Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Aise nikimkumbuka yule mwanamke naishia kujuta kwa nini nilimgegeda siku ile....ndio safari yangu ya arv ilipoanza[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Really!? Pole Sana chief [emoji849][emoji20][emoji20]
 
Pole ya nini tena wakati nilichokuwa nakitafuta nimekipa....haiwezekani upende uzinzi alafu ukipata ngoma ushangae
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119]
 
Najutia siku nilikua airport mtu akaomba nimsaidie kubeba mzigo kuleta Dar nikapewa mlangoni, kumbe ilikuwa ni poda. Shukuru kipindi iko airport hawajaweka scanner ya wanaofika.
Siku hizi Nina principle moja tu,sibebi mzigo wowote nisioujua hata kwenye daladala...Mambo ya nishikie, jibu langu Ni straight "No"
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp.
Kha!kha!,Uliua?,Dah!!,Lkn MUNGU wetu ni mwenye huruma sana,ukitubu atakusamehe.
 
Hamna ukawaida joo....acheni uzinzi. Msiniige... Mie mwenzenu safari yangu ya six feet under nilishaianza so bora muchukue tahadhari kabla ya ajali mliobakia
Waliokufa na ajali pale Moro na gari la Ahmed walifikia 30 baadae afu nasikia wote walikuwa -ve.Nadhani umenielewa.Ila ushauri nimeupokea mkuu
 
Kisa cha tatu......
Nilimaliza form four , nikafaulu kwenda advance mkoa fulani kwa division 1 , basi ndugu zangu kwa kunipenda na ukizingatia nililelewa na ndugu zangu upande wa mama , sababu ni yatima since then .

Ndugu wakaomba nisome dar nisiende mkoa niliopangiwa sababu ya hali ya kuhisi nitakuwa mpweke , dah walinipenda wajomba sana , basi ikatafutwa shule dar , mwisho nikapatiwa shule pale kimara mwisho, shule ya seminari chini ya dini ya Lutherani , dah na huku ni muisilamu , ila haya yote yalifanyika sababu upande wa mama huku ni wakiristo.

Ile hali sikupenda ila nilikubali kwenda tu maana hata msikitini sikuwahi kugusa, nikawa sina namna ila hiki kitu kilinifanya nianze kuona kweli bila wazazi hakuna haki, hivyo nikawa ni mtu napenda sana haki kwa yoyote hata kama hayaniusu ila tu haki ya mtu inavunjwa nilijihisi ni mimi.

Basi ile hali ya kupenda haki kwa yeyote mbele ya macho yangu ndiyo ikawa ni falsafa yangu, hakika mtu alikuwa akibuguziwa mbele ya macho yangu nahisi ni mimi vile .

Sasa basi ndani ya shule hii ya wanadini , nisharipoti na naendelea na masomo , nikaanza kuumizwa na mambo yanayoendelea pale shule, Ada tunayolipa ila haiendani na huduma tunazopata, kuanzia chakula na hata mazingira ya shule yenyewe, ila hata ratiba ya chakula haizingatiwi .

Dah nikajikuta nawaza ni vipi najikwamua na hili kwa kuitetea jamii ya wanafunzi wenzangu , dah nikaanza kwa kugombea ukaka mkuu hapo shuleni ila umri wangu , na pia umbile langu , vikaninyima ukaka mkuu , maana niliwaza ndiyo njia pekee ya amani ningeweza kukaa meza moja na walimu ili tuyajenge .

Basi walimu kwa udhubutu wangu wa kugombea wakaamua nipewe tu cheo cha kiongozi wa nidhamu , maana nilionekana mpole sana kumbe sio kweli mimi ni mpole wa sura ila mwingi wa fikra na hasira ukizingua.

Nikaanza majukumu yangu kama kiongozi wa nidhamu ila ndiyo nikaja kugundua ile shule mbali na kuwa ni ya dini ila imejaa ukabila maana kuanzia juu mpaka chini ni kabila fulani , ndiyo nikajakughamua kumbe hata viongoz wa wanafunzi wote ni kabila hilo isipokuwa mimi na jamaa mmoja kutoka kagera .

Basi miaka ilikata nikimaliza kidato cha tano , kuingia kidato cha sita , ndiyo jamaa yangu mmoja pale shule akaniita na kuniambia kuwa hawa walimu ni waoga sana, hivyo tukiamua kusimama mimi na yeye kupinga ujinga na ubwenyenye wote pale shule watapoa na watu watapata haki zao .

Nikamuuliza ni jambo zuri ila kwa njia ipi ni hapo akanipanga kuwa atajitaidi aombe ruhusa mwisho wa juma ili aende kwao , achapishe karatasi nyingi zenye orodha ya mambo ambayo sio Sawa yanayoendelea pale shule na akizileta mimi kazi yangu ni kuzisambaza usiku ili kupima upepo wa walimu wataamua nini?.

