Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp.
Polee sana mkuu,kama hukudhamiria kufanya hilo tukio huna haja ya kujutia sana,kikubwa fanya sana ibada .....pia nakushauri hii story usiipandishe jukwaani watu wanaweza kufungua code kufuatana na mtiririko wa tukio.
 
FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI

Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.

Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.
Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro[emoji2955][emoji2955][emoji2955].
Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.
Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.

Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.
Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.

Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91].
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.

Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.

Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.

Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.
Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.

Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.

Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.
Duuuuuh hii story sio Tabora boys kweli? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,

Wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa ww n km sister tu bhanaa ,

Weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA ,,,baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kbs
Itakuwa alikuwa mwanaume sema unaficha
 
Iv watoto wa kiume na udokozi vipo kwenye damu au?

Kipindi nipo form two nyumban tulikua tumezoeana sana na bibi mmoja jirani etu,alizoea kuniita mume kuanzia nikiwa primary na watoto wake walikua wakishua kimangoto hvyo nlikua nikitoka shule nikipta pale maziwa mtindi glass sikosi alaf ndo naenda home,,

Siku moja nmetoka shule kama kawaida nikapita kwake sikumkuta nikaingia chumba cha kijana wa kazi huyu alikua anachunga mbuzi wake nae hakuwepo,ndan kwake kulikua na radio flan ndogondogo kimtindo inasehem ya kanda na memory card na flash,shetani akaniambia sepa nayo hapo hata sijui naipeleka wapi,,

Nmefika home nikamkuta maza akaniuliza umetoa wapi radio nikampanga nmeiokota akasema sawa yaaan ile kiwepesi tuu na nnavyomjua mama sio wa hvyo,,bas mie nkapotezea,,
baadae nmeshasahau mama akaniuliza ulivyotoka shule ulipita wapi nikamuambia kwa bibi sijapita kwingine akasema haya nikaendelea na issue zangu,baadae akaniambia pakua ule nikamuambia ntakula (hadi leo najutaga kwann sikula muda uleule)kumbe alitoka akaenda kw bibi akauliza akaambiwa hata sisi tunatafuta radio hatuioni mama akarud akaniambia naomba urudishe ile radio ulioiba kule kwa bibi ile kiupole tuu,nikatoka nikairudisha lkn nikamwambia bibi naomba umwambie mama asinipige,bibi akampigia mama simu mama akaja pale akaniombea msamaha pale mama akasema siwezi kumchapa jaman najua aliteleza tuu,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],mama akaondoka na mie nikarud home ile kuingia ndani mama huyu hapa na fimbo kama 4 iv,mlango ukafungwa aisee nilichezea kipigo kimoja hatari sana,,alinipiga mpaka nikamuambia ujue umenizaa wewe lkn unanipiga kama huna uchungu na mm[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hapo natafuta huruma tuu,,

Btw wizi niliacha na chakula sikuweza kula mpaka kesho yake.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa nyumbani hautoshi kabisa.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules.

Sem ya kwanza ikaisha, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakasonga.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliuokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau, na ndio hapo unapoingia mtegoni unadakwa na kila kitu kinakua kichungu.

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?

Drogba? Vipi mwanangu? Unaendeleaje [emoji23]
 
Kufa kupo pale pale ndio maisha ya mwanadamu....ila kwanza lazima niondoke na wengi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Usifanye hivyo mkuu. Si jambo jema. Hata kama alikuambukiza alifanya akiwa anajua wewe usifanye hivyo kwa wengine.

Life is a precious gift, usibebeshe wengine huo mzigo kwa kudhamiria.
 
yaani wewe ni mi mi kabisa mkuu-mimi jana tu nimetoka kuwakiana na mmoja hapo Bungoni....kila kitu nalipa kuanzia ada,nguo,sikukuu,chakula etc,..halafu anawapigia simu rafiki zangu eti sihudumii mtoto.

mbaya sana
Jitahidi uwe unatunza risiti zote za Ada, na hata ukituma muamala kwa simu; tunza copy yake somewhere. Hata kesho akija kudanganya kwa mtoto kwamba ulikuwa huwajibiki; unamtolea tu hizo copies.

