Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

dah naumwa ila nimecheka sana[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mara nyingi sipend kukoment huwa nasoma tu ila jambo ninalojuta mpaka kifo changu ni mamayangu mdogo alikua anaiita mziwanda japo mimi kwetu ni mtoto wa 3 kuzaliwa tupo wa 4 kifupi tulikua tunapendana sana hata jando yangu ya kwanza nilipata nikiwa kwake,

Kipind anaumwa nilikua nishakua mkubwa lakin bado tu close sana sasa sijui ni uoga na kuamini atapona nipata taarifa mama yako mdogo mpendwa wako anasema ukamsalimie hospital nikasema nitaenda akitoka (kosa kubwa sana nilifanya japo niliamini atapona nitaenda kumchek akiwa mzima)
Nilikua sipend kwenda kumuangalia mgonjwa nilikua kama naona kama namkejel hiv so nikasema akitoka nitaenda kumchek tuu)

Alikua anauza viatu vya kimasai na kabla hajapelekwa hospital mama yangu mzazi (dada yake mkubwa) alienda kumsalimia akampa pair moja anipe.

Huwez kuamini baada ya siku kadhaa kama siku 3 akafarik BILA KWENDA KUMUONA MUHIMBILI HOSPITAL.

Hili jambo huwa linaniuma sana sana sana nikikumbuka wema wake kwangu na nilichofanya huwa najuta sana yan nataman siku zingerudi nyuma huwa nikiona picha zake na kukumbuka wema wake kwangu huwa najuta najuta najuta
Nyie acheni tu
 
Pole Sana ..inauma Sana..
Na Mimi Kuna Bibi yake mke wangu..alikuwa ananipenda Sana..aliugua akatwambia niende nimuone lakini sikwenda..baada ya muda akafariki bila Mimi kwenda kumuona..inaniuma Hadi Leo..nilikosea Sana..
 
Umenikumbusha kisa cha binti mmoja aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022, siku za nyuma kabla ya kifo chake alionyesha dalili za kunipenda sana kimapenzi na nilijua ila sikutaka kuingia mkenge sababu ameolewa na jamaa yake nafahamiana naye japo hatuko karibu sana.

Yule binti alipoona sielewi somo siku moja akajifanya amelewa, akasema yote ya moyoni kuhusu mimi, nilimsikiliza na nilielewa kiasi gani anamaanisha ila bado nikapuuza sababu ameolewa.

Wiki kadhaa baadaye akafariki kwenye ajali, huwa nawaza mengi sana. Ni kama alijua atakufa, bahati nzuri alikufa akiwa ameshatua mzigo wa moyo, imebaki siri kubwa, siri kati yangu na marehemu. Kila nikimuona mwanaye namkumbuka sana mama yake.

Ni miezi sita sasa, endelea kupumzika mama Ade***ina. Hata ungekuwa hai sikuwa na namna ya kukusaidia ulikuwa mke wa mtu nami mume wa mtu.
 
Niliwahi pita na nguruwe kwenye pikipiki mbele ya Msikiti dah tulichapana sana na madogo wa msikitini pale. Wakanizidia bahati raia wakajaa. Ila nilizongwa sana. Nilichapika sana
[emoji23][emoji23]
 
Hamna cha kujutia hapo. Ulifanya uamuzi sahihi.
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

[emoji23][emoji23][emoji23]hii story sitochoka kucheka
 
Asee mapenzi ni ufala
 
Nakumbuka mwaka 2018 nlipewa ada 3M ili nikaanze chuo PASIANSI MWANZA
Mhuni nkaweka ada mfukoni, nkafka mwanza nkapanga geto,nunua godoro, gesi na mahitaj mengne kama milioni ikaisha, nkabaki na 2M
Nkaanza kubet naweka stake ya lak 5 kwa game 4 tofauti, nakumbuka nlishinda shinda had mtaji kufika 4M, nkanunua pkpk King lion 1,nkawa napga boda pale buzuruga shule, kipind cha likizo nkawa naenda home kama kawa, sasa ikafka hatua mda wa kumalza chuo ukafka maana cozi ni mwaka mmoja, mzee akaniambia niende kuna mkubwa mmoj yupo ngorongoro anahitaj chet changu, hapo mhuni sijui ata definition ya elephant, kilichotokea mungu pekee ndo anajua, nlibadili line ya sim, had mwaka 2021, ndo nkaenda home nkiwa nipo stable financially, matusi hadi kupelekwa polisi,ila saiv mamb yameisha japo naumia maan mdgo angu alisoma pasiansi na saiv n askar game ngorongor ila mm bado nakomaa na mtaa, USIJARIBU KULA ADA,,, sorry kwa uandish mbovu
 
Umetisha sana mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…