, nafika babati tukaambiwa tuna dakika 10 za kula msosi, Nimekula fresh nikaingia kwenye basi nikae, kujisachi sion simu, nikakumbuka niliiweka mfuko wa shati, akili ikanijia na nikajua hapa nimeshapigwa. Kumwambia konda sioni simu akazidi kukazia ,dogo hapa ushaibiwa, Sio sehemu nzuri sana, pole sana...Daaah nikakumbuka laini ilikuwa ni mpya na namba sikuikariri, na nilishaweka hela ya ada, kichwa kikaanza kuniuma. Isitoshe namba ya yule jamaa nikawa nimeipoteza na sikuwa nimeikariri. Nilisafiri kwa mawazo sana siku ile. Nikafika Moshi usika kama saa 2 hivi, mfukoni nina elfu 4, nikaulizia magari yanayoenda shuleni, nikaambiwa huwa yanaenda mwisho saa 2 usiku kwahiyo nilishachelewa, ni nje ya mji kidogo. Dah, ikabidi niombe hifadhi kwenye basi nilale ili kesho niondoke, hapo nishaazima simu sana kumpigia mzee tangu mchana simu yake haipatikani, nikawa chakula cha mbu usiku ule.
Asubuhi nikaelekezwa magari ya shuleni na nikafanikiwa kufika shuleni kwa kulia sana na konda maana nauli ilipelea, sasa shuleni walimu wakawa wanagoma kunipokea sina ada sina godoro, kila napojaribu kuwaelezea mkasa ulionikuta wakawa wanahisi ninatunga, baada ya kuhangaika nao sana wakaniruhusu. Nakumbuka niliishi maisha magumu sana, mahitaji mengi yaliisha mixer madeni ya shuleni nikawa sina amani kabisa. Likizo time sikutaka kwenda home kabisa nilikosa hata nauli, tukabaki mimi na wenzangu (hasa wanafunzi waliokuwa wakiishi mikoa ya mbali kama kigoma na mwanza,) tukawa tunamsaidia mwalimu wa economics kulima shamba lake na kupanda, namshukuru sana likizo yote tulitumia shambani, alikuwa anatulipa vizuri sana na alikuwa mkarimu sana yule mwalimu (RIP), tulivyofungua Shule shida zote zikawa zimeisha nikafanikiwa kupunguza madeni na pia ile hela iliyokuwa kwenye laini voda waliirudisha kwani nilienda kurenew laini, kuna bro yule wa shulen alikuwa na namba yangu, hivyo kurenew ikawa simple sana, nikawa don sasa shulen hadi wanafunzi wakashangaa.
Ila nilijutia sana kuipoteza simu yangu, niliitumia siku moja tu, na niliitafuta kwa hela ya jasho langu😞
We mwizi uliyeniibia simu babati kama upo humu Mataccor yako

YNWA
 
Mim mpaka leo najuta kuwahadithia washkaj zangu namna nilivyomla jimama la miaka 45+.

Yaan mpaka leo wakimuona lazima wanizingue halaf jimama lenyewe halivungi likiniona na washkaj lazima lije[emoji51][emoji51]
[emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka sana aisee
 
Sasa hapa unajutia nini mkuu?

Kumbe ndio maana ulikua unakimbia mitihani.

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Na wewe hapa unajutia nini sasa?
Mashabiki wa Liverpool mkoje lakini?
 
Pole sana Mkuu. Ila kwenye maisha hayahaya tuliyonayo, bila unyonyaji, cheating, wizi, kurefusha mkono n.k kufanikiwa ni kugumu mno. Cha msingi ukizipata hata kama ni za wizi ziwekeze vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…