Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Duuuu
 
Funguka mkuu
Mimi naenda direct najua hata nikitaja shule wengi wamesoma pale, hii ni story ya kwanza.

Nilisoma shule moja inaitwa Shybush au Shinyanga sec, niliingia kidato cha pili msala ukatokea wananzengo wameiba bomba, Hp akakusanya wanafunzi nakwenda sehem inaitwa maganzo ambapo hapohapo na mimi nilikuwa sijui kama wameenda huko maana walikusanyana baadhi wengine tulikuwa hatujui basi sikuiyo namimi nikasema acha niende huko maganzo eeeebwanawee sinikakutana nao alafu huyo Hp alikuwa na misuli balaa si akanilazimisha nijiunge nao.

Basi baada yakujiunga nao na kusaka bomba tukalikosa maana hapo shuleni hatukuoga almost wiki hivi, basi Hp akaanza kupiga sim shule nzima ije ikichafue maganzo maana si unajua wanafunzi walivyo wakorofi? Duh! Hao wanafunzi wakagoma kwenda maganzo aisee Hp alikasirika wakati tunarudi tukaambiwa tuvae kininja tuchume bakora tukawachape waliobaki shuleni [emoji24][emoji24], masikini wengine walikiwa ni walemavu, aisee walichezea kichapo si cha polepole.

Kesho yake ukawa ni msala maana wengine walilazwa, wengine walivunjika vidole vya miguu, tukaitwa parade nakuambiwa tupige kura walioshiriki aisee nilianza kutetemeka huku nikijisemea si nimo kwenye huu msala? Dah! Bahati nzuri sikuwemo aisee niliponea tundu la sindano na walio gundulika wamefanya hivyo walifukuzwa shule aisee.
 
Bahati nzuri we misala yako inakupatiaga hela [emoji23][emoji23][emoji23]
Hela ndio ilikua motivation. Siwezi kuingia kwenye msala kama hakuna Chambi kidogo. Toka nikiwa mdogo kuna Mentality fulani Mother alikua anaijenga kichwani kwangu kila nikifanya kosa..

Mara nyingi alikua ananiambia "Wewe umefanya kitu flani umekamatwa, umechapwa sasa kilikua kinakusaidia nini hata kama usingedakwa?"

Kwaiyo ni kama alikua ananiambia niweke kila tukio kwenye uzani (balance) na faida nayopata kabla sijalifanya. Kama hakuna faida nitakayopata nikifanya tukio fulani ni bora niachane nalo tu maana its not worth it!

Kwaiyo ilikua nikisha calculate faida nayopata, nina jump-in chap sana, bila ku evaluate risks ndio maana nikawa nafeli, LOL
 
Inaonekana unapenda sana magendo na utapeli.
 
Mjita kama mjita kamlambisha kamanda mikwaju ...Ha ha ha ha Pole sana mzee
 
πŸ˜ƒ
Ulitokea mgomo shuleni na umeme ulikuwa umekata wana wameenda kumtia adabu headmaster mimi nikaamua kujificha bwenini nkalala deka la juu, maana mshua aliniasa mambo ya migomo nisishiriki sisi ni masikini.

Ebwana eeh majamaa wameenda wakakuta headmaster kakimbia wakaona waje kuzimalizia hasira kwa waliolala bwemi waliokataa kugoma aisee

Bwemi la mbele kuna wanawakadakwa wakaanza kushambuliwa kwa bakora huku wengine wakivunja vioo,

Nilijikuta tuu nipo sakafuni natimua mbio kuelekea kwenye shamba la mahindi, kumbe kuna mmasai na wenzake walikuwa mle ndani nao nilishangaa wameibuka kama mizimu tunaongozana kwenye mahindi
 
Pole mwanangu. Wengine wajifunze kupitia hii issue yako, wawe makini na suala la kuzaa na watu tofauti tofauti.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti kumbe kuna mmasai [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mengi mengi mengi ....mengi mnooo....ila kubwa kuliko ni kumwamini mwanaume....na sitokoma kujuta coz bado ni mwepesi sana kumwamini mtu mapema
Pole sana.....ila usijali utapata kidume atakae utendea haki moyo wako.
 
🀣🀣🀣🀣🀣 Sasa wee kwa nini hukumwambia ukweli wife kabla ya kumuoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…