Another One!
Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.
Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani hivi wa Computer [Sitasema ni System gani].
Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu ya namna ambavyo mfumo uliwarahisishia kazi.
Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.
Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!
Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.
Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao kimya kimya na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!
Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee
Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh
Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.
Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.
Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favour tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.
Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.
Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Naona kama mimi ni mtu wa mikosi tu. Kwanini michongo meusi inanipitia mimi tu? Dah nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!
Na hilo likawa funzo langu!