FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI
Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.
Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana😂😂😂😂😂 au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.
Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro🤨🤨🤨.
Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.
Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.
Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.
Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.
Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii🔥🔥🔥🔥🔥🔥.
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.
Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.
Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.
Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.
Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.
Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.
Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.