Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Oh this is Sad. Pole Sana Boss kwa hili.

Mungu akutie nguvu kwa kweli!
 
Aisee!!? Unajutia kwa mambo aliyojitakia mwenyewe?
 
Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.

Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.
 
kiukweli kuna mtu najuta mno kumfanya rafiki, sina wa kumsimulia kisa changu maana hii siri nitakufa nayo mwenyewe, lakini najuta mno kumfanya rafiki na sina namna ya kumuacha na kumuweka mbali lakini pia sina namna ya kumkimbia.

Mola wangu wa mbinguni nisamehe mimi siyapendi haya na yananigharimu mno kwenye maisha yangu.
 
Mimi nina juto kuu, ila ntaliandika siku nyingine kwa ID nyingine.

Linanitafuna ndani kwa ndani sometimes
 
Alikupeleka wapi mzee..?
 
NAIROBI

Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.

Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani wa Computer [Sitasema ni System gani].

Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu mfumo uliwasaidia sana kazi zao.

Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.

Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!

Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.

Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach kimya kimya wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!

Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee

Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh

Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.

Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.


Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favor tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.


Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.

Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!


Na hilo likawa funzo langu!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bahati nzuri we misala yako inakupatiaga hela [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…