Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Another One!

Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.

Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani hivi wa Computer [Sitasema ni System gani].

Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu ya namna ambavyo mfumo uliwarahisishia kazi.

Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.

Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!

Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.

Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao kimya kimya na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!

Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee

Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh

Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.

Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.

Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favour tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.

Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.

Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!

Na hilo likawa funzo langu!
Wewe ujanja ujanja umezoea nilidhani ile ishu ya risiti ingekuwa somo kwako kumbe wapi umeenda Nairobi tena kuharibu ila ndio hivyo ujana Mungu akutangulie
 
CRYPTOCURRENCY

Nimepambania kombe huku na kule Mil 3 hizi hapa. Nawaza sasa pa kuzipeleka ili mtonyo uongezeke. Mishe zilizopo mezani wakati huo zimebana sana. Kwaiyo kusema niende nikafanye kilimo au nifungue biashara mahali itakua changamoto kidogo kwenye kufuatilia.

Napita pita social media [wakati huo facebook ni moto sana sio kama saivi] nakutana na habari za kudownload pesa kwa mara ya kwanza; mambo ya cryptocurrency na forex. Nikawa interested. Nikaanza kufuatilia kwa ukaribu nikagundua kuna jamaa mmoja mkenya anasaidia watu ambao hawana uzoefu wa ku trade then baadae mnagawana faida.

Mshenzi yule alikua amejipanga. Alikua hadi ana post video za watu mbali mbali wanaotoa ushuhuda namna jamaa alivyo wasaidia na kubadilisha maisha yao. Duh, nikaona mtonyo si ndio huu sasa. Na hivi sina muda mishe kama hizi za kimtandao ndio zenyewe. Namalizia kila kitu kwenye simu. Sasa nikapiga mahesabu wale watu ninao waona kwenye clips hawakua hata na cha kuanzia kikubwa na sasahivi maisha yao yamebadilika, Je mimi mwenye Mita 3? Si ndio na kazi nitaacha kabisa. Nikaona hii ni fursa ngoja nim.dm mwamba.

Jamaa alikua Active sana. Akanitumia magazeti kadhaa ya kupitia ili nielewe namna utaratibu mzima unavyoenda. Nikayasoma yote nikawa nimeelewa. Maskini mtoto wa watu kumbe naingizwa mjini hata sielewi.

Nakumbuka alini.introduce kwenye platform moja inaitwa coinxtrading au paxel kama sikosei. Una create account unaweka details zako personal mpaka bank Account No. zako. Then kianzio cha chini ni USD 100, wakati huo ilikua kama laki 2 kasoro hivi, sikumbuki vizuri exchange rate ya siku hiyo. Mwamba nikatupia Dollar zangu 100.

Hiyo system ukishajisajili lazima umchague jamaa kama meta trader wako unayemuamini. Kwaiyo akaniambia jina la kuchagua pale nikamchagua chap kazi ikaanza.

Mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya kama siku mbili naingia kwenye system, nakuta mtonyo unasoma USD 400. Nikasema mambo si ndio haya sasa. Unaingiza Dollar 300 ndani ya masaa 48 tu, tena hata sijatoka Jasho. Ewaaa nimeulaaa huku nikicheka kitajiri. Sikujua kitakachonikuta..

Siku moja baada ya kuona ile $400, jamaa akanicheck inbox. Akaniambia mambo yanaenda vizuri kwaiyo nimtumie commision yake ya $150 maana tunagawana faida. Nikamwambia toa tu hapo kwenye hiyo iliyopatikana kwenye mfumo. Akasema niache ujinga kwa sababu nikipunguza pesa ya kwenye system itabidi nianzie chini tena. Wakati nikiacha hiyo $400 aka trade itaongezeka haraka zaidi. Akanipa ka somo nikamuelewa.

Basi nikaenda Bank nikafanya niliyotakiwa kufanya jamaa akapata pesa zake. Akaendelea kutrade.