Hizi drama nyingine; zinasababishaga hata mzazi asiwe na muda mzuri na mtoto; zaidi ya kutuma hela tu. Maana unaweza sema ngoja nipige simu nimsalimie mtoto; ila ukiwaza tu drama utakazokutana nazo; unapiga kimya.

Hizi drama zinaumiza sana watoto, sijui kwa nini baadhi ya wazazi hawataki kulea watoto kwa amani. Mtu mmeshaachana, hata ununaje hakurudii; si uendelee na maisha yako tu?
 
Usifanye hivyo mkuu. Si jambo jema. Hata kama alikuambukiza alifanya akiwa anajua wewe usifanye hivyo kwa wengine. Life is a precious gift, usibebeshe wengine huo mzigo kwa kudhamiria.
Sawa mzeya nimekusikia wacha niendelee kula mbususu liwalo na liwe
 
And Another...

Nimepambania kombe huku na kule Mil 3 hizi hapa. Nawaza sasa pa kuzipeleka ili mtonyo uongezeke. Mishe zilizopo mezani wakati huo zimebana sana. Kwaiyo kusema niende nikafanye kilimo au nifungue biashara mahali itakua changamoto kidogo kwenye kufuatilia.

Napita pita social media [wakati huo facebook ni moto sana sio kama saivi] nakutana na habari za kudownload pesa kwa mara ya kwanza; mambo ya cryptocurrency na forex. Nikawa interested. Nikaanza kufuatilia kwa ukaribu nikagundua kuna jamaa mmoja mkenya anasaidia watu ambao hawana uzoefu wa ku trade then baadae mnagawana faida.

Mshenzi yule alikua amejipanga. Alikua hadi ana post video za watu mbali mbali wanaotoa ushuhuda namna jamaa alivyo wasaidia na kubadilisha maisha yao. Duh, nikaona mtonyo si ndio huu sasa. Na hivi sina muda mishe kama hizi za kimtandao ndio zenyewe. Namalizia kila kitu kwenye simu. Sasa nikapiga mahesabu wale watu ninao waona kwenye clips hawakua hata na cha kuanzia kikubwa na sasahivi maisha yao yamebadilika, Je mimi mwenye Mita 3? Si ndio na kazi nitaacha kabisa. Nikaona hii ni fursa ngoja nim.dm mwamba.

Jamaa alikua Active sana. Akanitumia magazeti kadhaa ya kupitia ili nielewe namna utaratibu mzima unavyoenda. Nikayasoma yote nikawa nimeelewa. Maskini mtoto wa watu kumbe naingizwa mjini hata sielewi.

Nakumbuka alini.introduce kwenye platform moja inaitwa coinxtrading au paxel kama sikosei. Una create account unaweka details zako personal mpaka bank Account No. zako. Then kianzio cha chini ni USD 100, wakati huo ilikua kama laki 2 kasoro hivi, sikumbuki vizuri exchange rate ya siku hiyo. Mwamba nikatupia Dollar zangu 100.

Hiyo system ukishajisajili lazima umchague jamaa kama meta trader wako unayemuamini. Kwaiyo akaniambia jina la kuchagua pale nikamchagua chap kazi ikaanza.

Mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya kama siku mbili naingia kwenye system, nakuta mtonyo unasoma USD 400. Nikasema mambo si ndio haya sasa. Unaingiza Dollar 300 ndani ya masaa 48 tu, tena hata sijatoka Jasho. Ewaaa nimeulaaa huku nikicheka kitajiri. Sikujua kitakachonikuta..

