Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).
Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri. Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.
Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni. Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii. Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.
Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.
Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.
Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale. Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.
Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.