To cut a long story short;

Kuna muda ilifika hadi $3000. Akawa ameniambia nimpe faida yake then anifanyie namna nitoe pesa zangu. Yule Mbwa sijui alinusa harufu kuwa nitamsanukia maana nilikua kama nimeshachoshwa na hizo habari za niache hela kule kwenye mfumo hadi zijae jae.

Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu ku withdraw ikawa inagoma. Jamaa akaniambia siwezi ku withdraw bila yeye kunisaidia. Kana kwamba kuna process kidgo za kupitia mpaka pesa itoke. Daah nilitakiwa nikimbie haraka baada ya kuambiwa hivyo ila tamaa zikanifanya nimuamini ki bloody fool sana.

Baada ya kumtumia commision yake ya kitu kama $1200, dana dana zikaanza. Hapo karibu hela yote ameshachukua. Nimebaki na kama laki 2 tu kwenye ile Mil 3 niliyokua nayo. Sasa akili ndio zikaanza kurudi. Alivyoona kila anavyoniletea story za kuendelea kutrade nagoma, na ninachotaka ni kuwithdraw tu pesa.. akaniblock. Sijakaa vizuri nikawa logged out kwenye system. Aiseee

Niliumia sana. Nilijuta kuamini watu ki rahisi rahisi. Nilihangaika sana ku log in lakini wapi. Tukana sana jamaa inbox lakini wapi. Pesa imekwenda na maji. Hairudi tena. 3M niliyoitesekea zaidi ya mwaka is gone tena ndani ya wiki mbili tu. Nilikua depressed sana. Nikaona hii aibu siwezi hata kushirikisha wenzangu. Nikachukua leave nikaomboleze kidogo nyumbani.

Hapa nilijifunza kitu kuhusu utapeli. Nika recover, maisha yakaendelea [emoji1491]

Ukiona unalazimishiwa sana fursa, ujue wewe ndiyo fursa yenyewe.
 
And Another...

Nimepambania kombe huku na kule Mil 3 hizi hapa. Nawaza sasa pa kuzipeleka ili mtonyo uongezeke. Mishe zilizopo mezani wakati huo zimebana sana. Kwaiyo kusema niende nikafanye kilimo au nifungue biashara mahali itakua changamoto kidogo kwenye kufuatilia.

Napita pita social media [wakati huo facebook ni moto sana sio kama saivi] nakutana na habari za kudownload pesa kwa mara ya kwanza; mambo ya cryptocurrency na forex. Nikawa interested. Nikaanza kufuatilia kwa ukaribu nikagundua kuna jamaa mmoja mkenya anasaidia watu ambao hawana uzoefu wa ku trade then baadae mnagawana faida.

Mshenzi yule alikua amejipanga. Alikua hadi ana post video za watu mbali mbali wanaotoa ushuhuda namna jamaa alivyo wasaidia na kubadilisha maisha yao. Duh, nikaona mtonyo si ndio huu sasa. Na hivi sina muda mishe kama hizi za kimtandao ndio zenyewe. Namalizia kila kitu kwenye simu. Sasa nikapiga mahesabu wale watu ninao waona kwenye clips hawakua hata na cha kuanzia kikubwa na sasahivi maisha yao yamebadilika, Je mimi mwenye Mita 3? Si ndio na kazi nitaacha kabisa. Nikaona hii ni fursa ngoja nim.dm mwamba.

Jamaa alikua Active sana. Akanitumia magazeti kadhaa ya kupitia ili nielewe namna utaratibu mzima unavyoenda. Nikayasoma yote nikawa nimeelewa. Maskini mtoto wa watu kumbe naingizwa mjini hata sielewi.

Nakumbuka alini.introduce kwenye platform moja inaitwa meta trader kama sikosei. Una create account unaweka details zako personal mpaka bank Account No. zako. Then kianzio cha chini ni USD 100, wakati huo ilikua kama laki 2 kasoro hivi, sikumbuki vizuri exchange rate ya siku hiyo. Mwamba nikatupia Dollar zangu 100.

Hiyo system ukishajisajili lazima umchague jamaa kama trader wako unayemuamini. Kwaiyo akaniambia jina la kuchagua pale nikamchagua chap kazi ikaanza.

Mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya kama siku mbili naingia kwenye system, nakuta mtonyo unasoma USD 400. Nikasema mambo si ndio haya sasa. Unaingiza Dollar 300 ndani ya masaa 48 tu, tena hata sijatoka Jasho. Ewaaa nimeulaaa huku nikicheka kitajiri. Sikujua kitakachonikuta..

Siku moja baada ya kuona ile $400, jamaa akanicheck inbox. Akaniambia mambo yanaenda vizuri kwaiyo nimtumie commision yake ya $150 maana tunagawana faida. Nikamwambia toa tu hapo kwenye hiyo iliyopatikana kwenye mfumo. Akasema niache ujinga kwa sababu nikipunguza pesa ya kwenye system itabidi nianzie chini tena. Wakati nikiacha hiyo $400 aka trade itaongezeka haraka zaidi. Akanipa ka somo nikamuelewa.

Basi nikaenda Bank nikafanya niliyotakiwa kufanya jamaa akapata pesa zake. Akaendelea kutrade.

To Cut the Story Short.

Kuna muda ilifika hadi $3000. Akawa ameniambia nimpe faida yake then anifanyie namna nitoe pesa zangu. Yule Mbwa sijui alinusa harufu kuwa nitamsanukia maana nilikua kama nimeshachoshwa na hizo habari za niache hela kule kwenye mfumo hadi zijae jae.

Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu ku withdraw ikawa inagoma. Jamaa akaniambia siwezi ku withdraw bila yeye kunisaidia. Kana kwamba kuna process kidgo za kupitia mpaka pesa itoke. Daah nilitakiwa nikimbie haraka sana baada ya kuambiwa hivyo ila tamaa zikanifanya nimuamini ki bloody f*cking sana.

Baada ya kumtumia commision yake ya kitu kama $1200, dana dana zikaanza. Hapo karibu hela yote ameshachukua. Nimebaki na kama laki 2 tu kwenye ile Mil 3 niliyokua nayo. Sasa akili ndio zikaanza kurudi. Alivyoona kila anavyoniletea story za kuendelea kutrade nagoma, na ninachotaka ni kuwitthdraw tu pesa.. akaniblock. Sijakaa vizuri nikawa logged out kwenye system. Aiseee

Niliumia sana. Nulijuta kuamini watu ki rahisi rahisi. Nilihangaika sana ku log in lakini wapi. Tukana sana jamaa inbox lakini wapi. Pesa imekwenda na maji. Hairudi tena. 3M niliyoitesekea zaidi ya mwaka is gone tena ndani ya wiki mbili tu. Nilikua depressed sana. Nikaona hii aibu siwezi hata kushirikisha wenzangu. Nikachukua leave nikaomboleze kidogo nyumbani.

Ukiona unalazimishiwa sana fursa ujue wewe ndio fursa yenyewe.

Hapa nilijifunza kitu kuhusu utapeli. Nika recover, maisha yakaendelea [emoji1491]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nmecheka balaa

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Mengi mengi mengi ....mengi mnooo....ila kubwa kuliko ni kumwamini mwanaume....na sitokoma kujuta coz bado ni mwepesi sana kumwamini mtu mapema
Kuna mtu anaisoma hii comment na kujiinamia kwa uzuni huku akisema "i wish ningepata/nipate mwanamke kama huyu"

Bado una nafasi usijari utapata wa aina yako cha mhimu ni uzima tu
 
And Another...

Nimepambania kombe huku na kule Mil 3 hizi hapa. Nawaza sasa pa kuzipeleka ili mtonyo uongezeke. Mishe zilizopo mezani wakati huo zimebana sana. Kwaiyo kusema niende nikafanye kilimo au nifungue biashara mahali itakua changamoto kidogo kwenye kufuatilia.

