Iv watoto wa kiume na udokozi vipo kwenye damu au?
Kipindi nipo form two nyumban tulikua tumezoeana sana na bibi mmoja jirani etu,alizoea kuniita mume kuanzia nikiwa primary na watoto wake walikua wakishua kimangoto hvyo nlikua nikitoka shule nikipta pale maziwa mtindi glass sikosi alaf ndo naenda home,,
Siku moja nmetoka shule kama kawaida nikapita kwake sikumkuta nikaingia chumba cha kijana wa kazi huyu alikua anachunga mbuzi wake nae hakuwepo,ndan kwake kulikua na radio flan ndogondogo kimtindo inasehem ya kanda na memory card na flash,shetani akaniambia sepa nayo hapo hata sijui naipeleka wapi,,
Nmefika home nikamkuta maza akaniuliza umetoa wapi radio nikampanga nmeiokota akasema sawa yaaan ile kiwepesi tuu na nnavyomjua mama sio wa hvyo,,bas mie nkapotezea,,
baadae nmeshasahau mama akaniuliza ulivyotoka shule ulipita wapi nikamuambia kwa bibi sijapita kwingine akasema haya nikaendelea na issue zangu,baadae akaniambia pakua ule nikamuambia ntakula (hadi leo najutaga kwann sikula muda uleule)kumbe alitoka akaenda kw bibi akauliza akaambiwa hata sisi tunatafuta radio hatuioni mama akarud akaniambia naomba urudishe ile radio ulioiba kule kwa bibi ile kiupole tuu,nikatoka nikairudisha lkn nikamwambia bibi naomba umwambie mama asinipige,bibi akampigia mama simu mama akaja pale akaniombea msamaha pale mama akasema siwezi kumchapa jaman najua aliteleza tuu,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],mama akaondoka na mie nikarud home ile kuingia ndani mama huyu hapa na fimbo kama 4 iv,mlango ukafungwa aisee nilichezea kipigo kimoja hatari sana,,alinipiga mpaka nikamuambia ujue umenizaa wewe lkn unanipiga kama huna uchungu na mm[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hapo natafuta huruma tuu,,
Btw wizi niliacha na chakula sikuweza kula mpaka kesho yake.
Sent from my SM-A207F using
JamiiForums mobile app