Basi kweli mwisho wa juma , alifanya hivyo na aliporudi alikuja na hizo karatsi zimeandikwa shida zote pale shuleni na vile ada tunayolipa ilivyo kubwa na mwisho akaeleza na baadhi ya vifungu vya haki zetu kupitia katiba na vile ni kipi kitafanyika wasipokuwa tayari kutusikiliza kupitia hizo , karatasi zetu .

Dah aisee , kulingana na makubaliano na jamaa yangu , huyo kwake alikuwa kazi kamaliza ilikuwa ni mimi nifanye kazi ya kuzitapanya zile karatasi eneo lote la shule.

Kweli siku ile baada ya kunikabidhi nilimuambia alfajiri ya jumatatu, nitafanya hiyo kazi na hatoamini .Kweli usiku wa jumapili , mida ya saa nane usiku , niliamka na kuchunguza walinzi wote wamelala na shule iko kimya sana .

Nikaanza kazi yangu kwenye milango ya wachungaji, madarasani, assemble, na kila kona baada ya hapo , nilirudi bwenini nikalala na asubuhi kwa kuwa nilikuwa kiongozi sikuijari kengele ya morning preparation, niliendelea kulala ndio nikasikia kengele ikigongwa kuwa ni dharura.

Haraka nikawahi assemble ndiyo nakuta wanafunzi wamebeba hizo, karatasi na walimu pia kila mtu haelewi ni nani kafanya vile .

Katika zile karatasi mimi na rafiki yangu kuna jina tulijiita ila kwa ajiri ya kuficha identity yangu sitalitaja .

Kabla ya kufikia maamuzi haya nilijithidi sana kuwahimiza viongozi wenzangu kuhusu haki za wanafunzi wenzetu ila hawakuwa upande wangu hata kidogo .

Hivyo baada ya mambo hayo wengi walinishuku japo hawakunitaja, ilipigwa kura ya siri kwa unaemdhania ila bado sikuwemo .

Mwisho hiyo wiki ilikuwa wiki ya vikao vya walimu na maaskofu na wachungaji , na hitimisho huduma zikarudi kuwa nzuri kuendana na Ada ya wanafunzi .

Ila baadaye jamaa tulieshilikiana naye aliuza ramani kwa rafiki zake wengine , na ile shule ilikuwa na vitoto vipelelezi vya walimu , hivyo wakazipata habari ila yeye kwenye story alijisema yeye tu basi alipoitwa na walimu alikiri ndiyo huko akanitaja na mimi .

Ila nilivyoitwa kuhojiwa nilimkana sana mpaka wakaniamini, jamaa mwisho alifukuzwa shule.
Kiukweli niliumia ila mwisho nikasema hakuna zaidi ya kifo kwa msaliti.

Ila baada ya mimi kuhisiwa hivyo basi na uongozi nikavuliwa nikaanza , kuandamwa na kesi kibao mara nina wasichana o_level na advance , yaani ikapandwa chuki dhidi yangu kwa wanafunzi , nikawa ni mtu mpweke sana , wanafunzi mda mwingine wakaanza niona mimi ni spy wao na walimu wakawa wananiona adui wa maendeleo ya shule .

Hatimaye muda ulifika nikahitimu kidato cha sita ila ile shule mahafali hufanyika kabla ya mtihani wa necta , hivyo tulifanya mahafali ila mimi sikumuita ndugu yeyote hivyo nilikuwa alone pia .

Dah kilichoniumiza katika mahafali yale kuna masomo na baadhi ya vitu nilistahili kupewa zawadi mimi maana nilkuwa bora mbali na harakati zangu ila bado nilinyimwa mpaka cheti cha kuwa niliwahi kuwa kiongozi sikupewa pia .

Mwisho nilimaliza nikaondoka zangu pale ila najuta kufanya vile japo niliwasaidia wanafunzi wenzangu ila niliishi kama niko jela nilitengwa na kila mwanafunzi pale shuleni .

Nawamiss sana walimu wangu japo shule ishaanguka kimasomo na kimuundo ila nawakumbuka sana na wanafunzi wenzangu nawamiss pia japo hamkujua shujaa wenu alikuwa nani? Ila ni yule mliyemtenga na kumsimanga sana .
 
VISA NI VINGI,ILA ACHA NIANZE NA HIKI...

Ni 2010's niko form 4 shule ya kata hiyo mkoani Iringa huko. Nilikua mtoro sana,yani nikisema mtoro ni mtoro kweli. Kwa week naweza kuhudhulia shule mara mbili tu,siku nyingine zote nashinda Samora pale katika maroli ya mchanga,mawe fofali,n.k tunasubiri kazi za upakiaji. Au nakua Isakalilo nachimba zangu mchanga au mawe.

