Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six


Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa


Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)



Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)
Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea


Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani



Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana



Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform



Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika
Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)



Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa

Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
Mjita..mjita unaitwa huku
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.


Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
 
Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.

Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.

Acha kulalamika kijana, mwanaume mashine...

Njoo umasaini huku uone raia walivyo na boma ina wake na watoto kama utitiri na hakuna anaye complain
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri. Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni. Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii. Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.


Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale. Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.


Hahaha eti vinguruwe vinatoa sauti ya kukera.
 
Back
Top Bottom