Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Wewe ujanja ujanja umezoea nilidhani ile ishu ya risiti ingekuwa somo kwako kumbe wapi umeenda Nairobi tena kuharibu ila ndio hivyo ujana Mungu akutangulie
 
CRYPTOCURRENCY

Nimepambania kombe huku na kule Mil 3 hizi hapa. Nawaza sasa pa kuzipeleka ili mtonyo uongezeke. Mishe zilizopo mezani wakati huo zimebana sana. Kwaiyo kusema niende nikafanye kilimo au nifungue biashara mahali itakua changamoto kidogo kwenye kufuatilia.

Napita pita social media [wakati huo facebook ni moto sana sio kama saivi] nakutana na habari za kudownload pesa kwa mara ya kwanza; mambo ya cryptocurrency na forex. Nikawa interested. Nikaanza kufuatilia kwa ukaribu nikagundua kuna jamaa mmoja mkenya anasaidia watu ambao hawana uzoefu wa ku trade then baadae mnagawana faida.

Mshenzi yule alikua amejipanga. Alikua hadi ana post video za watu mbali mbali wanaotoa ushuhuda namna jamaa alivyo wasaidia na kubadilisha maisha yao. Duh, nikaona mtonyo si ndio huu sasa. Na hivi sina muda mishe kama hizi za kimtandao ndio zenyewe. Namalizia kila kitu kwenye simu. Sasa nikapiga mahesabu wale watu ninao waona kwenye clips hawakua hata na cha kuanzia kikubwa na sasahivi maisha yao yamebadilika, Je mimi mwenye Mita 3? Si ndio na kazi nitaacha kabisa. Nikaona hii ni fursa ngoja nim.dm mwamba.

Jamaa alikua Active sana. Akanitumia magazeti kadhaa ya kupitia ili nielewe namna utaratibu mzima unavyoenda. Nikayasoma yote nikawa nimeelewa. Maskini mtoto wa watu kumbe naingizwa mjini hata sielewi.

Nakumbuka alini.introduce kwenye platform moja inaitwa coinxtrading au paxel kama sikosei. Una create account unaweka details zako personal mpaka bank Account No. zako. Then kianzio cha chini ni USD 100, wakati huo ilikua kama laki 2 kasoro hivi, sikumbuki vizuri exchange rate ya siku hiyo. Mwamba nikatupia Dollar zangu 100.

Hiyo system ukishajisajili lazima umchague jamaa kama meta trader wako unayemuamini. Kwaiyo akaniambia jina la kuchagua pale nikamchagua chap kazi ikaanza.

Mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya kama siku mbili naingia kwenye system, nakuta mtonyo unasoma USD 400. Nikasema mambo si ndio haya sasa. Unaingiza Dollar 300 ndani ya masaa 48 tu, tena hata sijatoka Jasho. Ewaaa nimeulaaa huku nikicheka kitajiri. Sikujua kitakachonikuta..

Siku moja baada ya kuona ile $400, jamaa akanicheck inbox. Akaniambia mambo yanaenda vizuri kwaiyo nimtumie commision yake ya $150 maana tunagawana faida. Nikamwambia toa tu hapo kwenye hiyo iliyopatikana kwenye mfumo. Akasema niache ujinga kwa sababu nikipunguza pesa ya kwenye system itabidi nianzie chini tena. Wakati nikiacha hiyo $400 aka trade itaongezeka haraka zaidi. Akanipa ka somo nikamuelewa.

Basi nikaenda Bank nikafanya niliyotakiwa kufanya jamaa akapata pesa zake. Akaendelea kutrade.

To cut a long story short;

Kuna muda ilifika hadi $3000. Akawa ameniambia nimpe faida yake then anifanyie namna nitoe pesa zangu. Yule Mbwa sijui alinusa harufu kuwa nitamsanukia maana nilikua kama nimeshachoshwa na hizo habari za niache hela kule kwenye mfumo hadi zijae jae.

Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu ku withdraw ikawa inagoma. Jamaa akaniambia siwezi ku withdraw bila yeye kunisaidia. Kana kwamba kuna process kidgo za kupitia mpaka pesa itoke. Daah nilitakiwa nikimbie haraka baada ya kuambiwa hivyo ila tamaa zikanifanya nimuamini ki bloody fool sana.

Baada ya kumtumia commision yake ya kitu kama $1200, dana dana zikaanza. Hapo karibu hela yote ameshachukua. Nimebaki na kama laki 2 tu kwenye ile Mil 3 niliyokua nayo. Sasa akili ndio zikaanza kurudi. Alivyoona kila anavyoniletea story za kuendelea kutrade nagoma, na ninachotaka ni kuwithdraw tu pesa.. akaniblock. Sijakaa vizuri nikawa logged out kwenye system. Aiseee

Niliumia sana. Nilijuta kuamini watu ki rahisi rahisi. Nilihangaika sana ku log in lakini wapi. Tukana sana jamaa inbox lakini wapi. Pesa imekwenda na maji. Hairudi tena. 3M niliyoitesekea zaidi ya mwaka is gone tena ndani ya wiki mbili tu. Nilikua depressed sana. Nikaona hii aibu siwezi hata kushirikisha wenzangu. Nikachukua leave nikaomboleze kidogo nyumbani.

Hapa nilijifunza kitu kuhusu utapeli. Nika recover, maisha yakaendelea [emoji1491]


Ukiona unalazimishiwa sana fursa, ujue wewe ndiyo fursa yenyewe.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nmecheka balaa

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Mengi mengi mengi ....mengi mnooo....ila kubwa kuliko ni kumwamini mwanaume....na sitokoma kujuta coz bado ni mwepesi sana kumwamini mtu mapema
Kuna mtu anaisoma hii comment na kujiinamia kwa uzuni huku akisema "i wish ningepata/nipate mwanamke kama huyu"

Bado una nafasi usijari utapata wa aina yako cha mhimu ni uzima tu
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijaona kinachoweza kukufanya ujute hapa [emoji2365]
 
We jamaa fala sana [emoji23][emoji23][emoji23]
Eti "Siwezi kuingia kwenye msala kama hakuna Chambi kidogo"
 
Daaah [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekata tamaa mkuu,wanaokuja ni walewale umiza kichwa....
Kuna utumwa FULANI umeasisiwa na Dini hasa kikristo ambao ni KUFUNGA ndoa tena ndoa ya mke MMOJA tu!!!kwamba bila jicho ndoa unakua mdhambi na mnateseka kweli!!!

KWA Kuwa una kipato Chako Kuwa HURU Angalia mtu ambaye unajivunia hata ukiwa nae Karibu mtu ambae anatosha nafsini mwako na usiwe na wazo la kuvaa shela utumwa bali ukaribu ule wa KILA siku wa kushea changamoto zote hata kama ameoa wewe kama una mfeel Kuwa nae!!wala Dini sijui moto sijui ujinga GANI na presha za Maisha zisikuchanganye, mradi awe anaingia kwako na kutoka na WATU wanaona kwamba mwamba anamiliki!

Ulilelewa kelele coz ameoa we sema mi mke wa pili na fresh tu SIJALI!!!usifinyangwe moyo I na wazo la ndoa na shela wakati ubikira ulishaupoteza!!wanaofunga ndoa na sio bikra wanajidanganya kwani ndoa yao ya kweli ni ile siku wamepoteza bikra hizo nyingine ni tafrija za kula wali na picha za kwenye fremu!!!!Achana na matazamio makubwa ya uongo AMBAYO yatakuumiza usifurahie Maisha!

IMANI ZA KIDINI ZINATESA WATU SANA COZ ZIMAZUIA ASILI HALISI ZA BINADAMU NA UUMBAJI!!!!CHANGAMKA WEWE MBONA MSOMI!HALAFU UNATUANGUSHA !!!?
 
Nimekata tamaa mkuu,wanaokuja ni walewale umiza kichwa....
Kuna utumwa FULANI umeasisiwa na Dini hasa kikristo ambao ni KUFUNGA ndoa tena ndoa ya mke MMOJA tu!!!kwamba bila jicho ndoa unakua mdhambi na mnateseka kweli.

KWA Kuwa una kipato Chako Kuwa HURU Angalia mtu ambaye unajivunia hata ukiwa nae Karibu mtu ambae anatosha nafsini mwako na usiwe na wazo la kuvaa shela utumwa bali ukaribu ule wa KILA siku wa kushea changamoto zote hata kama ameoa wewe kama una mfeel Kuwa nae!!wala Dini sijui moto sijui ujinga GANI na presha za Maisha zisikuchanganye!!mradi awe anazingua kwako na kutoka na WATU wanaona kwamba mwamba anamiliki!!ukipigiwa kelele coz ameoa we sema mi mke wa pili na fresh tu SIJALI!!!usifinyangwe moyo I na wazo la ndoa na shela wakati ubikira ulishaupoteza!!wanaofunga ndoa na sio bikra wanajidanganya kwani ndoa yao ya kweli ni ile siku wamepoteza bikra hizo nyingine ni tafrija za kula wali na picha za kwenye fremu!

Achana na matazamio makubwa ya uongo AMBAYO yatakuumiza usifurahie Maisha!!!!IMANI ZA KIDINI ZINATESA WATU SANA COZ ZIMAZUIA ASILI HALISI ZA BINADAMU NA UUMBAJI.

CHANGAMKA WEWE MBONA MSOMI!HALAFU UNATUANGUSHA !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…