Siku moja baada ya kuona ile $400, jamaa akanicheck inbox. Akaniambia mambo yanaenda vizuri kwaiyo nimtumie commision yake ya $150 maana tunagawana faida. Nikamwambia toa tu hapo kwenye hiyo iliyopatikana kwenye mfumo. Akasema niache ujinga kwa sababu nikipunguza pesa ya kwenye system itabidi nianzie chini tena. Wakati nikiacha hiyo $400 aka trade itaongezeka haraka zaidi. Akanipa ka somo nikamuelewa.

Basi nikaenda Bank nikafanya niliyotakiwa kufanya jamaa akapata pesa zake. Akaendelea kutrade.

To cut a long story short;

Kuna muda ilifika hadi $3000. Akawa ameniambia nimpe faida yake then anifanyie namna nitoe pesa zangu. Yule Mbwa sijui alinusa harufu kuwa nitamsanukia maana nilikua kama nimeshachoshwa na hizo habari za niache hela kule kwenye mfumo hadi zijae jae.

Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu ku withdraw ikawa inagoma. Jamaa akaniambia siwezi ku withdraw bila yeye kunisaidia. Kana kwamba kuna process kidgo za kupitia mpaka pesa itoke. Daah nilitakiwa nikimbie haraka sana baada ya kuambiwa hivyo ila tamaa zikanifanya nimuamini ki bloody f*cking sana.

Baada ya kumtumia commision yake ya kitu kama $1200, dana dana zikaanza. Hapo karibu hela yote ameshachukua. Nimebaki na kama laki 2 tu kwenye ile Mil 3 niliyokua nayo. Sasa akili ndio zikaanza kurudi. Alivyoona kila anavyoniletea story za kuendelea kutrade nagoma, na ninachotaka ni kuwitthdraw tu pesa.. akaniblock. Sijakaa vizuri nikawa logged out kwenye system. Aiseee

Niliumia sana. Nulijuta kuamini watu ki rahisi rahisi. Nilihangaika sana ku log in lakini wapi. Tukana sana jamaa inbox lakini wapi. Pesa imekwenda na maji. Hairudi tena. 3M niliyoitesekea zaidi ya mwaka is gone tena ndani ya wiki mbili tu. Nilikua depressed sana. Nikaona hii aibu siwezi hata kushirikisha wenzangu. Nikachukua leave nikaomboleze kidogo nyumbani.

Hapa nilijifunza kitu kuhusu utapeli. Nika recover, maisha yakaendelea [emoji1491]

Ukiona unalazimishiwa sana fursa, ujue wewe ndiyo fursa yenyewe.
Ila mwamba kwenye michezo ya pesa umebakisha mambo mawili. Utusue au zikutoe uhai
 
Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.

Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.

Ankol ilibidi mkeo ajue hili mapema hata kabla hujamuoa. Ili ajue tu kutakuwa na simu za baby mommas, kuna muda utakuwa na watoto wako wengine possibly wakiwa na mama zao n.k. Imagine mtu kukutamkia kuwa angejua kuwa una watoto asingekukubali.

It hurts mnoooo, maana ni dhahiri kuna muda anajuta kuolewa na wewe kwa sababu ya anayoyapitia kwa ajili yako

Weka tu mazingira mazuri ya kuwasiliana na hao wazazi wenzio. Zidi kuongea na mkeo kuwa akusamehe na mshikamane pamoja katika kuwalea watoto wako na wenu; mpeane suggestions bora za kulea watoto. Usijefanya siri kwenye kitu chochote kinachohusu hao watoto wako; itakuwa vita nyingine

Watoto ni baraka, bila kujali wamepatikana kwa wakati au mazingira gani. Sema ndiyo vile wakija nje ya utaratibu; kuna changamoto zitajitokeza tu
 
Aisee nyinyi ndo watu mlifukuzwaga chuoni kwetu, hilo dili mulikuwa mkifanya kupitia mgongo wa crdb , aisee umenikumbusha mbali, walifukuzwa wanachuo kama 10 na zaidi chuoni kwetu. Pole
Hii ni MU. Hawa watu walisabanisha turudishwe benki kulipia mia mbili halafu tusubiri siku nzima kupewa risiti yani
 
FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI

Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.

Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.
Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro[emoji2955][emoji2955][emoji2955].
Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.
Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.

Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.
Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.

Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91].
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.

Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.

Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.

Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.
Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.

Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.

Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.
Hii sio singida,ilongero?
 
Nakumbuka angali nipo kidato cha tatu mim na rafiki angu tuliwapiga Stiki madogo wa Form 1 sasa kamoja kaka zimia Pale pale
na bahati mbaya mwalim nae anatokea kule Chimbo basi tuka kimbia Tukasepa zetu kijj jirani

Tukakaa pale kijjn siku tatu uko shule tunatafutwa kesi ilibidi iende polisi lakin mkuu wa shule tumekutana kabila moja akaliziwia pale tukaenda shule kujisalimisha wenyewe Tumekuta walimu wanatusubiri kwa bashasha Basi pale kengere ikagongwa wanafunzi wote wakafika paredi.

Tukapewa suspendi mpaka bod ikutane ikae balaza iamue basi tukaaa kitaani na mwanangu yule kurudi home jau inabidi tukapige vibarua kulima songea aridhi ngumuAisee nilijuta sana tulitegemea mkuu atuite lakini wapi mwaka mzima uku wazee hawana taarifa mwezi wa kwanza inabidi turudie darasa Mwenzangu akakataa akawa anafanya mishe zake mimi nikaamia shule nyingine jiarani ilikuw
a 2011 iyo Yule mwanangu sana saizi ametangulia mbele ya haki Rest easy Rasta.

Baaada ya kuamia ile shule jirani sasa angali nipo kidato cha nne nikapata mwanangu mwingine ten mbishi na muhuni alikuwa anagombea dem na Ticha akataka wapigane sasa mimi nliingilia ule ugomvi na kutaka kuchoma nyumba ya yule mwalimu alikuw makamu mkuu wa shule ,

Yule jamaa alipigana na mwalimu mim kosa langu kuingilia ule ugomvi ilikuwa usiku wanafunzi wengine wapo prepo sisi tunapigan bombani na yule mwalimu kesi ile ilienda adi kw mkuu wa shule nikapewa tena pendi nije siku ya mtihani wa taifa ilikuwa mwezi wa 5 iyo nilkaa ad mwezi wa kumi lakin sikwenda home nilibak hapo hapo kijjn ad mwez wa kumi nimepiga sana boda boda hadi nikapata zero pro max mtihani wa mwisho.. utoto ulitusumbua sana.
 
Japo nimewahi isoma kule ila nimecheka kinoma aisee. Maombi tu ni like ombi la baba yako kwamba Na wewe utazaa lisikurudie aisee maana kuiba nguruwe Na kelele zote zile. Wewe ni kiboko
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri. Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni. Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii. Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.

Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale. Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
 
....hakika.
Jitahidi uwe unatunza risiti zote za Ada, na hata ukituma muamala kwa simu; tunza copy yake somewhere. Hata kesho akija kudanganya kwa mtoto kwamba ulikuwa huwajibiki; unamtolea tu hizo copies.

