Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Hii umekopi na kupaste katika movie moja hivi ya kichina. Hivi hivi umebadili tu majina ya maeneo. Sikumbuki ile movie inaitwaje ni ya comedy. Na nlijua lazima watakuja watu waanze kuuza chai humu. Movie ipo hivi hivi kila kitu. Kasoro majina na hiyo michezo wenyewe walitumia yule mtu anayekaa chini anajifanya kilema kumbe kakunja mguu pale kwenye goti kaweka kofia. The rest ni story hiyo hiyo mpaka kuvua sweta, kushuka kwa mbele kwenye daladala...kuja rudi kumchapa mapanga ya ubapa.kuchukua pochi n.kPart 2
Siku ile baada ya kudhurumiwa niliumia saana sana hasa kwa kuwa hela haikuwa yangu pia hali ya uchumi mtaani kugumu. Basi bwana, kufika jioni dogo akanichek kupata mrejesho wa betri lake, ikabidi nimwambie yule jamaa kafunga kaenda msibani so atarud after siku tatu na kununua sehemu nyingine ni bei sana. Nashukuru dogo alinielewa japo kishingo upande.
Ishu ya kudhurumiwa iliniima saana sanaa sana ilifika kipindi nipo busy na mambo mengine lakini moyoni unakuwa kama kuna kitu hvi hakiko sawa ukikumbuka unagundua hela yako imeenda kiboya. Hivo nkapanga mikakati narudishaje pesa yangu niliyodhurumiwa hadi kwa wakati ule usiku sikujua nn ntafanya.
Kesho yake mchana nkapada gari hadi pale pale kwa wachezesha bahati nasibu, lengo lilikuwa niende nisome mazingira tena nimezurumiwaje kiboya vile tena laki. Laki yangu ilikuwa inaniuma kinoma na isitoshe nimemdanganya dogo so baada ya siku tatu anategemea nimtumie betri lake na isitoshe dogo ananiamini kinoma.nilishukia kituo kinaitwa pamba road sheli. Mdogo mdogo hadi pale kufika tu pale nkasimama kuchek wahusika nkakuta yule mdada aliyeshinda begi ndo anagawa tiket yule niliyechanga nae hela ni msaidizi ndo nkagundua huu ni mchezo hakuna bahati nasibu wala nini hapa, kuwaona pale kichwa kikazidi kujaa sumu. Wale watu bhana kumbe wana mabaunsa nkaona hapa nkileta fujo ntajikuta nipo polisi so nikawa mpole. Sasa kumbe yule mdada tuliyechanga nae hela alinijua akasema kwa nguvu "kuna wengine wamerudi kufanya fujo baada ya kuliwa jana" basi mabaunsa wakaja wakanifukuza baada ya kuoneshwa kuwa ni mimi na isitoshe ni kweli jana nilitaka kufanya fujo baada ya kudhurumiwa. Nkajua hapa kitumbua kishaingia mchanga, wakanifukuza pale nkatoka lakini nikawa najua mchawi wangu ni yupi ni yule dada aliyenichongea kwa mabaunsa.
Nkatoka pale nmejaa sumu kinoma, nkaenda zangu kamanga "Bismark rock" kuna kabustani pale kwa wenyeji wa mwanza washapafahamu, nkalipia jero nkakakaa kwenye nyasi napunga upepo wa ziwa huku natafakari nini cha kufanya.
Kichwani likaja wazo nilisema nipambane nao siwawezi kwanza wana mabaunsa, niende polisi siwezi, inamaana polisi hawajui kuwa hawa jamaa ni matapeli? Nkajisemea hapa nadeal na huyu mdada aliyenichongea anajifanya mwema kumbe ni snichi. Sasa ikawa muda wa kupanga mikakati namna ya kurudisha pesa yangu.
Njia ya kwanza nkawaza nimvamie nimnyang'anye simu na hela nkaona ntaitiwa mwizi nkasema hapa lazima nijue anakaa wapi kwanza ndipo mambo mengine yaendelee.
Sasa baada ya kurudi home ilikuwa mwanzo wa mwezi na mimi ndo nakusanya hela ya maji, tunapokaa tupo wapangaji wengi kidogo, nkakusanya hela ya maji kama laki na 30 hvi nkaenda kulipa 60 na 70 nkanunua betri la dogo nkamtumia. Nkachonga na jamaa anaekujaga kukata maji kama hujamaliza deni coz tulikuwa tunafahamiana nae kiasi na namba zake nilikua nazo coz kuna msala ashawahi nisaidia, nkamuahidi baada ya wiki mbili hvi ntakuwa nshamaliza deni so likitokea lolote anisitiri coz wapangaji wenzangu wanajua bill ishalipwa yote.
Nkapanga mikakati, mkakati wa kwaza ni kubadili mwonekano ili nikirudi pale nisijulikane kirahisi, hivo nilienda kunyoa nyele zoote na ndevu yaani full para coz nilikua na nyele ndefu na madevu mengi. Kiukweli nilibadilika saana hadi demu wangu alisema hajazoea kuniona vile, pia washkaji wengine walinisahau kabisa, nilifanya hvi ili nisigundulike hata nikimfatilia yule dada anapokaa hata tukipanda daladala moja asihisi chochote.
Katika maisha mimi huwa naamini kuwa tunaishi mara moja tu so ninachoamini, jambo likiumiza kama umeamua kusamehe basi samehe kama kulipiza kisasi, lipiza coz maisha ni kma maji yanayo toka mlimani kwenda bondeni yakipita hayarudi tena kwa kifupi tunaishi mara moja tu, punguza majuto katika maisha. falsafa hii ndio chanzo cha kujiita "MTAMAUSHI" kwa waliosoma somo la kiswahili vizuri levo ya chuo na advance wanaelewa nini maana ya falsaha hii ya ndugu E kezilahabi kma sijakosea.
Tuachane na falsafa, baada ya kubadili mwonekano nkarudi tena pale pale kwa wanapochezesha bahati nasibu lakini awamu hii nilirudi jioni saa 10:30. Nilikaa pembeni kidogo walikua wanakaanga chipsi, nkaagiza chipsi na soda nikawa nakula taratibu nkivizia wafunge. Baada ya kumaliza kula nkaagiza soda nyingine nkaanza kunywa taratibu, kweli bhana saa 11: 30 hvi wakawa wamefunga wanakusanya kila kitu pale wakakutana pembeni kama kimduala hvi wakagawana hela ndo nilipojua kumbe wanapiga mkwanja mrefu. Hela alikuwa anagawa kiongozi wao, baada ya kugawana wakaanza kusepa wengine kwenye gari lililobeba vyombo wengine kwa miguu, target yangu ilikua ni yuje mdada tu. Akatoka pale mdogo mdogo akaingia sokoni mimi nyuma yake ila kwa mbali na umakini mkubwa sana asijue lolote. Yule dada alinunua vitu vichache pele akaenda kupanda gari. Baada ya kufika kwenye gari alikaa siti ya mbele kwa dereva nilichofurahi ni kwamba alikuwa kumbe anakaa njia ambayo namimi naishi huko hvo alinipunguzia garama ya usafiri coz niliapa kokote anakokaa nitamfata tu. Basi bhana baada ya abiria kujaa nkajisogeza pale nikakaa ndani ya daladala gari likaondoka likapita kituo ninachoshukiaga mimi hadi kama vituo 5 mbele yule dada akashuka. mimi sikushuka, gari lilipoanza kuondoka limetembea mita chache nkamwambia konda anishushe nilikua nimejisahau kweli nilishushwa ila kwa matusi na misonyo kibao ya konda kwamba sipo makini kumbe nilipanga iwe hvo. Baada ya kushuka tu nilianza kwenda kituoni kumchek yule dada, nikamwona kwa mbali anatembea. Nilikua nmevaa sweta jeusi nikavua nkabaki na shati tu nilifanya hvo asikumbuke kama tumepanda wote daladala kama aliniona. nilimfatilia hadi anapokaa nkapajua uzuri nyumba ilikua imejitenda kidogo na njia ina kichaka na uchochoro kidogo.
Baada ya kujua anapokaa nilirudi zangu geto kusubiri nifanye revange yangu, baada ya siku kadhaa saa 12:00 nipo kituoni namsubiri mfukoni nina bonge la panga. Saa moja na dk kadhaa nkamwona kashuka nikatangulia mbele coz yeye alipita kununua mhindi choma pale standi. Kwa wakati ule nilikua nakumbuka ile kauli yake ya "kuna wengine wamerudi kufanya fujo baada ya kuliwa" hii kauli iliniuma sana. Sikuwa na lengo la kumdhuru ila tu nirudishe hela yangu tu.
Baada ya kutangulia mbele nnkaanza kutudi nilikotoka tukakutana jiani nkachomoa panga. Nkamwambia naomba hela zangu, akauliza hela ipi? nilimpa ubapa wa mgongoni nkamwambia ukipiga kelele umekwisha, alitetemeka yule dada sijapata ona. nkamwambia leo nimekufata na huku mnapenda kudhurumu watu mbwa nyie. lete mkoba akawa anabisha nkampa bapa la pili akaachia nkazama kwenye mkona nkatoa simu na hela nkasepa zangu mbio uchochoroni nkamwacha anali na isitoshe watu hawakuwepo .Njiani nkadaka boda hadi karibu na geto nkashuka. Nilipofika home kuhesabu nkakuta hela kma 70 hvi simu, nkawafata wahuni kesho yake nkawauzia kama 50 ilikua smartphone. Nkalipa deni la maji na usumbufu.
Inayofuata:
Fema club walisababisha nikamatwe na bro nikiwa napiga punyeto kisa ile kauli yao ya punyeto ni njia salama, ntawalete kisa soon