The asker
Member
- Oct 14, 2014
- 31
- 87
Nakumbuka A-level mi na mwanangu cayafas tulikuwa hatupigi msuli na kuingia darasani ilikuwa kwa makando makando
Muda wetu mwingi tulikuwa bwenini tunapiga stori, kucheza draft nk, sometimes tulikuwa tunashinda kijijini.
Ilifika time mwalimu wa darasa alinikana kuwa mimi sio mwanafunzi wake maana hajawahi kuniona darasani.
Bas bwana kutokana kutoingia class perfomance ikawa siyo ya kuridhisha.
Kuepuka hilo me na kayafa tukasema kama vip hatutakuwa tunafanya mitihani, bas tukaadhimu mioyoni mwetu kuwa hatutakuwa tunafanya mitihani na huo mswada ukapitiswa.
PAUKWA PAKAWA hatukufanya baadhi mitihani kadhaa huku tukisingizia kuwa tumefanya na tumekusanya hivyo tunahitaji matokeo yetu. Issue ilikuja sanuka kuwa hatufanyi mitihani baada ya kukwepa test paper kadhaa za ticha mmoja, nae akamua kuwa anatubana tukawa tunafanya kishingo upande.
Basi siku moja huyo ticha akatangaza kuwa atatunga mtihani ila kila mwanafunzi anayetaka kufanya atatoa buku.
Me na kayafa tukajisemea "tayari huu umetupita", sio kwamba hatukuwa na pesa ila kukwepa paper maana kuna mishe tulikuwa tunazifanya pale school zinatupatia pesa za kuishi ki doni.
Siku ya paper me na mwanangu pamoja na wengine ambao hawakujisikia kutoa buku tukawa tuko huko bwenini tunapiga stori Ticha kaingia kugawa paper haoni watu kadhaa kuuliza akaambiwa ni watu ambao hawakutoa pesa.
Ticha akasema poa ila "The asker na cayafas" hawa watafanya huu mtihani bure.
Basi akaamua kutufuata bwenini kutupige paper. Sisi pale ndani tulikuwa tuna kaa kwa machale so wakati anakuja nikamuona nika msitua mwanangu.
Kumbe yule ticha alimstua ticha mwengine waje kutuvamia afu yule ticha mwingine akapita njia ambayo ni blind spot.
Basi pale bwenini kulikuwa na ki store ambacho juu tulitoboa ceiling kwa ajili ya kujificha endapo tuta vamiwa na vikosi vya urusi. Mim nikachumpa nikazama kwenye dari,cayafa akaamua kukimbilia uhamishoni( vichakani) coz bweni lilikuwa karibu na vichaka MAKOSAA
Yule ticha aliyekuwa blind spot akamnoki jamaa yetu akaanza kumuita "we cayafas unakwenda wap embu twende ukafanye mtihani" kayafa hakutaka kugeuka akaendelea kutokomea, mwalimu akasema tena "we kayafa nimekuona embu njoo hapa ukafanye mtihani" lakini kayafa asisikie.
Wakati huo mm nipo darini nawasikiliza nkatamani kucheka ila nkajizuia maana pia ningetoa siri juu la lile handaki.
Basi walimu wakatoa maneno yao pale ya ghadhabu na uchuro kisha wakaondoka.
Basi wakati wa chakula ukafika tukaenda kuchukua chakula hakukuwa na ticha na mtihani ushafanyika so amani amani.
Akatumwa Headboy akaja kutuambia tunaitwa na headmaster. Hapo hata hatujagusa msosi.
Tukaenda mpaka ofisi ya walimu tukawakuta wamejaa full maana walikuwa wanakula pamoja pale ofisini.
Basi tukasomewa mashitaka tukajitetea hatukuwa na pesa, walimu wengine wakachangia tabia zetu mbovu kama za mademu, kutohudhuria parade, class na kulala bwenini.
Basi ikaamuriwa tutafanya mtihani pale ofisini mbele yao na tukitoroka siku nyingne tutafanyia paredi mbele ya halaiki ya wanafunzi,
Tukapewa mtihani kisha wao wakapakua wali nyama na kuanza kula huku sisi tukiteseka na maswali ya physical geography. Nakumbuka ubwabwa ulikuwa unanukia sana na wakati huo sisi hatujala hivyo akili ikawa inawaza chakula kuliko contour za map.
Baada ya kumaliza paper tukakusanya tukarudi kukaa wakatuambia mnaweza kwenda, sisi tukasema huko chakula kimeisha na sisi tuna njaa tukiwa tunalenga ule ubwabwa, maana msosi wa skuli ulikuwa ugali na mchuzi wa wadudu wale weusi wa kwenye maharage maana walikuwa wengi kuliko maharage yenyewe.
Basi tukatia ngumu pale maana tuliona ubwabwa umebaki, headmaster akaamua kutupatia ule ubwabwa tukala kisha tukatokomea kama washindi.