Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Another One!

Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.

Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani hivi wa Computer [Sitasema ni System gani].

Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu ya namna ambavyo mfumo uliwarahisishia kazi.

Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.

Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!

Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.

Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao kimya kimya na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!

Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee

Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh

Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.

Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.


Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favour tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.


Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.

Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Naona kama mimi ni mtu wa mikosi tu. Kwanini michongo meusi inanipitia mimi tu? Dah nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!


Na hilo likawa funzo langu!
Daah wazungu walikuheshim sana mkuu .hiyo mitaa ulikua ukiishi ni ushuani sana ,haipishani sana na spring valley ni uzunguni kama osterbay na masaki kwa bongo
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua,,,, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp
Duuh how ? Ndiyo origin of this name Terminator?
 
JKT

Katika harakati za kutafuta Ugali nilijikuta nimeomba kujiunga na jeshi la JKT. Nikatupiwa Kigoma, kule Bulombora 821KJ.

Nikapigishwa jaramba na kulishwa vumbi huku nikitazama ziwa Tanganyika kwa ukaribu kabisa lililozungukwa na mawese ya kutosha. Ruka Juu, Kanyaga Chini kwa nguvu mpaka mguu utoke nje ya kiatu.


Mikesha ilivyozidi nikaona hapa nitakufa. Nikaanza harakati za kutafuta nafasi ya kulala vizuri maana zile Dakika 5 unazopewa za kulala hazitoshi kabisa. Nikaanza kutafuta machimbo. Wenzangu wakienda mkesha, mimi najipeleka porini. Siku nyingine nakutana na ma afande na wao wamedoji kwenda lindo wananitimua najikuta nimerudi kulala uvunguni.

Tabia yangu ya kujizoesha kulala ikaanza kunigharimu. Ikafika mahali nikawa siwezi kabisa kwenda kukesha hata siku moja. Nikaanza kuona hadi uvivu wa kwenda kulala mbali na anga letu. Nakumbuka nilikua Eagle Coy.

Siku hiyo nimelala uvunguni nakoroma kabisa, saa ngapi afande asiingie ndani kutafuta watoro. Si akaniskia navyokoroma kule chini ya kitanda. Dah sitasahau hiyo kipigo niliyopewa. Nakumbuka al manusura nipoteze jicho. Maana vile vitanda vimechomelewa kwaiyo kuna kama vichuma flani hivi kama nondo vimejitokeza kwa juu, alinibamiza kichwa kwenye kile kitanda ile nondo ikachubua kidogo pembeni ya jicho.

Sijui nilipata wapi ujasiri nikamsukuma pembeni nikasogeza kioo cha dirisha nikarukia nje nikaanza kukimbia huku nachechemea machozi yananitoka ya kutosha. Jamaa nadhani aliniangalia navyokimbia kwa tabu akanionea huruma akaamua kuachana na mimi huku akisema "Nitakuua Mbwa Wewe".

Nilivyofika walipo wenzangu kwenye mkesha nikapokelewa tena na adhabu za kubiringita na kukwepa ndege za kivita. Dah.. nilihisi mwisho wangu umefika, nikasema kwa sauti "Nakufa" huku machozi yanatoka ili hata jamaa anionee huruma lakini wapi. Yeye kakazana kunioshea na kunifanya mfano kwa wengine. Saiyo pumzi imekata, maumivu kila mahali, machozi yameshatoka mpaka yamekauka, siwezi kuongea tena. Ni kwa Neema za Allah pekee nilifanikiwa kuona tena Jua siku iliyofuata maana nilikua nahisi kabisa nakufa. Hali yangu ilikua mbaya sana!

Sikuwahi kujuta kwenye maisha yangu kama hiyo siku. Nililaani uamuzi wangu wa kwenda huko. Kile kitu kilinikaa sana moyoni kwa muda mrefu. Niliona kabisa huku sio kwangu. Course ilivyoisha, wakati wengine wanasikilizia kwenda JWTZ na Polisi, mimi nikaandaa nauli yangu, nikavizia ule muda tunaotumwa kwenda town...nikatorokea huko mazima na nikaapa sitarudi tena. Ikawa imeisha hiyo!

Kwa kweli mambo ya Jeshi yana watu wake. I was not one of them!
 
Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa ww n km sister tu bhanaa ,weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA ,,,baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kbs
🤣🤣🤣 Daah! Nimecheka sana
 
Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six


Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa


Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)



Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)
Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea


Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani



Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana



Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform



Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika
Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)



Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa

Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
😆😆😆 inafurahisha na kusikitisha at the same time. Vipi magodoro ulilipa?
 
Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.

Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.
Pambana baharia, ndo matokea ya nature yenu wanaume. Halafu mnajiuliza why wanaume hufa mapema...jibu ni kwasababu ya hizo stress zenu za kujitakia.
 
Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.

Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.
Njia pekee ya kuishi kwa amani kama wanao wanajitambua muombe mkeo mje muishi nao,wanawake somtym tuna mambomengi

Kwanza kufanya watoto wetu ndo sehemu ya kumaliza shida zetu la pili unaweza jikuta unawekwa mbali na mwanao siku ambayo utamjibu huna kitu so kuepusha hayo Lea wanao kma unaweza kuwahudumia wakiwa mbali sidhani km itashindikana.
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua,,,, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp
Ukiua bila kukusudia siyo murder ni manslaughter kwakuwa hakukuwa na malice afforethought.Katubu moja kwa moja kwa Mungu wako unayemuamini na Toba yako itapokelewa.
 
Nikiwa sekondari nilikuwa na masela wangu tunatoroka daily. Yaani tukiona shuleni tuu haukueleweki tunasepa. Mtoto wa headmaster ndiyo alikuwa kiongozi alikuw na mkasi wa kukatia fensi, anakata raia tunayeya.

Basi bana siku moja tuko njemba kama sita. Wa kwanza akapita kweny tundu la fens akaruka, kulikuwa na kimtaro halaf ndiyo unaingia main road. Watano Tukapita wote frexh tukaanza kuicha main road tunazitafuta CHOCHO, sasa yule wa Sita anaingia tuu main road mara gari ya headmaster hii hapa ikasimama mbele yake.

Headmaster akamuita jamaa anatukimbilia sisi, headmaster akatucheki na sisi pia japo kwa mbali tukawa hatuna namna ikabidi tuongeze spidi. Kufika chocho zaidi Tukamlaum sana jamaa katupa msala bora asingemkimbia headmaster angeend wamalizane. [emoji16]

Kesho yake school ikapigwa ambush ya maana jamaa akataja alikuw na sisi tulichezea haswa na tukanunua fensi ya shule nzima
 
Hahahah- pole sana mkuu, kisa chako najiona kabisa ni mimi, japo tofauti ni ndgo, mimi nlifanya nikiwa sekondari shule ya private, nlifanya kuanzia form 3 na 4 then advance nkafanya mwaka mmoja nlipata msala tofaut na huo nkafukuzwa mazima, nlimfanyia pia mdgo angu form 3 na 4 akamaliza flesh na haikuwah kugundulika

nlikua nikipewa ada lets say laki tano mim natumia si zaid ya elfu 30 kukamilisha mchakato wote . Inayobk ni bata tu, nlienjoy sanaa
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana. Lakini sehemu kama Jamiiforums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa nyumbani hautoshi kabisa. Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza. Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules.

Sem ya kwanza ikaisha, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakasonga. Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande. Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka. Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliuokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana. Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi. Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana. Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana : (

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau, na ndio hapo unapoingia mtegoni unadakwa na kila kitu kinakua kichungu.

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana??
 
Back
Top Bottom