Licha ya mahudhulio yangu kuwa mabaya,ila walimu wengi wa ile shule walikua wananijua,haswa Headmaster. Huyu alinijua kwasababu alinisaidia sana kipindi naingia pale form 1.(Hili nilieleza katika ule uzi wa "Msoto")

Tatizo lilianzia hapa.Siku moja bila hata kutarajia alikuja ndugu yangu mmoja wa karibu kabisa akanichafua sana pale shule,wakati huo nimewekwa mtu kati ofisi za Walimu. Yani aliongea mambo mengi sana,kutokana nae ni mtu mzima na ana mwonekano wa busara busara! Basi walimuamini 100%.

Alisema mimi mhuni(Kibaka),MLEVI sana na nakunywa Ulanzi sanaaa! Nashinda na wahuni, sina nidhamu hata kidogo,n.k,n.k. Wakati huo kumbuka sijawahi kuishi nae tangu namaliza standard 7 huko,nikitelekezwa nikawa naishi tu kama mtoto wa mtaani. Nilikua Chokoraa ambae shule niliipenda ila nilikua nashindwa nijigawe vipi,huku nihudhurie shule au nitafute hela ya kula.

Basi ndugu zangu tuendelee, Headmaster na wale maticha hawakutaka hata kunipa nafasi nijitetee, na hata wangenipa nafasi ya kujitetea sidhani kama ningeweza,nilikua nacheka cheka tu kwa hasira. (Mimi nikikasirika sana huwa natabasamu sana na kakicheko kwa mbaliii).

Kama unavyojua shule zetu za kata,mimi nikadhani yanaishia pale,ajabu yule ndugu yangu akaamuru nichapwe viboko hadharani. Ikagongwa kengere pale,wanafunzi wakakusanyika pale,nikachafuliwa sana pale assemble,daah yani chafuliwa sanaaaa! Muda huo mimi hasira zimejaa level yake ila tabasamu limejaa usoni halikauki,ndio nilivyo.

Kama unavyojua wanafunzi, mashtaka yalikua kibao,ila points za msingi walizochukua ni "Mimi Kibaka" na "Mlevi,nakunywa sana Ulanzi".

Daah wakawa wananitania sana kila nikienda shule katika zile siku mbili zangu za week, nikawa nahisi karaha,basi nikapunguza mahudhulio kutoka siku mbili mpaka siku moja kwa week au siendi kabisa.

Basi kuna siku nikaenda shule ni kipindi tunakaribia kufanya mtihani wa Mock, Headmaster akaniita Ofisini. To be honest sijawahi kwenda shule nikiwa na "Majagi" kichwani,ila siku hiyo nilikua Majagi haswaa,ila nimekula majani ya mti wa limao ili kuzuia harufu. Daah kufika ofisi ya Headmaster si akaanza kunikumbushia yale ya siku zile,akawa kama ananisimanga na ule msaada ambao alinipa kipindi naanza form 1.

Siwafichi uvumilivu ulinishinda,nikawa natetemeka kwa hasira yule mzee yuko mbele yangu kakaa anaendelea kutema shombo zake. Nikagonga meza kwa hasira "Kaa kimya wewe mzee",...aah mzee akajaa upepo baada ya kuona kama namchimba mkwara,si akasimama tukawa tunatazamana ila yeye yuko upande wa pili wa meza.

Aisee! Nilimpa ndonga (Kichwa) moja matata sana mpaka akajikuta kakaa chini bila kutarajia,alafu kimyaa!. Nikajua nimeua wakuu,ila nikavaa roho ngumu nikatoka mle ndani kama hakuna kitu kimetokea,nikatimkia mtaani.

KITU NAJUTIA
Ni kumpiga kichwa mtu ambae anakaribiana na babu yangu. Yani najuta sana.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji119][emoji119][emoji119] vijana wa hovyo everywhere
 
Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.

Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ni kweli aisee inakera
 
[emoji2]
Ulitokea mgomo shuleni na umeme ulikuwa umekata wana wameenda kumtia adabu headmaster mimi nikaamua kujificha bwenini nkalala deka la juu, maana mshua aliniasa mambo ya migomo nisishiriki sisi ni masikini.

Ebwana eeh majamaa wameenda wakakuta headmaster kakimbia wakaona waje kuzimalizia hasira kwa waliolala bwemi waliokataa kugoma aisee

Bwemi la mbele kuna wanawakadakwa wakaanza kushambuliwa kwa bakora huku wengine wakivunja vioo,

Nilijikuta tuu nipo sakafuni natimua mbio kuelekea kwenye shamba la mahindi, kumbe kuna mmasai na wenzake walikuwa mle ndani nao nilishangaa wameibuka kama mizimu tunaongozana kwenye mahindi

Ikawaje sasa hujamalizia
 
Back
Top Bottom