Napita pita social media [wakati huo facebook ni moto sana sio kama saivi] nakutana na habari za kudownload pesa kwa mara ya kwanza; mambo ya cryptocurrency na forex. Nikawa interested. Nikaanza kufuatilia kwa ukaribu nikagundua kuna jamaa mmoja mkenya anasaidia watu ambao hawana uzoefu wa ku trade then baadae mnagawana faida.

Mshenzi yule alikua amejipanga. Alikua hadi ana post video za watu mbali mbali wanaotoa ushuhuda namna jamaa alivyo wasaidia na kubadilisha maisha yao. Duh, nikaona mtonyo si ndio huu sasa. Na hivi sina muda mishe kama hizi za kimtandao ndio zenyewe. Namalizia kila kitu kwenye simu. Sasa nikapiga mahesabu wale watu ninao waona kwenye clips hawakua hata na cha kuanzia kikubwa na sasahivi maisha yao yamebadilika, Je mimi mwenye Mita 3? Si ndio na kazi nitaacha kabisa. Nikaona hii ni fursa ngoja nim.dm mwamba.

Jamaa alikua Active sana. Akanitumia magazeti kadhaa ya kupitia ili nielewe namna utaratibu mzima unavyoenda. Nikayasoma yote nikawa nimeelewa. Maskini mtoto wa watu kumbe naingizwa mjini hata sielewi.

Nakumbuka alini.introduce kwenye platform moja inaitwa meta trader kama sikosei. Una create account unaweka details zako personal mpaka bank Account No. zako. Then kianzio cha chini ni USD 100, wakati huo ilikua kama laki 2 kasoro hivi, sikumbuki vizuri exchange rate ya siku hiyo. Mwamba nikatupia Dollar zangu 100.

Hiyo system ukishajisajili lazima umchague jamaa kama trader wako unayemuamini. Kwaiyo akaniambia jina la kuchagua pale nikamchagua chap kazi ikaanza.

Mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya kama siku mbili naingia kwenye system, nakuta mtonyo unasoma USD 400. Nikasema mambo si ndio haya sasa. Unaingiza Dollar 300 ndani ya masaa 48 tu, tena hata sijatoka Jasho. Ewaaa nimeulaaa huku nikicheka kitajiri. Sikujua kitakachonikuta..

Siku moja baada ya kuona ile $400, jamaa akanicheck inbox. Akaniambia mambo yanaenda vizuri kwaiyo nimtumie commision yake ya $150 maana tunagawana faida. Nikamwambia toa tu hapo kwenye hiyo iliyopatikana kwenye mfumo. Akasema niache ujinga kwa sababu nikipunguza pesa ya kwenye system itabidi nianzie chini tena. Wakati nikiacha hiyo $400 aka trade itaongezeka haraka zaidi. Akanipa ka somo nikamuelewa.

Basi nikaenda Bank nikafanya niliyotakiwa kufanya jamaa akapata pesa zake. Akaendelea kutrade.

To Cut the Story Short.

Kuna muda ilifika hadi $3000. Akawa ameniambia nimpe faida yake then anifanyie namna nitoe pesa zangu. Yule Mbwa sijui alinusa harufu kuwa nitamsanukia maana nilikua kama nimeshachoshwa na hizo habari za niache hela kule kwenye mfumo hadi zijae jae.

Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu ku withdraw ikawa inagoma. Jamaa akaniambia siwezi ku withdraw bila yeye kunisaidia. Kana kwamba kuna process kidgo za kupitia mpaka pesa itoke. Daah nilitakiwa nikimbie haraka sana baada ya kuambiwa hivyo ila tamaa zikanifanya nimuamini ki bloody f*cking sana.

Baada ya kumtumia commision yake ya kitu kama $1200, dana dana zikaanza. Hapo karibu hela yote ameshachukua. Nimebaki na kama laki 2 tu kwenye ile Mil 3 niliyokua nayo. Sasa akili ndio zikaanza kurudi. Alivyoona kila anavyoniletea story za kuendelea kutrade nagoma, na ninachotaka ni kuwitthdraw tu pesa.. akaniblock. Sijakaa vizuri nikawa logged out kwenye system. Aiseee

Niliumia sana. Nulijuta kuamini watu ki rahisi rahisi. Nilihangaika sana ku log in lakini wapi. Tukana sana jamaa inbox lakini wapi. Pesa imekwenda na maji. Hairudi tena. 3M niliyoitesekea zaidi ya mwaka is gone tena ndani ya wiki mbili tu. Nilikua depressed sana. Nikaona hii aibu siwezi hata kushirikisha wenzangu. Nikachukua leave nikaomboleze kidogo nyumbani.

Ukiona unalazimishiwa sana fursa ujue wewe ndio fursa yenyewe.

Hapa nilijifunza kitu kuhusu utapeli. Nika recover, maisha yakaendelea [emoji1491]

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nami nishee yangu moja,
Nimemaliza chuo mwaka wa jana yaani 2021. Sasa mwanzoni wakati naanza chuo nilifanikiwa kulipa ada yote iliyokuwa inatakiwa ili nisajiliwe chuoni ni kama 1.4m, kwani sikufanikiwa kupata mkopo katika awamu ya kwanza na ya pili. Basi masomo yaliendelea kwa wiki kama tatu ivi, baadae ikatoka awamu ya tatu na jina langu likawepo asilimia kama 50% ya ada nalipiwa na loan board.
Hivyo nikapata ushauri kwanini nisiende kudai hela yangu ile ambayo inazidi ilikua kitu kama laki 7 na ushee. Nikaona ni wazo zuri na bora ukizingatia na maisha ya chuo bila doh ni unyonge sanaa. Sasa katika harakati za kuandika barua ya madai na kuifatilia sanaaa yaaani sanaaa by mwezi wa sita mkuu wa chuo ndo akasain cheki yangu ya laki 7. Basi kidume nikatoka na kudondoka bank kuchukua mapene kwa ajiri ya kuyaburuza alooo niliburuza atari (sijawahi kula ada ila jamani ada tamu aseee kuliko ata boom).
Sasa mwaka ukakatika na kuanza mwaka mwingine ajabu ni kwamba kwenye account yangu ada ilikua inasoma ile ile kwamba nawadai chuo 700,000/= kwamba ile hela nilioomba nirudishiwe haikupunguzwa kwenye system nikasema apa bingo nkajaribu kwenda kwa muhasibu na payslip ya id na student union, nkashangaa kaanguka sign [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] nkasema maisha si haya.
Mpaka namaliza mwaka wa tatu, nafanya mahafari nachukua certificate na hadi juzi nimechukua transcript naona kimya.

APA JANA NIMETOKA CHURCH KUTOA SADAKA YA SHUKRANI KWA MIUJIZA

OVA[emoji41][emoji41][emoji41]
Sijaona kinachoweza kukufanya ujute hapa [emoji2365]
 
Hela ndio ilikua motivation. Siwezi kuingia kwenye msala kama hakuna Chambi kidogo. Toka nikiwa mdogo kuna Mentality fulani Mother alikua anaijenga kichwani kwangu kila nikifanya kosa..

Mara nyingi alikua ananiambia "Wewe umefanya kitu flani umekamatwa, umechapwa sasa kilikua kinakusaidia nini hata kama usingedakwa?"

Kwaiyo ni kama alikua ananiambia niweke kila tukio kwenye uzani (balance) na faida nayopata kabla sijalifanya. Kama hakuna faida nitakayopata nikifanya tukio fulani ni bora niachane nalo tu maana its not worth it!

Kwaiyo ilikua nikisha calculate faida nayopata, nina jump-in chap sana, bila ku evaluate risks ndio maana nikawa nafeli, LOL
We jamaa fala sana [emoji23][emoji23][emoji23]
Eti "Siwezi kuingia kwenye msala kama hakuna Chambi kidogo"
 
[emoji2]
Ulitokea mgomo shuleni na umeme ulikuwa umekata wana wameenda kumtia adabu headmaster mimi nikaamua kujificha bwenini nkalala deka la juu, maana mshua aliniasa mambo ya migomo nisishiriki sisi ni masikini.