Hizi drama nyingine; zinasababishaga hata mzazi asiwe na muda mzuri na mtoto; zaidi ya kutuma hela tu. Maana unaweza sema ngoja nipige simu nimsalimie mtoto; ila ukiwaza tu drama utakazokutana nazo; unapiga kimya. Hizi drama zinaumiza sana watoto, sijui kwa nini baadhi ya wazazi hawataki kulea watoto kwa amani. Mtu mmeshaachana, hata ununaje hakurudii; si uendelee na maisha yako tu?

anasema ni lazima nisiwe na amani-atakuwa ananichafua
 
Ninachojutiaa ni 2016 dem mmoja hv sister aliniombaa niendee kwakee nikamsaidiee kufungaa kitandaa chake alinunuaa ,nikaendaa bhanaa kilichonikutaaa baada ya kufungaa kitandaa nikaanza kupigishwa story za hapa napale wkt nataka kusepaa akaniambia unaondokaje ujanywa hata soda c ndio akaletaa coca na wine bhanaaa tukaanza kunywa hapo ilikuwaa mida ya saa nne asubuh cku ya jpili huku tunapiga story ,maraa akasemaa ngojaa aandaee breakfast bhanaa bhanaa breakfast ikajaa tukaendeleaa na winee nikamtaniaa ,

Wine aipandi bhanaa nifanyie mpng wa safari mbili kubwaa nikampaa ten afate dukani akakataa akasemaa nisijali ataninuliaaa bhanaa akafata safar akaja nazo ,yy nikamwachia wine [emoji485] mm nikaanza kunywa safari mdg mdg tu ,baada safari zikakoleaa na dem wine ishamlegeza macho full kujichekeshaa tu mwishowee nikatakaa kusepaa ndipo dem akaniambia JIONGEZE nikamwambia hapanaaa ww n km sister tu bhanaa ,

Weeee akakimbilia mlango akafungaa na funguo akachomoaaa bhanaa bhanaa akawaa sasaa ananitaka tuduuu wt uku akiongeaaa mambo mengi na jinc anavyonizimiaaa tokaa cku aliponionaaa mtaani kwangu tokaa ameamia akaona mm ndio mwanaume namfaaaa bhanaa ajaongeaa mengi mwishowee ALINIBAKAAA ,,,baada yakubakwaa na yulee dem ckutegemeaa kbs kilichokujaa tokeaa maishan maana nawaambiaaga watu nilibakwa na mwanamkeee hawaamini kbs
Daah ulizingua sana Mkuu,vipi ulirudi tena kwa mara nyingine kufanya kweli ili kufuta hiyo dosari?
 
Wajuba mimi sintokaa nisahau kipind nasoma O level ilikua form 3 kama sikosei shule ilikua ya day....
Kuna Mdau mmoja kitaa alikua anataka vipande vya nondo kutokana na pale shule kulikua kuna gorofa afu kashanitangazia dau kwa hio ilitakiwa nichukue zile za kusukia nguzo..
Sasa nilikua na kawaida ya kutoroka shule na tulikua na teacher mmoja mpare alikua second master mnoko kinoma noma na mateacher wa enzi hizo walikua wanatutembezea mboko balaa...
Sasa ile nimeenda nikabeba vipande vyangu vine vya nondo nikawa nakatiza njia ambayo ipo karibu na toi za mateacher mara paaap bin Vup yule mpare Huyu hapa mbele yangu.. Akaniuliza unapeleka wapi hivi vipande? Dah nilihis mkojo unatoka huyo akanipeleka hadi kwa headmaster.. Nikampiga kiswahili headmaster hanielew... Duh sitakaa nisahau yani mikono jasho mdomo kigugumizi mate mazito mdomoni
akaniambia njoo kesho na mzazi afu dingi kavu kinoma yani unataman usiingie anga zake anakupiga kama punda na haangalii pa kupiga..
Kesho yake sikwenda shule wala sikumwambia baba nikaamka mapema poriniii... nikawa narud ucku..
Kiufupi kilichonisaidia yule headmaster alianza kuugua na mkewe akafa akawa yuko bize kulea wanae ila shuleni niliishi kama digdigi mbele ya simba pared hupatamani class asiingie headmaster so niliuskip msala kwa utoro na mwisho nae alikufa kwa ajali ya basi pale Wamii ila bada ya mm kumaliza shule ..
Daaah!pole kwa watoto wao!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom