Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,

Wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa wewe ni kama sister tu bhanaa.

Weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA, baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kabisa.
 
Mi najuta kuwa na huyu niliye naye nilijua naondoa upweke kumbe naongeza maumivu

Ngoja nilee tu Hawa watoto
JamiiForums-382154248.jpg
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua,,,, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp
Pole Sana mkuu..Ila hao unaosema walikutumia pengine walijua ....sema hawakukwambia maana labda usingekubali.. ..
.
Ukiisha kujuta majuto ya kweli ..jua uko huru ... ..

Usijielemeze mzigo wa kuyaishi mashaka ya wenzio.. ..

Maana haikuwa lengo lako .. ...
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua,,,, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp
Angalia mkuu jinai huwa haifi hata siku moja,usiamini sana mitandao, ni ushauri tu lakini.
 
Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa ww n km sister tu bhanaa ,weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA ,,,baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kbs
Pole kwa kubakwa mkuu....nini kilikupata?
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana. Lakini sehemu kama jamiiforums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakua nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekua magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa nyumbani hautoshi kabisa. Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidgo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Basi bhana, kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza. Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwaiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules.

Sem ya kwanza ikaisha, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakasonga. Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi mlungula! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Sitasahau Kilichonitokea!!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande. Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Heheee, unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidgo kesho yake unatoka. Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality.

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikua unapeleka wapi? Uchungu niliuokua nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwaiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana. Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi. Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa!

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana. Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika tunajifunza kutokana na Makosa. Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana inatabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau, na ndio hapo unapoingia mtegoni unadakwa na kila kitu kinakua kichungu.

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana??
Hii kitu iligharimu watu pia chuo cha Iringa!
 
Asee katika vitu ambavyo tunapaswa kuzingatia na kuepuka kwenye Maisha ni kufanya kitu ambacho badae kitakufanya ujutie kwa maana Majuto uumiza sana moyo
Mkuu kuna vitu mtu huvifanya kwa ajili ya ujana tu "Ujana maji ya moto" ila kadiri umri unavyo sogea na akili kukomaa ndipo hua tunagundua kuwa lile jambo tulilolifanya kumbe ni kosa na halikuwa jambo jema.

Tujitahidi tu kulea watoto wetu na kuwafahamisha mambo gani hayafai kufanywa na yapi ya maana yafanywe,

Yaani tuwalee kwenye maadili mema.
 
Hakika mkuu
Mkuu kuna vitu mtu huvifanya kwa ajili ya ujana tu "Ujana maji ya moto" ila kadiri umri unavyo sogea na akili kukomaa ndipo hua tunagundua kua lile jambo tulilolifanya kumbe ni kosa na halikua jambo jema,

Tujitahidi tu kulea watoto wetu na kuwafahamisha mambo gani hayafai kufanywa na yapi ya maana yafanywe,

Yaani tuwalee kwenye maadili mema.
 
Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six

Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa

Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa, tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza

Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)

Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)

Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea

Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani

Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana

Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform

Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika

Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)

Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa

Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
 
Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja hivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja.

Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....

I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel naamini asingekutana na yaliyomkuta, ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako.

Kifo ni fumbo kubwa.

Tuwajali Sana wanaotupenda, life is too short.
 
Sitakuja kusahu aisee maana mie nilililelewa na mzazi mmoja bimkubwa, mshua enzi hizo mambo mengi hivyo bimkubwa akajitaa so mshua akaanzisha familia yake nyingine ambayo aliipa thamani kubwa halafu ukizingatia na mshiko mrefu wa dili zake za mbao.

Sasa bimkubwa akifight sana mpka nikamaliza chuo mwanzoni mwa 2000, mshua kule madogo walizingua wote kwenye elimu halafu kwetu hakuwa anahudumia chochote sio kwa kuambiwa ni kwa kuona kabisa, alikata networks baada ya muda mambo yakamuendea kombo hapo tayari nipo kwenye ajira.

Akaanza kunitafuta nimpe sapoti ya kiuchumi nilikuwa Nampa kimtindo bila kinyongo ila nguvu kubwa niliwekeza kwa bimkubwa, mshua akajua hilo akaenda kumkoromea bi mkubwa kuwa kwanini mie nampendelea sana yeye kuliko yeye mshua?

Hakika sintasau na hakika najutia maana hamaki niliyokuwa nayo nilienda kumuwakia mshua tena kwa facts aache kabisa kumzonga bi mkubwa ila baadae nilijutia sana maana mshua alikuwa mdogo sana hali hiyo ikapelea pressure kupanda ila Mungu ni mwema yupo poa ila alishakuwa mgonjwa mgonjwa ambapo moyoni najihisi hatia kuwa nahusika na ugonjwa wake.
 
Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja ivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja
Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....[emoji24]

I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako
Kifo ni fumbo kubwa
Tuwajali Sana wanaotupenda life is too short
Pole ilikuaje alijiua au
 
Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja ivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja
Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....[emoji24]

I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel naamini asingekutana na yaliyomkuta, ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako
Kifo ni fumbo kubwa
Tuwajali Sana wanaotupenda life is too short
Aisee.
 
Back
Top Bottom