Ebwana eeh majamaa wameenda wakakuta headmaster kakimbia wakaona waje kuzimalizia hasira kwa waliolala bwemi waliokataa kugoma aisee

Bwemi la mbele kuna wanawakadakwa wakaanza kushambuliwa kwa bakora huku wengine wakivunja vioo,

Nilijikuta tuu nipo sakafuni natimua mbio kuelekea kwenye shamba la mahindi, kumbe kuna mmasai na wenzake walikuwa mle ndani nao nilishangaa wameibuka kama mizimu tunaongozana kwenye mahindi
Daaah [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekata tamaa mkuu,wanaokuja ni walewale umiza kichwa....
Kuna utumwa FULANI umeasisiwa na Dini hasa kikristo ambao ni KUFUNGA ndoa tena ndoa ya mke MMOJA tu!!!kwamba bila jicho ndoa unakua mdhambi na mnateseka kweli!!!

KWA Kuwa una kipato Chako Kuwa HURU Angalia mtu ambaye unajivunia hata ukiwa nae Karibu mtu ambae anatosha nafsini mwako na usiwe na wazo la kuvaa shela utumwa bali ukaribu ule wa KILA siku wa kushea changamoto zote hata kama ameoa wewe kama una mfeel Kuwa nae!!wala Dini sijui moto sijui ujinga GANI na presha za Maisha zisikuchanganye, mradi awe anaingia kwako na kutoka na WATU wanaona kwamba mwamba anamiliki!

Ulilelewa kelele coz ameoa we sema mi mke wa pili na fresh tu SIJALI!!!usifinyangwe moyo I na wazo la ndoa na shela wakati ubikira ulishaupoteza!!wanaofunga ndoa na sio bikra wanajidanganya kwani ndoa yao ya kweli ni ile siku wamepoteza bikra hizo nyingine ni tafrija za kula wali na picha za kwenye fremu!!!!Achana na matazamio makubwa ya uongo AMBAYO yatakuumiza usifurahie Maisha!

IMANI ZA KIDINI ZINATESA WATU SANA COZ ZIMAZUIA ASILI HALISI ZA BINADAMU NA UUMBAJI!!!!CHANGAMKA WEWE MBONA MSOMI!HALAFU UNATUANGUSHA !!!?
 
Nimekata tamaa mkuu,wanaokuja ni walewale umiza kichwa....
Kuna utumwa FULANI umeasisiwa na Dini hasa kikristo ambao ni KUFUNGA ndoa tena ndoa ya mke MMOJA tu!!!kwamba bila jicho ndoa unakua mdhambi na mnateseka kweli.

KWA Kuwa una kipato Chako Kuwa HURU Angalia mtu ambaye unajivunia hata ukiwa nae Karibu mtu ambae anatosha nafsini mwako na usiwe na wazo la kuvaa shela utumwa bali ukaribu ule wa KILA siku wa kushea changamoto zote hata kama ameoa wewe kama una mfeel Kuwa nae!!wala Dini sijui moto sijui ujinga GANI na presha za Maisha zisikuchanganye!!mradi awe anazingua kwako na kutoka na WATU wanaona kwamba mwamba anamiliki!!ukipigiwa kelele coz ameoa we sema mi mke wa pili na fresh tu SIJALI!!!usifinyangwe moyo I na wazo la ndoa na shela wakati ubikira ulishaupoteza!!wanaofunga ndoa na sio bikra wanajidanganya kwani ndoa yao ya kweli ni ile siku wamepoteza bikra hizo nyingine ni tafrija za kula wali na picha za kwenye fremu!

Achana na matazamio makubwa ya uongo AMBAYO yatakuumiza usifurahie Maisha!!!!IMANI ZA KIDINI ZINATESA WATU SANA COZ ZIMAZUIA ASILI HALISI ZA BINADAMU NA UUMBAJI.

CHANGAMKA WEWE MBONA MSOMI!HALAFU UNATUANGUSHA !!!
 
Back
Top Bottom